Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Sehemu ya Taarifa juu ya kinachojiri katika utekelezwaji wa vipaumbele vilivyopitishwa katika warsha ya ufunguzi wa mradi wa TUSHIRIKISHANE.

Taarifa ni kuwa ifikapo mwezi Januari mwaka 2017 Kigamboni inategemea kupata kivuko kingine ambapo jumla kufanya idadi ya vivuko kuwa vitatu.

Hii ikiwa ni katika hatua za kuboresha na kurahisisha huduma ya kivuko kwa watu na vyombo vya usafiri.

Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Kigamboni ndugu Faustine Ndugulile alilitolea ufafanuzi suala hili tarehe 10/12/2016 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mnadani baina yake na wakazi wa kata ya Tungi ikiwa pia kama sehemu ya utekelezaji wa vipaumbele vilivyopitishwa katika ufunguzi wa warsha ya mradi wa TUSHIRIKISHANE.
 
Taarifa ya kinachoendelea katika utekelezwaji wa vipaumbele vilivyopitishwa kuingia katika mradi wa TUSHIRIKISHANE.

Taarifa ni kuwa kwa maeneo yasiyo kwenye mtandao wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu (Phase III) yaani maeneo kama vile Tundwi songani,Kimbiji, na Kisarawe II yapo mbioni kufikiwa na huduma hiyo huku maeneo kama Pembamnazi tayari huduma hiyo ikiwa imeanza kusogea.

Kuhusu wateja ambao wamelipia ada ya kufungiwa umeme na huku bado hawajapata umeme Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile amewaagiza Tanesco kuwapa wakandarasi binafsi baadhi ya miradi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi.

Hii nayo ikiwa kama Sehemu ya utekelezaji wa ahadi kupitia mradi wa TUSHIRISHANE/Mjadala wa mipango ya maendeleo kwa jimbo la Kigamboni hususani katika kuboresha sambamba na kuongeza miundombinu ya umeme kwa eneo la Kigamboni.
 
Mkuu, kuna Gezaulole ambayo ni kilometa 15 tu toka Posta na hakuna umeme. Na hakuna jitihada zozote za makusudi za kupeleka umeme huko. Ni maeneo ya viwanja vipya ambako kuna wakazi zaidi ya 100 kwa sasa (wanaoishi) achilia mbali walojengana hawajahamia bado. Hivi inawezekanaje mahali pa kilometa 15 tu toka katikati ya mji mkubwa wa kibiashara kama Dar kukosa umeme? Inashangaza sana aiseee...
 
Keep it up Dr ndungulire changamoto ni nyingi komalia vipao mbere vyako maana mwishowe tuyakuhoji kwa kuangalia vipao mbere,tunatakabkusoma agizo lako kwa tanesco na feedback yao
 
Mkuu, kuna Gezaulole ambayo ni kilometa 15 tu toka Posta na hakuna umeme. Na hakuna jitihada zozote za makusudi za kupeleka umeme huko. Ni maeneo ya viwanja vipya ambako kuna wakazi zaidi ya 100 kwa sasa (wanaoishi) achilia mbali walojengana hawajahamia bado. Hivi inawezekanaje mahali pa kilometa 15 tu toka katikati ya mji mkubwa wa kibiashara kama Dar kukosa umeme? Inashangaza sana aiseee...

Naomba unijulishe kitongoji ulichopo ili niweze kukupa taarifa iliyo sahihi. Asante
Dkt Ndugulile Mb
Kigamboni
18.01.2017
 
Keep it up Dr. Ndugulile changamoto ni nyingi komalia vipaumbele vyako maana mwishowe tutakuhoji kwa kuangalia vipaumbele. Tunataka kusoma agizo lako kwa TANESCO na feedback yao

Nakushukuru kwa kunitia moyo. Natambua changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara Kigamboni. Hii inasababishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja:
1. Mahitaji ya umeme Kigamboni ni 20MW lakini tunapata 8MW.
2. Laini tunayopata Kigamboni inaanzia Kipawa na inahudumia pia Mbagala, Mkuranga na maeneo ya njiani.
3. Uchakavu wa miundombinu.

HATUA ZA MUDA MFUPI
Tunarajia hali ya umeme kuwa nzuri kuanzia mwezi Machi, 2017 baada ya ujenzi wa laini toka Mbagala na Kurasini kuja Kigamboni kukamilika.

HATUA ZA MUDA MREFU
Tanesco wameshanunua eneo la zaidi ya ekari 10 huko Somangila na makisio ya ujenzi wa kituo cha Umeme yameingizwa kwenye makadirio ya bajeti ya 2017/18.

Dkt Ndugulile
Mbunge Kigamboni
18.01.2017
 
Naomba unijulishe kitongoji ulichopo ili niweze kukupa taarifa iliyo sahihi. Asante
Dkt Ndugulile Mb
Kigamboni
18.01.2017
Asante mheshimiwa.

Mimi nipo viwanja vipya block namba 16. Lakini katika block zote za mradi wa viwanja Gezaulole, ni block moja tu ya 15 ndiyo yenye umeme. Namba yangu ya simu ni 0767 210 396 ikiwa utahitaji maelezo zaidi.
 
Taarifa ya kinachoendelea katika utekelezwaji wa vipaumbele vilivyopitishwa katika mradi wa TUSHIRIKISHANE

Mpango juu ya matengenezo ya kipande cha barabara ya kutoka darajani hadi kwa Msomali kwa kiwango cha lami

Taarifa rasmi hadi hivi sasa ni kuwa fedha ya mradi imeshatengwa ambayo ni takribani shilingi bilioni ishirini na nne za kitanzania huku michoro ya barabara hiyo ikiwa imekamilika na mkandarasi pia akiwa ameshapatikana hivyo ujenzi wa barabara hiyo unategemewa kuanza muda wowote kuanzia sasa.
 
Taarifa ya kinachoendelea katika utekelezwaji wa vipaumbele vilivyopitishwa katika mradi wa TUSHIRIKISHANE kwa jimbo la Kigamboni.

Mikakati ya kuboresha huduma za afya jimbo la Kigamboni, serikali kupitia wizara ya afya mwishoni mwa mwaka 2016 iliipatia halmashauri ya Kigamboni gari la kubebea wagonjwa (Ambulance)

Kupatikana kwa gari hilo kunaifanya kigamboni kuongeza idadi ya magari ya wagonjwa na kufikia magari manne (4) hadi hivi sasa

Magari hayo yanahudumia hospitali na vituo vya afya Vijibweni, Kigamboni na Kimbiji.


Aidha zahanati ya kata ya Kisarawe II mapema mwaka huu 2017 mwezi huu wa Januari imepata wodi mpya ya wazazi iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kwa ufadhili wa kampuni ya Oilcom.

Pia Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile amedokeza kuwa mfalme wa Morocco pindi alipowasili nchini Tanzania kwa ziara fupi aliahidi kufadhili ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kigamboni.
 
Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dr F. Ndugulile amehoji na kutoa mapendekezo kwa Wahusika. Amesema, "NSSF yakusanya Tsh 5 Bilioni ndani ya miezi 8 kwenye Daraja la Nyerere. Ni jambo jema. Wana Kigamboni wangependa kuona yafuatayo yanafanyika:

1. Madirisha yote 14 ya kukatia tiketi yanatumika badala ya sasa ambapo madirisha machache yanatumika na hivyo kusababisha foleni.

2. Tozo kwa daladala zinapunguzwa ili kuvutia wenye magari kuanzisha ruti ndefu na kupunguza gharama za nauli. Mwananchi wa Kigamboni anahitaji nauli 3-4 kufika maeneo mbalimbali ya Jiji la DSM.

3. Kumalizia kipande kilichobaki cha barabara toka darajani upande wa Kigamboni."

=======

Hii habari ilitoka kwenye Gazeti ya nipashe ikisomeka Hivi....

Shirika la taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF)limekusanya shilingi bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane katika daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni Dar es Salaam.

Makusanyo hayo, imeelezwa, ni kuanzia katikati ya Mei, mwaka jana hadi mwezi huu na ni juu ya lengo kwa asilimia 20.

NSSF inakuwa taasisi ya pili ndani ya wiki moja kutangaza mapato ya mradi, baada ya Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kufanya hivyo Alhamisi.

Akizungumza na Nipashe jana juu ya maendeleo ya mradi wa daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema limeingiza jumla ya Sh. bilioni sita.

Aidha, Prof. Kahyarara alisema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu.
Prof. Kahyarara alisema NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya wakala.

Alisema awali makaridio yalikuwa ni kukusanya Sh. bilioni tano katika kipindi hicho.

“Sera yetu ni kwamba hizi fedha hatuzitumii," alisema Prof. Kahyarara."

"Tunaziwekeza moja kwa moja BoT (Benki Kuu) katika mnada wa dhamana za serikali (treasury bonds) ambayo ni ya asilimia 13.5 ambayo ikiiva miaka 15 ijayo ni Sh. bilioni 18."

Alisema kwa uwekezaji huo, NSSF itarudisha fedha zilizojenga daraja na faida ya kutosha.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, kwa utaratibu wa BoT kila baada ya miezi sita wanaweza kuvuna faida ambayo watawekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo.

“Utaratibu huu tumeona unalifanya Shirika kuwa na uhakika, kwamba likihitaji fedha ya haraka wanaweza kuzitumia na taarifa zitaonyesha fedha za daraja zilishapatikana. Ni ubunifu tulioanzisha kwa kuwa tuliona ukiweka sekta binafsi huwezi kupata faida hiyo,” alifafanua.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF alisema iwapo kazi ya kukusanya fedha hizo ingepewa kampuni binafsi wangepata hasara ya Sh. milioni 300.

Prof. Kahyarara alibainisha kuwa NSSF ilitaka tangu siku ya kwanza ya kutumika kwa daraja hilo faida ianze kukusanywa jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Tuna uwezo mkubwa wa kukusanya fedha, tuna madirisha ya kutosha na watu wenye utaalamu kama walioko mabenki. Itakuwa ni kituko kumuita mtu kutukusanyia fedha, hivyo hatuna mpango wa kutumia kampuni binafsi," alisema Prof. Kahyarara.

"Kwa kutumia wafanyakazi wetu wenyewe tuna uhakika mkubwa wa kukusanya zinazoingia na kurudisha fedha zetu kwa wakati.”
Prof. Kahyarara alisema kazi ya NSSF ni kuandikisha wanachama, kukusanya fedha za wanachama, kulipa mafao na kuwekeza ili fedha ziwe na thamani zisikae bila kuwa na thamani.

Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola za Kimarekani milioni 128, ulianza mwaka 2012 na kufanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Daraja hilo lililozinduliwa Aprili 19, mwaka jana, na Rais John Magufuli, lina urefu wa mita 680 na jumla ya barabara sita.

Chanzo: Nipashe
 
Kuna kero nyingi zinawakabiri wananchi wa Kigamboni, Lakini baadhi ya kero zimetolewa Majibu na Munge wa Kigamboni. Mradi wa Tushirikishane NI kuwawezesha wananchi kuwasiliana na Mbunge wao, Hili swala la Mawasiliano JamiiForums imerahisisha kwani unaweza kuandika duku duku lako hapa kwenye hii thread na Ukapatiwa Majibu sahihi kutoka kwa Mbunge wa Kigamboni.

Hapa chini nakuwekeeni majibu ya Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dr F. Ndugulile kwa Baadhi ya Maswali Yaliyohojiwa.

Kasema hivi;

Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na huduma isiyoridhisha kwenye Daraja la Nyerere linalounganisha Kigamboni na Kurasini.

Malalamiko ya wananchi yako kwenye maeneo makuu matatu:

1. Kutumika kwa madirisha machache ya kukatia tiketi. Daraja la Nyerere lina madirisha 14 ( Saba wakati wa kuingia na Saba wakati wa kutokea). Madirisha yanayotumika ni machache na hivyo kusababisha foleni isiyo na msingi.

2. Tozo za Daraja la Nyerere zipo juu sana hususan kwa magari ya abiria. Hali hii imepelekea Kigamboni kukosa ruti ndefu za kuelekea maeneo mengine ya Jiji la Dar Es Salaam. Gari la abiria linatozwa kati ya Tsh 5000-7000 kwa kila safari ambayo ni gharama kubwa sana kwa kutwa.

3. Kutokamilika kwa kipande kilichobaki toka Darajani hadi kwa Msomali.

Kama Mbunge wa Kigamboni nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa karibu sana bila ya mafanikio. Tukumbuke kuwa Daraja la Nyerere lilizinduliwa tarehe 19.04.2016 na sasa ni zaidi ya miezi 9 hamna kinachoendelea na wahusika hawatoi majibu yanayotosheleza.

HATUA NILIZOCHUKUA HADI HIVI SASA

1. Mnamo tarehe 15.06.2016 nilimwandikia barua Waziri wa Ujenzi Mhe. Makame Mbarawa (Mb) kuhusiana na hoja hizi. Pamoja na kufuatilia zaidi ya mara kumi kwa simu, maongezi ya ana kwa ana na meseji, barua yangu haijajibiwa hadi hivi sasa (Angalia kiambatanisho).

2. Vile vile nilikutana na Mkurugenzi wa NSSF Prog Godius Kahyarara tarehe 3.10.2016 kuhusu hoja tajwa hapo juu. Aliahidi kuchukua hatua za haraka lakini hadi hivi sasa hakuna kilicofanyika.

3. Kwa kuwa usimamizi wa Daraja la Nyerere upo chini ya NSSF na kipande kilichobaki kitajengwa na NSSF, niliomba kukutana na Waziri anayesimamia taasisi hii. Nilikutana na Mhe. Waziri Jenista Mhagama (Mb) tarehe 3.12.2016 ofisini kwake. Pamoja na maelezo ya mdomo, nilimkabidhi barua ya malalamiko (Angalia kiambatanisho). Mheshimiwa Waziri aliahidi kuchukua hatua za haraka.

Tarehe 13.12.2016 nilipata nakala ya barua aliyoandika Mhe. Waziri Mhagama kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ili kupata maelezo na ufumbuzi wa hoja nilizotoa. Pamoja na kukumbushia Mhe. Waziri Mhagama hajanipatia majibu ya hoja zangu.

Aidha, maelezo niliyopata toka kwa Mkurugenzi wa NSSF wakati Waziri Mkuu anatembelea Kigamboni tarehe 04.01.2017 ni kwamba fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande kilichobaki ni Tsh 24 Bilioni na alinihakikishia kuwa FEDHA HIZO ZIPO. Michoro (design) ya barabara hiyo IMESHAKAMILIKA. Mkandarasi kwa ajili ya kazi hiyo YUPO.

Pamoja na NSSF kuwa na fedha ya ujenzi wa barabara hiyo, mkandarasi aliye tayari na michoro iliyokamilika, kumekuwa na kigugumizi ya lini kazi hii itaanza.

Inasikitisha pia kuona Mawaziri hawajibu barua pamoja na kukumbushwa mara kwa mara.

Kinachoendelea sasa hakuna lugha nyingine ya kuielezea zaidi ya UZEMBE na KUTOWAJIBIKA.

Naleta taarifa hii kwenu wakazi wa Kigamboni ili nanyi mjue kinachoendelea. Ninakusudia kuyapeleka malalamiko yenu kwa mamlaka ya juu zaidi, baada ya mamlaka tajwa hapo juu kushindwa kupata ufumbuzi.

Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge
 
Mh mbunge ulituahidi kupata umeme sisi wakazi wa Mwembe mdogo hadi eneo linafahamika kama Vumulia - ukooni uliahidi hadi kufikia november 2016 umeme ungekuwa unawaka lakini hadi sasa hii ni february hakuna hata dalili za kuleta nguzo. And at that time ulisema kuna kampuni binafsi ambazo ndo zilikuwa zikifanyiwa pre qualification kwa ajili kuja kuwa shindanisha waweze ku supply hizo line za umeme, cha kushangaza ukienda tanesco kigamboni hakuna taarifa kama hiyo na wala hakuna zoezi la prequalification lililofanyika na inaonekana ni jambo jipya. Mwisho kabisa Tanesco kigamboni haijayajua maeneo ya kigamboni wao wanajua ferry , mjimwema na kibada hilo nalo ni tatizo. Watoke wayajue maeneo yao ya kazi na sisi wananchi tuko tayali kushirikiana nao
 
Muheshimiwa mbunge mimi kilio changu ni katika mambo mawili;
1. Ubovu wa barabara ya kibada - mwasonga
2. Kukosekana kwa taarifa za usambazaji wa umeme Mwasonga, kata ya kisarawe 2

Barabara
Hii barabara imekeuwa inafanyiwa ukarabati wa mara kwa mara ila wa kiwango cha chini sana.
Vifusi vya kokoto haviwekwi au vitawekwa vichache na sio vya kokoto bali udongo. Kinachofanyika sehemu kubwa ni kupiga greda tupu .Jambo hili husababisha barabara kuharibika mapema kwa kuwa ardhi ya huku ina asili ya mchanga na barabara inahudumia magari makaubwa na mazito yaendayo kiwanda cha Nyati cementi na dar fresh. Zaidi ya hayo maeneo ya njia za maji hayana makalavati au mifereji imara hivyo barabara huchimbika na kukatika kirahisi kila msimu wa mvua.

Umeme
Kijiji cha mwasonga sasa kina wakazi wengi waliojenga nyumba nzuri na za kisasa. Kuna shughuli nyingi za kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme. Nguzo kuu za umeme zimefika na kupita ila umeme haujasambazwa. Kuna harufu ya ufisadi na ubinafsi kwa kuwa kijiji kizima kumefungwa ka transfoma kadogo kanakohudumia nyumba ya diwani na kiwanda kidogo cha matofali cha mtu binafsi.
Wananchi wengine tunautaka umeme huu na uwezo kwa kuulipia tunao ila kuna vikwazo kati ya tanesco kigamboni na uongozi wa kijiji hususani diwani. Ninaomba majibu
 
Kuna Mambo Mengi ya Maendeleo yanaendelea Jimbo la Kigamboni. Je wajua Kuna vyandarua vinagawiwa bure?
15284010_10154543987135901_119648924345797236_n (1).jpg
15327468_10154543987150901_7547506438821274_n.jpg

Mbunge Dkt Faustine Ndugulile ambaye ni akiwa na wajumbe wa Serikali ya Mtaa ya Kibene, Vijibweni baada ya kukagua zoezi la ugawaji vyandarua.

Kwa wale waliopoteza vocha au kutosajiliwa kupewa vocha mwezi Februari mwaka huu, waende kwenye ofisi za Serikali kuanzia siku ya Jumanne na watapatiwa utaratibu wa kupata chandarua.

NB: Vyandarua vinatolewa bure
 
image2.jpg

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuangalia upya tozo za daladala zinazo pita katika daraja la kigamboni hili kuweza kutoa unafuu kwa wananchi waishio Kigamboni kama ilivyokua madhumuni ya kujengwa kwa daraja hilo.

Akizungmza na globu ya jamii Dk Ndugulile amesema kuwa wananchi wamekuwa watumwa kwa usafiri kwa miaka mingi huku wakitegemea daraja liwe mkombozi lakini sasa imekuwa kinyume kutokana na gharama za kupita kwa daladala katika daraja hilo.

“gari moja yaani daladala linatakiwa kulipa shilingi 5000 huku kwa kila trip kitu ambacho ni gharama kuliko biashara yenyewe ambayo ni huduma kwa wanachi hivyo kwa hesabu za haraka kama dereva atafanya trip 10 atatakiwa kulipa shilingi 50,000/- kitu hicho kinawawia vigumu kufanya kwa madereva wa daladala” amesema Dk Ndugulile.

Amesema kuwa amefanya jitiada za kila namna kwa kuzungumza na mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF ambo wao ndio wanaendesha daraja hilo kwa kuwaandikia barua rasmi hili waweze kupunguza tozo hizo kwa ajili ya daladala lakini bado aoni dalili.

Ameongeza kuwa gharama za mkazi wa Kigamboni katika safari za mjini ni kubwa kuliko mtu yoyote licha ya kuwepo kwa miundombinu ya barabara na vivuko bado gharama za kifedha ni juu katika kutumia miundombinu hiyo.
 
Mheshimiwa Mbunge wa KigamboniFaustine Ndugulile, Aliliona hili Tatizo wakati akipita daraja la Kigamboni na Kusema, "Foleni kwenye Daraja la Nyerere leo tarehe 26 01.2017 inayosababishwa na uzembe na usimamizi mbovu wa NSSF kwenye Daraja hili.
16252135_10154726299780901_5616306308235236351_o.jpg

Changamoto za daraja hili ni pamoja na:

1. Foleni ya ukataji tiketi (madirisha yako 14, yanafunguliwa machache).

2. Tozo kubwa kwa magari ya kawaida na abiria

3. Kutokamilika kwa barabara ya kutokea darajani upande wa Kigamboni.

Ni mwezi wa tisa tangu uzinduzi wa daraja na hakuna majibu ya msingi toka uongozi wa NSSF, Waziri wa Ujenzi wala Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge....) kuhusu lini kero hizi zitatatuliwa. Mapendekezo nimeshawapatia. Wao ni kuchukua hatua lakini inaonekana kuwa ni kazi ngumu kwao.

Natarajia kulifikisha suala hili ngazi ya juu zaidi.
[HASHTAG]#Kigamboni[/HASHTAG] [HASHTAG]#DarajalaNyerere[/HASHTAG]
 
Mh.mbunge,kiganboni ni shida. Mm nimeuziwa kiwanja kibada toka 2007.cha ajabu makaburi hayajaoondolewa. Nimezunguka wizarani mpaka nimechoka. Block 19 kibada
 
15895010_10154657047985901_5569511591226152551_n.jpg

Mbunge Faustine Ndugulile akiongea na wakazi wa Kisarawe II wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipotembelea Kigamboni kuongea na watumishi wa Halmashauri, kuzindua wodi ya Wazazi ya zahanati ya Kisarawe II na pia kutembelea kiwanda cha maziwa cha Milkcom.

======

Waziri Mkuu Aagiza Umeme Wa Uhakika Kisarawe II


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II linakuwa na umeme wa uhakika ili kuwezesha viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata nishati hiyo.

Alitoa agizo hilo wakati alipotembelea kiwanda cha Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na kiwanda cha Watercom kinachozalisha maji vilivyoko katika kata ya Kisarawe II wilayani Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

“Waziri wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata umeme wa uhakika ili kuviwezesha viwanda hivi kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika maeneo haya nao watanufaika na upatikanaji wa nishati hiyo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema amefarijika na jitihada za muwekezaji huyo za kuunga mkono mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya Tanzania kujenga uchumi wa viwanda utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Awali, Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar Faraj akisoma taarifa ya viwanda hivyo kwa Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo linasababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji.

“Punde umeme unapokatika tunalazimika kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji ambazo huumiza kiwanda kwa sababu haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,” alisema.

Faraji alisema changamoto nyingine ni miundombinu ya barabara ambayo usababisha wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda hivyo kwa urahisi, hivyo aliiomba Serikali kuwatatulia kero hilo.

Aliongeza kuwa kwa sasa viwanda hivyo vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo alisema endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa umeme na barabara wataongeza ajira kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2018.

Mapema Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe II iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi hiyo yenye vyumba vitatu itawapunguzia akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata huduma hiyo.
 
Taarifa kuhusu hatua ikiyofikia katika mchakato wa kukamilika na kuwasili Kivuko kipya. Taarifa rasmi iliyopo mpaka hivi sasa ni kuwa kivuko kipya kinachotarajiwa kuwasili kwa ajili ya kutoa huduma ya kivuko katika eneo la kivukoni (Ferry) jimbo la kigamboni mpaka hivi sasa matengenezo yamefikia asilimia themanini (80%)

Hivyo inatazamiwa mpaka ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu (2017) kivuko hicho kipya kitakuwa kimeshawasili eneo husika na kuanza kazi.
 
kig6.jpg

Hapa ni Daraja la Kigamboni
daraja 00.JPG

Hii ni barabarabra Itokayo darajani Kigamboni kuna hadi taa za barabarani
DSC01065.JPG

Hapa ni Mwisho wa barabara Itokayo Daraja la Kigamboni ambapo sehemu iliyobaki ni vumbi hadi njia panda ya Kibada.
DSC01067.JPG

Hii ndo sehemu inalalamikiwa ambayo wananchi wanasema haiendani na hadhi ya Daraja. Hii barabara ya vumbi inaenda kuunganishwa na barabara itokayo Kivukoni Magogoni kwenda Kibada.
mbili.JPG
mbili1.JPG

Hapa ndipo barabara itokayo daraja jipya la Kigamboni inapotokea Kwenye barabara ya Kibada Kivukoni. Kuanzia barabara ya lami itokayo darajani hadi hapa ndi njia panda ya Kibada ndio inayolalamikiwa.

Ni kipande kidogo kama Kilometa mbili au tatu(?).

Hivi karibuni January 30, 2017, SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walisema limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, katika daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Makusanyo hayo, imeelezwa, ni kuanzia katikati ya Mei, mwaka jana hadi mwezi January 2017 na ni juu ya lengo kwa asilimia 20.

Wanashindwa nini kutengeneza hiki kipande ambacho kinalalamikiwa?
 
Back
Top Bottom