Mjikumbushe Mzumbe High School

Mjikumbushe Mzumbe High School

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,548
Bila shaka Wana Mzumbe mpo hapa JF, nimetumwa kuwakumbuka wafuatao John Mongela, James Bwana, Michael Thomas Sebastian Sarota, Hassan Rajab Hassan, Patrick Maleva, Anderson Segereti, David Black, Obed Mwakitalika, Clement Mwashambwa, Kwela Mgaya, Theophil Alexander, Njaule Mdendu, Johnson Jasson, Sollomon Shati, Obed Msenga, Charles Nakembetwa, Gideon Mandesi, Isaac Kassanga, Dereck Kassanga, Deus Changala, Timilai Sheshangali, Shemaghembe Ntulwe, Sainet Katulunga, na wengine wengi sana. Waliosoma pale mmeombwa kuongezea majina ya wale mnaowakumbuka.
 
Nje kiduchu kwa mchomeko, wale wa Sengerema,Bwiru,Nsumba,Ihungo,Kahororo,Tabora Boys,Kantalamba,Moshi Tech,Old moshi,Tosa boys,kasino Mkwawa,SHYCom,Kibohehe, na kule abroad Zenji mpo?
 
Duh, hivi Shema yupo wapi? nilikaa nae pale Mkwawa namba mbili hahaha loooooooooooooooooongtime, jamaa alimaliza form six mie nikiwa form one first term (1991)...was a very nice guy, mgosi wa kaya mwenzangu na alinipa michongo ya ku-survive pale Uzumbeni.

Ndio kusema ulikuwa darasa moja na kina Khamis Mwisongo??? Long time, hivi Tabu Samike yuko wapi siku hizi?
 
Babu, na mimi nipo ktk hilo kundi Mtweve, MD. wanaomkumbuka MOHAMED KISERA, naomba unipe kontakti zake plse. Nimepanga vakesheni ya kwenda kutembea MZUMBE wiki ya pili ya Decemba, na nitatembelea pia sehemu niliyokuwa nazamia msosi pale IDM.
 
Yap, darasa moja form 1-4!! Tabu mara ya mwisho nilimuona Mwanza mtaa wa Uhuru na rafiki yake Seba wapo njwiiiiii (hiyo ilikuwa mitaa ya 1997)......zaidi ya hapo sina ze dataz!!

Duh si mchezo, Lile darasa lenu nilikuwa naliadmire sana.
 
Babu, na mimi nipo ktk hilo kundi Mtweve, MD. wanaomkumbuka MOHAMED KISERA, naomba unipe kontakti zake plse. Nimepanga vakesheni ya kwenda kutembea MZUMBE wiki ya pili ya Decemba, na nitatembelea pia sehemu niliyokuwa nazamia msosi pale IDM.

ee bwana uko wapi siku hizi wewe?
 
Munaboa,ili mrabi mimi ni member mzuri wa mzumbe lakini siwaungi mkono kwa maana hakuna cha maana munachotukumbusha,hata Afande sele alisema mwimbo gani munatajataja majina munachoongea hakina maana,kama munataka mambo ya maana fanyeni mavituzi ili ije siku watu wakisikia then waseme hawa ndio wazumbe.
Tatizo elimu ya Tanzania ilikaa kwa kubebabeba mno ndio maana hao watu waliotokea huko Mzumbe,Ilboru,kibaa na kwingineko huku sioni cha maana wanachokifanya.
Jamani elimu sio kufaulu au kuwa TO bali ni nini unakifanya,Nimekaa mzumbe na ninawajua wazumbe ambao walikuwa vipanga ila sasa sioni wanachokifanya especialy wale walioenda nje sehemu ambazo watu wanapima kipaji sio ukaliliji wa pepa za Mungai ambazo wibo tayari kashalikisha 80%.
Nakumbuka kipindi tunamaliza kuna ile kumi bora yetu ya kitaifa,hao watu waliochukua kumi bora,jamani...Elimu ya Tanzania bado ni tete na imekaa kubeba mno.
Naomba watupe kamuda kadoogo mno tuje tuprove kuwa sio wote walioko special ni vichwa bali ni idadi ndogo mno kati yao.
Kumbuka tunaposema Special student tunahitaji ubunifu na si kiwango cha kubeba na kuja kushusha kwenye mtihani.
 
Sawa, watu wanajaribu ku-socialize, huwezi kuanza from nowhere thread imeanzishwa hapo hapo mmeanza kuongelea proteonomics! Una point kidogo lakini chuki binafsi imekuzidi- kama 'ulifeli' shauri zako na makarai au ma-D yako.
 
Mkuu kama mimi ningepata hayo ma D basi nadhani Tanzania nzima ni wachache mno ambao wangepata hata F kama si -F,mimi ni mwana mzumbe mmojawapo na mkeleketwa mmoja,ila huwa napenda kusema ukweli pale kwenye ukweli,sasa kama kila shule italeta tujikumbushe si JF yote itajaa Tujikumbushe??(Nadhani umeshaona kazi iliyoanza)
Sisi wazumbe ni wasomi na tunajiita ni vichwa,je tumeshidwa kutafuta njia ambayo itatuweka pamoja na kuitangaza shule yetu zaidi ya mithread ya hapa ambayo punde tu admin ataiban?? Nilikuwa natoa changamoto kwa wanamzumbe,ila pia sipendi hii ya kutajataja majina ya watu eti mutumie hapa kujifagilia,si bora mungeniletea story ya Virei au nyuji ya shangazi au hata mambo ya mongwe ningewaelewa? mungetaja majina ya watu muhimu ambao wanawahusu wote kama Kinunda,Mzee Mwasha,Baba Wibo nk bila kusahau mambo ya Planet,Jidi au Fede hapo tungekuwa wote.
Ushauri.Tujaribu kutafuta njia ambayo itatuweka pamoja bila ya kubughudhi au kuwakera wengine,stay tuned nipo njiani kudesign kitu ambacho kweli kitafanya kazi na watu mutakiappreciate,ndani ya wiki mutayaona matunda ila sitaki mambo ya kutajataja majina kwani misifa mingi ilikuwa kutokana na Elimu dume.
Nawakilisha toka Duolojie.
 
Munaboa,ili mrabi mimi ni member mzuri wa mzumbe lakini siwaungi mkono kwa maana hakuna cha maana munachotukumbusha,hata Afande sele alisema mwimbo gani munatajataja majina munachoongea hakina maana,kama munataka mambo ya maana fanyeni mavituzi ili ije siku watu wakisikia then waseme hawa ndio wazumbe.
Tatizo elimu ya Tanzania ilikaa kwa kubebabeba mno ndio maana hao watu waliotokea huko Mzumbe,Ilboru,kibaa na kwingineko huku sioni cha maana wanachokifanya.
Jamani elimu sio kufaulu au kuwa TO bali ni nini unakifanya,Nimekaa mzumbe na ninawajua wazumbe ambao walikuwa vipanga ila sasa sioni wanachokifanya especialy wale walioenda nje sehemu ambazo watu wanapima kipaji sio ukaliliji wa pepa za Mungai ambazo wibo tayari kashalikisha 80%.
Nakumbuka kipindi tunamaliza kuna ile kumi bora yetu ya kitaifa,hao watu waliochukua kumi bora,jamani...Elimu ya Tanzania bado ni tete na imekaa kubeba mno.
Naomba watupe kamuda kadoogo mno tuje tuprove kuwa sio wote walioko special ni vichwa bali ni idadi ndogo mno kati yao.
Kumbuka tunaposema Special student tunahitaji ubunifu na si kiwango cha kubeba na kuja kushusha kwenye mtihani.
Well well man wangu.......ma TO nawaona ovyoo sana kazi hawajui material hamna kichwani i could say that walikuwa wanakariri as Wibonele(nimem miss Wibo) alivyowalikishia pepa......Nani asiyejua mzumbe wanapewa pepa(maswali) kabla ya mtihani.Kuna To mmoja nilienda nae sehemu fulani alikimbia akarudi Bongo kwenye elimu ya kukariri.
 
Munaboa,ili mrabi mimi ni member mzuri wa mzumbe lakini siwaungi mkono kwa maana hakuna cha maana munachotukumbusha,hata Afande sele alisema mwimbo gani munatajataja majina munachoongea hakina maana,kama munataka mambo ya maana fanyeni mavituzi ili ije siku watu wakisikia then waseme hawa ndio wazumbe.
Tatizo elimu ya Tanzania ilikaa kwa kubebabeba mno ndio maana hao watu waliotokea huko Mzumbe,Ilboru,kibaa na kwingineko huku sioni cha maana wanachokifanya.
Jamani elimu sio kufaulu au kuwa TO bali ni nini unakifanya,Nimekaa mzumbe na ninawajua wazumbe ambao walikuwa vipanga ila sasa sioni wanachokifanya especialy wale walioenda nje sehemu ambazo watu wanapima kipaji sio ukaliliji wa pepa za Mungai ambazo wibo tayari kashalikisha 80%.
Nakumbuka kipindi tunamaliza kuna ile kumi bora yetu ya kitaifa,hao watu waliochukua kumi bora,jamani...Elimu ya Tanzania bado ni tete na imekaa kubeba mno.
Naomba watupe kamuda kadoogo mno tuje tuprove kuwa sio wote walioko special ni vichwa bali ni idadi ndogo mno kati yao.
Kumbuka tunaposema Special student tunahitaji ubunifu na si kiwango cha kubeba na kuja kushusha kwenye mtihani.
watu kukumbuka good old days sio vibayaa. mimi sikusoma Mzumbe ila kuna washkaji zangu wa karibu niliokutana nao high school waliotokea Mzumbe walikuwa good people na wanasimulia kwamba wali-have fun sana huko, sasa kama wewe hayo yalikuwa yanakupita acha ku-hate. Kusimuliana yaliyopita sii mbaya na kila mtu anapambana na future kivyake, whether ka-make it or not yote maisha.
2974d1227768266-mjikumbushe-mzumbe-high-school-afande.jpg
 
watu kukumbuka good old days sio vibayaa. mimi sikusoma Mzumbe ila kuna washkaji zangu wa karibu niliokutana nao high school waliotokea Mzumbe walikuwa good people na wanasimulia kwamba wali-have fun sana huko, sasa kama wewe hayo yalikuwa yanakupita acha ku-hate. Kusimuliana yaliyopita sii mbaya na kila mtu anapambana na future kivyake, whether ka-make it or not yote maisha.

Wewe una utani na baba nanihii wa Houston,TX. Anzisha thread ya Mkwawa tuwachane.
 
...Mzumbe was a good school na memory kubwa ni manyapu wa kilakala na basketball viwanja vya IDM mzumbe,ila lile dongo jekundu na ngama la mama masikio kwenye ndabuli nalo is somethin to remember...nakumbuka kuna teacher mmoja matekele alinipa adhabu ya kuchunga ile ming'ombe basi ilikuwa balaa tupu siku hiyo,niliwachapa wale ng'ombe wakapata kichaa katika kukimbizana nao wakaingia ofisi ya walimu,ilikuwa balaa tupu siku hiyo maana Chiduo na matekele kwa misifa walinishindilia mabakola yasiyo na idadi na kuniongezea mituta ya michicha ...hawa madikteta wangekuwa unyamwezini lazima ningetambaa nao,btw nilikua pale early 90's (Karume village).....tuendelee...
 
Nakumbuka Jaji Makaramba alisoma pale na alikuwa kiongozi wa Mahanga ya Shaaban Robert na nakumbuka akiwa kidato cha sita niliwahi kumpa Shikamoo kwa sababu enzi hizo fashion zilikuwa ni Bugaluu, na Tinaboo zilikuwa ni kwa ajili ya Wazee na walimu, baada ya kuona amevaa hivyo nikajua ni mwalimu. Pia alikuwa mtunzi mzuri wa michezo ya kuigiza kama vile Mafupa - The revenge of the skeleton. lakini hii ni longi ago.
 
Mzumbe sekondari ilikuwa poa sana. Mimi nilikuwa hapo 1990-92, Mkwawa.
Listi ni ndefu sana ya walipitia hapo miaka hiyo..hii ni kabla haijawa special school!!
 
Mi nimepita si mbali sana,2000-2002.Hakuna ng'ombe tena.Yale mabanda ya nguruwe kule chini kwenye machungwa ndo ilikuwa sehemu ya wasiopenda kuonekana wanasinzia darasani kusomea.Mie mmojawapo.Mama masikio hadi naondoka bado alikuwepo,ila Wibonele ndio alifariki.Matekere alikula masters pale IDM,sasa ni Lecturer Mzumbe university.Mikwala ile ile bado ipo,ukifika unaonyeshwa kitanda chako alafu unaambiwa hapo jamaa aliramba 3 na alikuwa alali.
Kama kawa,wa kutoka mkoani tulikuwa tunapangiwa "Mzumbe day" Shaban Robert,ila badae paligeuka kuwa dili kwa wapenda disco IDM na watu wa msikitini.
Misamiati: Jidi-Msikitini,Nyali-wali,Ngama-ugali,Nyuji-uji,Piriton-Msinziaji darasani,Mbonji-Usingizi,Kufufuka-Kuamka usiku wa manane kusoma,Kuitafuta asubuhi-Kukesha,Salo-Mboga mboga zilizokuwa zinauzwa na akina mama,Vilei-Kilakala girls,Kilaza-Mtu asiye na shule,CG(Central of Gravity)-Mtu anayekuwa wa kwanza.
 
hivi ule utaratibu wa kula maharage kila siku bado unaendelea mzumbe au?????maana sie kule ilburu tulikuwa twapata na mbonga za majani,teh teh teh
 
Msabato mkuu umenikumbusha mbali,katika watu wote waliochangie wewe ndio umenikuna mno kwani ulivyonikumbusha mambo ya Salo hapo ndio umeniacha hoooooi.Watu tulikuwa tunagombania salo ya shangazi,akitokea tu bonge la msururu,kweli maisha tunatokea mbali.
 
Back
Top Bottom