Mjamzito haelewi ana nini!

Mjamzito haelewi ana nini!

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,651
Reaction score
4,758
******************************
NB: Uzi huu nimeupeleka pia JF DOCTOR kwa ajili ya msaada wa kitaalamu zaidi...LAKINI HAPA NIMEULETA KUPATA USHAURI WA EXPERIENCE...

*******************************

Mke wangu ni mjamzito wa miezi 10 hivi sasaa...yaani amepita tarehe yake ya makadirio jana tarehe 29...

CHA AJABU NI YEYE KUTOHISI CHOCHOTE...NI JUZI TAR 27 KAMA SIKOSEI NDIO ALIANZA KUTOKWA NA MAJI MAJI MEUPE UKENI...KIDOGO KIDOGO YAKAWA YANAZIDI...NIKAMKIMBIZA HOSPITAL...WAKAPIMA NJIA...WAKAONA BADO HAIJAFUNGUKA...

Wakamwambia afanye fanye mazoezi...lakini wapi mpaka leo yupo bado hospital...maji yanaendelea kutoka..hakuna chochote kinachomuuma zaidi ya KICHWA MARA MOJA MOJA KINAACHA...

HASIKII KICHOMI WALA TUMBO KUKATA WALA MGONGO WALA KIUNO...NI UKENI TU NDIO PANAVUTA NA MAUMIVU KIDOGO ...

NDIO AMESEMA YAANI PANAVOVUTA UKENI NDIO KUNAUMA...

Na chooni ndio anaenda mara kwa mara kukojoa...

MANESI WALIVYOPITA JANA WAKAMPIMA PIMA KWA KUGUSA TUMBO LAKE...WAKAWA WAMEGUSA VITU KAMA N VICHWA VIWILI PEMBENI WAKADHANI NI MAPACHA...LAKINI DOCTOR AKAJA AKAGUSA VIZURI AKAWAAMBIA SIO MAPACHA MMEGUSA MBAVU LABDA...KICHWA KIPO CHINI MBONA TAYARI...BADO KUTOKA TU...

Na mtoto bado mapigo yake ya moyo yanapiga kawaida tu...na anacheza kawaida tu sanaaa...

TATIZO LANGU NI HILO MKE WANGU HAELEWEKI...MAANA YUPO SAWA TU...HAKUNA MENGINE YANAMSUMBUA KAMA MJAMZITO ZAIDI YA HIZO DALILI NILIZOZIELEZA HAPO JUU...

NAOMBENI UTAALAM WENU NDUGU ZANGU KAMA KUNA MADAKTAR NA WATAALAM WA HAYA MAMBO WANITULIZE AKILI YANGU KWA KUNIPA NINI CHA KUFANYA...

Maana nasikia sijui kuna wanawake wengine wana nyonga ya kiume...haziwezi zaa kawaida...sijui wengine nyonga ya mnyama sijui...nijuzini nitulize nafsi yangu...

MAANA ANAZIDI KUKAA HOSPITAL TU...NA MNAVYOJUA HOSPITAL CHAKULA NI CHA KUNUNUA NA WANAUZA GHARAMA UTASEMA KULE NI SEHEMU YA STAREHE...

YAANI MTU CHAI YA RANGI ANAUZA KIKOMBE 500 KWELI NA HALF CAKE 500...NI UPUMBAVU SANA KURUHUSU BIASHARA KAMA HIZI MAHOSPITAL...NI DHULMA NA UNYONYAJI MKUBWA SANAA...
 
Duuh! pole mkuu ila kwakua Jf ni kisima Cha Maarifa tusubiri wajuzi wa hili waje kutia neno
 
Kupitiliza kwa siku ya kujifungua hutokea wanachofanya madaktari wanachukua ultrasound tena wanaangalia kama placenta imechoka au vipi kama siku zimepita kama bado basi watampa muda tena, hapo madaktari huwa wana rely sana kwenye ultrasound ya kwanza kabisa kutumia kujua mtoto yupo week ya ngapi ,halafu kama maji yameshatoka nilifikili yupo nyumbani kama yupo hospital basi haina shida,cha msingi weka matumaini kwa madaktari hofu haina maana zaidi ya kukufanya kuwa chizi
 
Mungu atamsaidia,hiyo case nimeishuhudia Shemeji yangu alijifungua miezu 11but alijifungua salama tu
 
So what to do next..nataka nichukue hatua kama mwanaume...ukikaa tu usubiri...je inasaidia nini
Mwanaume ukipanik zaidi ya mke una hatarisha maisha ya mama na mtoto,kuwa jasiri
 
Kupitiliza kwa siku ya kujifungua hutokea wanachofanya madaktari wanachukua ultrasound tena wanaangalia kama placenta imechoka au vipi kama siku zimepita kama bado basi watampa muda tena, hapo madaktari huwa wana rely sana kwenye ultrasound ya kwanza kabisa kutumia kujua mtoto yupo week ya ngapi ,halafu kama maji yameshatoka nilifikili yupo nyumbani kama yupo hospital basi haina shida,cha msingi weka matumaini kwa madaktari hofu haina maana zaidi ya kukufanya kuwa chizi
Nashukuru sana kidogo umenipa relief...
 
Sasa yaani mwezi mzima akae tu hospital jamani...c bora huyo shemej yako alikaa nyumbani...
Mungu atamsaidia,hiyo case nimeishuhudia Shemeji yangu alijifungua miezu 11but alijifungua salama tu
 
DsmicSound,
Hakuna ultra sound huko mkuu maana naona madokta wanafanya unajimu kwenye dunia ya kidigitali.

Ikiwa ipo wampime ujue mtoto kakaaje, wapo wangapi na kadhalika. Vitu vingine kama baba chukua hatua usikabidhi kila kitu cha maamuzi kwa hao jamaa.
 
BABA NASHUKURU SANAAA...NITAUFANYIA KAZI USHAURI WAKO...TENA KUANZIA SASA...
 
Unaletewa kidume, kuwa na subra mkuu.
Aisee...mpaka sometimes naogopa labda naingilia kazi ya Mola wangu narudi nyuma...lakini wakati mwingine Kufanya jitihada ni sehemu ya Qadar ya Allah...
 
DsmicSound, Hapo nahisi mkeo anaumri mkubwa wa kuzaa au mara ya mwisho alijifungua ni muda mrefu umepita. Au anakula sana vitu vya baridi huwa vinadababisha kutokupata uchungu kwa muda muafaka au hakuwa akifanya mazoezi haswa ya kutembea ili kuuandaa mwili kwa ajili ya kujifungua
 
Back
Top Bottom