Mji mpya wa kisasa kujengwa Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B - Mkoa wa Mjini Magharibi .

Rais Dk. Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban, amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

Naye Waziri Shaaban alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya wananchi, ujenzi wa hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo.
IMG-20231215-WA0025.jpg
IMG-20231215-WA0027.jpg
IMG-20231215-WA0026.jpg
IMG-20231215-WA0035.jpg
IMG-20231215-WA0034.jpg
 
Mwinyi ana mindset ya kibiashara na anaibadilisha Zanzibar kutoka kwenye kisiwa cha wazawa kwenda kwenye kisiwa cha starehe duniani. Itapoteza utamaduni wa asili wa Zanzibar lakini tutegemee Zanzibar kuwa kama Seychelles baada ya miaka kadhaa
 
Katika kitu hatujawai kushindwa kwenyw kada ya ujenzi ni kwenye kuwa na picha nzuri na muonekano mzuri wa mradi!
Lakini hadi leo asilimia 90 ya miradi haifanani kabisa na kile kilicho kwenye mchoro na muonekano wa mchoro!

Nawahakikishia kabisa mradi huu ukiisha utacho shuhudia ni kituko na vichekesho……
 
Mwinyi ana mindset ya kibiashara na anaibadilisha Zanzibar kutoka kwenye kisiwa cha wazawa kwenda kwenye kisiwa cha starehe duniani. Itapoteza utamaduni wa asili wa Zanzibar lakini tutegemee Zanzibar kuwa kama Seychelles baada ya miaka kadhaa
ile Spice city project ilifia wapi?
 
Kuna maana gani ya kuita waandishi wa habari kukabidhiana mchoro wa mradi ambao bado haujaanza kabisa?
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B - Mkoa wa Mjini Magharibi .

Rais Dk. Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban, amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

Naye Waziri Shaaban alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya wananchi, ujenzi wa hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo.View attachment 2843233View attachment 2843234View attachment 2843235View attachment 2843236View attachment 2843237
Safi

Ila hizo facilities zitakazoambatana na huo Mji zinaweza kupokonya Utalii wa Mikutano kutoka Bara(Arusha na Dar) Kwa sababu kimbi zetu hazina Huduma nyinginezo kama zitakazokuwepo hapo Zanzibar.

Hongera Yao.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B - Mkoa wa Mjini Magharibi .

Rais Dk. Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban, amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

Naye Waziri Shaaban alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya wananchi, ujenzi wa hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo.View attachment 2843233View attachment 2843234View attachment 2843235View attachment 2843236View attachment 2843237

View: https://youtu.be/zFP-2vCF-Qg?si=Rh5z0sBlnyrDTvkG
 
Back
Top Bottom