Mji wa Dar es Salaam Vs Mji wa Maputo

Mji wa Dar es Salaam Vs Mji wa Maputo

Steph Curry

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
5,936
Reaction score
4,713
Wanajamvi kuna mmakonde mmoja wa Msumbiji ananitambia hapa, anasema Maputo imejengeka, umepangika na ina ustaarabu mkubwa kuliko Dar.. Ananiambia Dar haifikii hata robo ya Maputo kuanzia kwenye investment za majengo, hotels na beach nzuri kama Miami.. Miundombinu ya barabara pia anasema iko vizuri mno.. Pia mzunguko Wa biashara ni mkubwa kuliko dar

Jamaa kanitambia mpaka nimewish nitake a vacation there, kama kuna ambae ashafika hebu aprove kama hayo ya huyo mmakonde ni ya kweli au lah
 
Ni ukweli usiopingika; maputo zamani ikiitwa Lorenco Marques is about twice the size of bandari ya Salama; Big multi lane streets; high rise buildings, gardens kubwa kubwa; club za starehe na mahoteli mazuri mazuri; street lights kila kona;
Wareno waliujenga kama nyumbani kwao kwa kudumu; hawakutarajia kuondoka; slum dwellings na malundo ya takataka mjini vimeanza kuonekana katika miaka ya karibuni; si unajua utawala wetu huu wa kibongo bongo!

Visit maputo, it will be money well spent; hautajuta hata kidogo
 
Dar is the worse city in africa. nimetembeatembea kidogo ....dar in aibu...!!! Nenda tu hapo kigari rwanda ushangae..!!!jamaa wamepigana vita ...ila saafii...!!
 
Maputo hiyo.
 
Attachments

  • 1411720622162.jpg
    1411720622162.jpg
    60.7 KB · Views: 1,124
Ni ukweli usiopingika; maputo zamani ikiitwa Lorenco Marques is about twice the size of bandari ya Salama; Big multi lane streets; high rise buildings, gardens kubwa kubwa; club za starehe na mahoteli mazuri mazuri; street lights kila kona;
Wareno waliujenga kama nyumbani kwao kwa kudumu; hawakutarajia kuondoka; slum dwellings na malundo ya takataka mjini vimeanza kuonekana katika miaka ya karibuni; si unajua utawala wetu huu wa kibongo bongo!

Visit maputo, it will be money well spent; hautajuta hata kidogo

Asante mkuu.. Umenichambulia vizuri kabisa, huyu jamaa ananiambia jinsi miji ya south Mozambique ilivyojengeka hawezi fananisha na mji wowote hapa Tz
 
Dar is the worse city in africa. nimetembeatembea kidogo ....dar in aibu...!!! Nenda tu hapo kigari rwanda ushangae..!!!jamaa wamepigana vita ...ila saafii...!!

Hivi tuna laana ama nin?? Sasa na sisi tujitahidi hii miji inayochepuka miaka hii tuipange vizuri
 
kuna bwana mmoja ali post thread hapa jamvini , eti Mbeya ni kama kijiji , nilimuona hajatembea ,( Maputo sijafika, ila Lusaka, Jberg, Cape Town, Nairobi) kiukweli ni heri mtu aliyeko mji wa mkoani kuliko Dar ( kwa mtazamo sanitaion, social welfare SIO fedha) ukienda miji hiyo hasa south, utajiuliza sana viongozi wetu wanashinda ulaya wanjifunza nini ? Kama fedha za mipango miji wakoloni walitoa wapi ? Kwa mfano angekuwepo mkoloni eneo la Chalinze angeshastka kwamba pale panahitaji kupawahi kabla hapajaaharibika maana bandari inajengwa kule Bagamoyo n.k .
 
Hivi tuna laana ama nin?? Sasa na sisi tujitahidi hii miji inayochepuka miaka hii tuipange vizuri

mkuu ni laana...hatuna viongozi. dar ni jiji pekee ambalo unaweza ukawasha moto wa mkaa kituo cha daladala na ukaanza kuchoma mahindi na mishikaki....!!

ukiwa ndani ya gari...barabara zote ni jalala...kila ulacho ndani ya gari unatupa nje..!
 
na mifereji ya road drainage ndio dampo ya taka ngumu na maji taka.
 
Mi naijua Maputo, ni ya kawaida tu wala tusiongopeane. Hao wamakonde wengi hawajafika Maputo, kwao ni Pemba kama wameshuka sana ni Nampula tu. Sasa we ukitegemea mmakonde akupe habari za Maputo, na wamakonde walivyo waongo vile unategemea nini?

Maputo city center ni Polana, ukilinganisha na ya Dar bado sijakubaliana na wewe kwamba city yao ni babu kubwa. Alafu unasema Lanes, sijui zimejengwa lini. Maputo ufukwe wa kung'aa ni Costa do Sol, wakati Dar tuna beach za kigamboni na kaskazini bado zinavutia tu.

Eti ukiniambia Dar ni chafu, sasa hiyo Maputo usafi wameutoa wapi? Labda huijui vizuri Maputo ulipita kijuu juu tu. Hayo mambo ya starehe ndio tusidanganyane, Dar unaweza kujirusha kuanzia jumatatu mpaka weekend, wakati Maputo kuna weekend nyingine labda uende machafuchafu.

Mji kama Maputo huwezi kuishi kama umezoea Dar.
 
Salamander umesema kweli,hivi uliyeleta thread hii unauhakika na unasokisema au umeamua kuwa mchekeshaji?Dar na Maputo wapi na wapi?Mji wa maputo majengo mengi ni chakavu,anzia pale Afrin Hotel ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Polana hotel (sio super market) iliyo karibu na mtaa wa ubalozi wa uingereza (ni ya kawaida tu),mji wao ni mchafu hasa centre unapotoka kituo chao cha ferry(karibu na afrin hotel),population ni ndogo,gari nyingi za made in south afrika ndo nyingi,air port ya maputo ni kama ya mwanza,soko lao la ferry ni chafu kwenye samaki wachanga,ila wanapenda raha sana na viwanja huwezi fananisha na dar,fedha yao ina thamani kuliko yetu (MITIKASI),wewe mleta thread ondoa uongo wako hapa wa kuifananisha Dar na Maputo.Kwa kukusaidia zaidi tafuta majarida ya The Economist na The African kuhusu takwimu za watu na maendeleo duniani yalivyoizungumzia Tanzania na Dar yake inavyopaa.Achana na magazeti ya udaku we mmakonde.Hahahahaaaaa!!!!!:A S 109:
 
Maputo ni kweli iko well planned na imepangika vizuri, lakini biashara ya Real Estate na Hotels huko bado ndugu yangu askudanganye kitu, Hapa Dar ukikohoa tu unataka appartment ndani ya dakika moja zinakuja apartment nyiiingi kwa bei tofautitofauti kuanzia za bei chini mpaka za juu kabisa, nenda leo Maputo ukaone mziki, Nyumba bei mbaya na hazipo, Hotels hakuna, ni South Africans naona ndiyo wamewekezawekeza na wanaendelea kujenga, Mwambie aje ajionee.
 
Salamander umesema kweli,hivi uliyeleta thread hii unauhakika na unasokisema au umeamua kuwa mchekeshaji?Dar na Maputo wapi na wapi?Mji wa maputo majengo mengi ni chakavu,anzia pale Afrin Hotel ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Polana hotel (sio super market) iliyo karibu na mtaa wa ubalozi wa uingereza (ni ya kawaida tu),mji wao ni mchafu hasa centre unapotoka kituo chao cha ferry(karibu na afrin hotel),population ni ndogo,gari nyingi za made in south afrika ndo nyingi,air port ya maputo ni kama ya mwanza,soko lao la ferry ni chafu kwenye samaki wachanga,ila wanapenda raha sana na viwanja huwezi fananisha na dar,fedha yao ina thamani kuliko yetu (MITIKASI),wewe mleta thread ondoa uongo wako hapa wa kuifananisha Dar na Maputo.Kwa kukusaidia zaidi tafuta majarida ya The Economist na The African kuhusu takwimu za watu na maendeleo duniani yalivyoizungumzia Tanzania na Dar yake inavyopaa.Achana na magazeti ya udaku we mmakonde.Hahahahaaaaa!!!!!:A S 109:

Jiheshimu mkuu au soma huo uzi vizuri..
 
Habari zenu wadau
Mimi nipo hapa Maputo tangu mwaka 2011 labda nieleze kwa ufupi kuwa Maputo ni mji ambao umepangika sana kuliko Dar es salaam ila tatizo la Maputo ni uchafu hapa Maputo yani mjini kabisa huku maeneo ya museu pananuka mikojo kila kona ukienda maeneo ya baixa ndio usisema mji unanuka mikojo msiba.
Hawa jamaa wanatuzidi plan za miji kusema kweli mitaa ya maputo ni mikubwa sana ila majengo ni ya zamani Dar kuna majengo mazuri sana ya kisasa kwa mfano hapa Maputo bado sijaona majengo ya vioo.
Slums hata hapa Maputo ni nyingi sana mfano pale mafalala, chamanculo etc pia kuna sehemu nje ya mji ila zimejipanga sana kama Matola ni mji mdogo ila umejengwa vizuri sana tofauti na Dar ukitoka nje ya mji hakuna mpangilio kabisa
Kuhisu apartments kwa kweli hapa Maputo pana apartments nyingi sana tena wabongo tujifunze kwa hawa jamaa maana after 10yrs watakua hawana slums kwa mfano pale costa de sol barabara imetanuliwa jamaa wamesogeza bahari wanajenga rod halafu ule ukanda wote zinajengwa apartments za hatari sana na shoping mall kibao asikwambie mtu.
ukizungumzia hotel kubwa hapa Maputo ni hotel Rouvuma, hotel serena Polana , hotel avenida pia kuna hotel cardoso na nyingine nimeisahau jina ipo maeneo ua baixa kule karibia na makao makuu ya mcel ukizilinganisha na za Dar kwa kweli hotel za Dar ni nzuri sana
Katika eneo la barabara jamaa kiasi fulani wamejitahidi ila nilichokipenda hapa kuna kitu inaitwa portagem ya geti ukiwa unatoka matola kwenda town ukishapita Casa branca unakutana na geti kubwa la kisasa ambapo kila gari inayopita hapo inalipa hiyo ni kwasababu barabara ilijengwa na wasouth hivo inabidi warudishe pesa zao na pia pesa baadhi ni katika maintainance ya rod hizi portagem south africa zipo ni njia nzuri sana ya serikali kupata Mapato.
Ila Maputo mpaka sasa ni nzuri kuliko Dar kwakuwa sehemu kubwa sanA imepangiliwa na slums zinapunguzwa ila ni chafu sanaa sana mara 100 ya Dar
 
Dar is the worse city in africa. nimetembeatembea kidogo ....dar in aibu...!!! Nenda tu hapo kigari rwanda ushangae..!!!jamaa wamepigana vita ...ila saafii...!!

Huu ni upotoshaji, na mimi nimenahatika kutoka toka kidogo, kiukweli Dar sio jiju baya kihivyo kama ulivyosema hapo. Narudia tena nimebahatika kutembea miji mingi.
 
Mi naijua Maputo, ni ya kawaida tu wala tusiongopeane. Hao wamakonde wengi hawajafika Maputo, kwao ni Pemba kama wameshuka sana ni Nampula tu. Sasa we ukitegemea mmakonde akupe habari za Maputo, na wamakonde walivyo waongo vile unategemea nini?

Maputo city center ni Polana, ukilinganisha na ya Dar bado sijakubaliana na wewe kwamba city yao ni babu kubwa. Alafu unasema Lanes, sijui zimejengwa lini. Maputo ufukwe wa kung'aa ni Costa do Sol, wakati Dar tuna beach za kigamboni na kaskazini bado zinavutia tu.

Eti ukiniambia Dar ni chafu, sasa hiyo Maputo usafi wameutoa wapi? Labda huijui vizuri Maputo ulipita kijuu juu tu. Hayo mambo ya starehe ndio tusidanganyane, Dar unaweza kujirusha kuanzia jumatatu mpaka weekend, wakati Maputo kuna weekend nyingine labda uende machafuchafu.

Mji kama Maputo huwezi kuishi kama umezoea Dar.
tembelea na mji wa beira pia
 
Back
Top Bottom