Mji huu jimbo la Oregon Marekani unauzwa $3.8m

rr4

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
3,332
4,649
  • 16 Machi 2017
Mshirikishe mwenzako
_95159395_tiller1.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Mji wote wa Tiller, katika jimbo la Oregon nchini Marekani unauzwa, bei yake ikiwa $3.8m (£3.1m).

Mji huo unapatikana eneo ambalo halina watu wengi ambalo lipo umbali wa kilomita 362 kusini mwa mji wa Portland.

Miongoni mwa vitu vinavyouzwa, kuna nyumba sita, jumba moja lenye vyumba vingi vya makazi, kituo cha petroli na duka moja.

Wakazi takriban 250 huishi maeneo yaliyo karibu na mji huo.

Wakazi walianza kuuhama mji huo baada ya kudorora kwa biashara ya mbao na kufungwa kwa kiwanda cha kupasulia mbao.

Mji wa Tiller ulianza kuuzwa mara ya kwanza mwaka 2015 shule ya msingi ya zamani haikuwa imejumuishwa miongoni mwa vilivyokuwa vinauzwa.

Ni wakazi wawili pekee ambao kwa sasa bado wanaishi katika mji wa Tiller wenyewe. Wakazi hao ni mwalimu wa zamani ambaye anaishi karibu na shule iliyokuwa ikitumiwa zamani, pamoja na mhubiri wa kanisa moja.

Vipande vyao vya ardhi haviuzwi.

_95160924_tiller2.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionMji wa Tiller umezingirwa na milima na msitu
_95161176_tiller3.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionMaporomoko ya maji ya South Umpqua yanapatikana karibu na mji wa Tiller
_95161180_tiller5.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionNyumba moja mjini Tiller
_95161182_tiller6.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionDuka kuu mjini Tiller bila linauzwa, lakini linauzwa kando
_95161184_tiller7.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionWapenzi wa filamu ya Walking Dead wanaweza kupendezwa na duka hili
_95161206_tiller8.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionShule hii ya msingi ya zamani pia inauzwa, pamoja na paa anayeishi humo
_95161209_tiller9.jpg
Haki miliki ya pichaLAND AND WILDLIFE.COM
Image captionChumba cha kufanyia mazoezi ya viungo shuleni humo
Mbona mtu atake kuishi humo?

"Pesa kutoka kwa serikali kuu za kutumiwa katika biashara ya kupasua mbao zilipoanza kupungua, kiwanda kilifungwa," anasema Garrett Zoller, mmiliki wa shirika la Land and Wildlife.

"Na kiwanda kilipofungwa, wengi wa wapasuaji mbao walianza kuondoka."

Familia inayomiliki mji wa Tiller kwa sasa ilinunua mji huo kipande kwa kipande familia nyingine zilipoendelea kuhama.

Miongoni mwa walioonesha nia ya kutaka kununua mji huo ni wawekezaji kutoka China, pamoja na watu wanaotaka kuanzisha taasisi za matibabu au kukuza miti.
 
Back
Top Bottom