Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

JUST

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
552
234
Leo Mh. Mbowe ameonyesha njia kwa kuwachapa viongozi wetu bakora kumi alizozituo wakati wa kuchangia mjadala wa bajeti ya fedha na uchumi ya mwaka 2011/2012. bakora hizo alizito kwa nyakati tofauti akiwa anachangia hoja hiyo.



1. waache kusafiria ndege business/first class at USD 5000 badala yake wasfirie economy class ya USD 1200 wanaotumia donors. mbona wengi wao akistaafu hawapandi tena fisrt class na wengine hata ndege hawapandi tena.

2. waache kutembelea mashangingi wakati wagonjwa wanapelekewa ambulance za bajaji

3. waache kukimbizana na semina kama zinazoanadliwa za kuhusu chanzo cha ukimwi ili wapate posho badala yake wakae ofisini na kama kuna kiongozi mpaka leo hafahamu chanzo cha ukimwi basi aachie ngazi.

4. kama kweli viongozi wanastahili maisha wanayoishi sashivi mbona wakistaafu hawawezi kununua magari mapya sanasana wananunua Rav 4 au Mark II.

5. magari yote yakifahari yauzwe na wahusika wapewe mikopo ya magari wanunue ya kwao.

6. posho zinafaidisha viongozi wa ngazi ya maamuzi tu na sio waalimu, polisi au nesi.

7. tuache uchama tueke maslahi ya taifa mbele kwa maslahi ya wanachi wa tanzania.

8. hotuba ya mbowe ilifanya mawaziri waliokuwa bungeni kuangalia chini na kuonyesha sura za huzuni.

9. posho inasababisha kiwe ni chanzo cha watumishi kuhudhuria vikao muhimu na kama haipo hakuna mahudhurio.

10. mbowe alipokuwa anchangia ni kwa mara ya kwanza wabunge wote walikaa kimya na kusikiliza kwa umakini wa hali ya juu.


source TBC kipindi cha kutoka bungeni.
 
Tatizo serikali yetu siyo sikivu. Haisaidii kitu. Nothing will change
 
Tatizo serikali yetu siyo sikivu. Haisaidii kitu. Nothing will change

siku hizi hatuhitaji serikali isikilize kwa niaba yetu.

kama hawajasikia, sisi (wananchi) tumesikia, na tutawaonesha 2015 kwamba tumesikia.
 
Tatizo serikali yetu siyo sikivu. Haisaidii kitu. Nothing will change


kila jambo lina mwisho wake enzi na kudanganya watu zinakarinia kuisha by 2015 wewe binafsi unswaonaje watu wanokuzunguka na shule hawana. je ni wakudanganyika na serikali tena?
 
Tundu amewajibu wale magamba ambao wanawaponda wabunge wa CDM kuwa wanapinga kila kitu kuwa kupinga unyanyasaji ni kumtii Mungu.
Bravo Kamanda.
 
Nimefurahishwa sana na majibu yake kwa mbunge wa Buchosa aliyesema wabunge wa upinzani wana macho lakini hawaoni, wanamasikio lakini hawasikii ila wanamidomo wanaongea. Ametoa data jinsi misamaha ya kodi kwenye madini yanavyotafuna nchi halafu akamjibu jamaa kwamba kwenye mazingira hayo hatuwezi kuona wala kusikia! Nimeipenda sana hiyo!
 
that's what m talking about...
ila angalia tu wasikuwekee sumu.
big up my brother from another mother.
 
A wise response to a stupid comment. Suala la haya makampuni ya madini linachefua sana mpaka natamani wangefukuziliwa mbali!
 
Data za Lissu zimenitoa machozi! Ni aibu tupu kwa nchi yetu. Na data zote zimetokana na ushauri wa wataalamu na tume mbalimbali zilizoundwa na JK na BWM lakini wamezitia kapuni! Inakera sana.
 
Huyu Mh Lisu mi namkubali sana katika bunge hili mpaka nashindwa kuona pengo slaa, is a serious man
. Nadhani amedhutu,ameweza na atasongo mbele ktk bunge hili.
 
chadema has the cream of this national while ccm has the ukoko. Mtanisaidia ukoko unaitwaje kwa kizungu!

Chadema gogogoooooooooooo
Lisu keep it up, you have won our hearts!
 
Soon we will get there. Hata wenzetu walianza hivi hivi mpka kikaeleweka.
 
Mie huwa nashindwa kuielewa serikali na mambo ya kuunda TUME! Yaani huwa inatumia pesa nyingi na muda kuunda tume. Tume ikikamilisha kazi na kutoa mapendekezo haiyajali wala kuyafanyia kazi! Sijui huwa wanaunda tume kwa manufaa ya nani!
 
nasikia obama atakuja Tz sasa cjui anakuja Wekeza nini,mana Barick mining Bush anahisa pale,ndo mana haki kupatikana ni ngumu.
 
Mie huwa nashindwa kuielewa serikali na mambo ya kuunda TUME! Yaani huwa inatumia pesa nyingi na muda kuunda tume. Tume ikikamilisha kazi na kutoa mapendekezo haiyajali wala kuyafanyia kazi! Sijui huwa wanaunda tume kwa manufaa ya nani!
Another mean of buying time,.....
 
ccm wafanye wanachotaka lakini tutakutana kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 wala sio mbali sana.
 
Back
Top Bottom