chimwemwe2
New Member
- Jul 19, 2012
- 4
- 0
Hi to all, napenda kuchukua nafasi hii kwenu kuomba ushauri juu ya sula la wanawake pindi wanapo ondokewe na waume zao mbona jamii inaangalia kwa mtazamo tofauti sana, tofauti na wanaume wanapofiwa na wake zao? Pili ni muda gani unafaa kwa mwanamke aliyefiwa na mume kuweza kuingia tena kwenye mahusiano na mwanaume mwingine?
Mpaka atakapo mpata wanayependana!
Atampataje kama akileta kilio chake mfano hapa JF mnamzodoa na kumcheka?
Atampataje kama akileta kilio chake mfano hapa JF mnamzodoa na kumcheka?
That is our Wise Babu DC!
Wana haki ya kupenda tena!
Unajua Dark City, mwanamume umri ukienda anaweza bado kuoa binti ambaye anamzidi 20yrs, lkn mwanamke akiwa hata na mwanaume wanayepishana 7 yrs (she has to be rich ili kumpata huyo kaka), jamii inamuangalia kwa macho mawili. Na mbaya zaidi wazee wenzake (wanaume) go for younger girls hivyo huishia au kuokoka (kumpenda Yesu) au kuiba waume za watu au kutafuta viserengeti boys!
Mimi nafikiri jamii iwaruhusu wabibi nao wamiliki viSBs na ukizingatia vijana wa sasa hivi wanapenda mteremko, au unaonaje Babu DC?
Kama watafuata huu ushauri basi watasubiri sana..
Ukitegemea jamii ikuruhusu itakula kwako aisee..
Better to decide on your own..
Unaweza kutupatia ushahidi wa mtu au watu wanaozodoa wajane na kuwacheka?
Na ni nani anaweza kufanya kitu cha namna hiyo wakati kila mtu ni mjane mtarajiwa??
Babu DC!!
ukakwapue mali alizoacha mwanaume mwenzio...lol
Kwani tunaaccess ya inbox yake? Kuzodoana ni kupima userious na kifua cha mtu; kwani anataka sympathy au mtu atakayempenda? Kwani ujane ni ulemavu?
ukakwapue mali alizoacha mwanaume mwenzio...lol