Heshima kwenu wakuu.
Kuna mama /dada ni mjamzito. Sio ujauzito wake wa mara ya kwanza.
Anapitia changamoto hizi.
★Tumbo kuuma chini ya kitovu, linauma baadae linaachia lenyewe na kujirudia rudia.
★ Kichwa kuuma mara kwa mara.
★ Kuhisi baridi sana mara kwa mara.
★ Kuhisi kizunguzungu
Watalaamu wa afya na wakubwa (mna uzoefu) naomba kufahamu nini hasa chanzo cha haya matatizo kwa mjamzito??
Je, ni hali ya kawaida, yaani huwatokea wajawazito wengine??
Je, suluhisho ni nini??
NB: Hajaanza kliniki na hajaenda hospitali kufanyiwa check up.
ASANTENI SANA NA MBARIKIWE SANA.
Habari!
Kwa mwanamke yeyote anaehisi au kujitambua ni mjamzito, sera ya sasa inamtaka kufika kuthibitisha au kuanza Kliniki ya Uzazi mara moja/hakuna sababu kusubiri.
Pia mama atapata elimu ya uzazi na utunzaji mzuri wa afya yake pamoja na kiumbe alichonacho. Atapata virutubisho hitajika kulingana na umri wa ujauzito. Pia , tiba mahsusi na ushauri kulingana na afya yake.
Kwa changamoto anazopitia mhusika, si rahisi kupata jibu mwafaka kulingana na kutokuwepo kwa maelezo zaidi ili kupunguza au kuongeza uwezekano wa matatizo yanayomsibu. Pia ukaguzi wa mwili/examination ni muhimu.
Haya unaweza kuyaona kwenye maelezo hapa chini:
[ ] Tumbo kuuma chini ya kitovu, linauma baadae linaachia lenyewe na kujirudia rudia.
1: Maambukizi ya UTI.
2: Shida kwenye mfumo wa chakula.
3: Nyonga kutanuka/kutegemea na umri wa ujauzito.
4: Tatizo linalohusu mimba yenyewe.
[ ] Kichwa kuuma mara kwa mara.
1: Hii inaweza kuwa inaambatana na mabadiliko ya vichocheo wakati wa ujauzito.
2: Maambukizi yoyote ya virusi, malaria au bakteria.
3: Kutokula vyema au kunywa maji ya kutosha
4: Kutokupumzika vyema
5: Upungufu wa damu
[ ] Kuhisi baridi sana mara kwa mara.
1: Maambukizi yoyote kati ya: virusi, bakteria, UTI na malaria.
[ ] Kuhisi kizunguzungu.
1: Hali ya ujauzito wenyewe.
2: Kutokula au kunywa maji ya kutosha.
3: Kutokupumzika vyema.
4: Madhira ya maambukizi hapo juu.
5: Presha yake kushuka.
6: Upungufu wa damu
Suluhisho:
Unaweza kuona mlolongo wa mchanganyiko wa matatizo hapo juu. Ila mengine yanaweza kuondoka kupitia maelezo zaidi ya mgonjwa, vipimo vya awali/vital signs, ukaguzi wa mwili na baadaye vipimo maabara. Hapo ndo umuhimu wa KUFIKA KWENYE VITUO VYA AFYA NA KUWAONA WATAALAMU WA AFYA UNAPOONEKA.
Timiza wajibu wako sasa kikamilifu.