Mjadala wa Mchakato wa kupata katiba mpya uliofanyika Geita jioni ya leo 8.8.11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala wa Mchakato wa kupata katiba mpya uliofanyika Geita jioni ya leo 8.8.11

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Sungurampole, Aug 8, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani wana jf

  Nimefuma mjadala huu ambao unaendelea sasa naona unaratibiwa na Mabere Marando
   
 2. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ngoja niwamegee machache niliyoyadaka kutoka mjadala huo:

  · Mahakama maalumu ipo tu khs muungano wa tz na zenj

  · Serikali imegawanyika mara 2
  - serikali kuu na
  - serikali za mitaa lakini kuna mkanganyiko katika uongozi katika ngazi ya wilaya.

  Wananchi katika wilaya wanaongozwa na:
  - DC -Anayechaguliwa na rais na anawajibika kwake. Ndiye mtawala na anayeamuru polisi. Hapigiwi kura
  - MBUNGE ambaye anapigiwa kuwa kura kuwawakilisha bungeni. Hana mamlaka.
  - Mwenyekiti wa halmashauri ambaye anachaguliwa na wananchi lakini hana mamlaka ya utawala

  · Rais ana madaraka amkubwa mno anateuwa watu wengi kufanya kusimamia wananchi

  · Kenya wamepitisha katiba mpya na wanapiga hatua kubwa sana- kwao wanaajiri hata mwanasheria mkuu, jaji mkuu n.k kwa kutuma maombi na kuhojiwa live on tv na wananchi wanaweza kutuma maswali

  · Wamehoji viti maalumu na

  · ukubwa wa serikali wizara uwepo ktk katika katiba mpya
  · Swali muswada huu unasomwa kwa mara ya ngapi? Jibu hii ni mara ya pili
  · watumishi wa nyumbani wanataka watambuliwe na katiba mpya.
  · Pendekezo la serikali za Majimbo
  · Japo sheria inasema wananchi wote ni sawa mbele ya sheria mbona rais hawezi kushtakiwa?
  · Hoja-ELIMU imeachiwa matakwa ya waziri anaibadili apendavyo. Inadidimiza elimu haswa lugha ya kufundishia
  · Rasilimali zidhibitiwe kunufaisha wananchi

  · Mawaziri wasitokane na wabunge

  · Ma DC watoke wilaya husika kwani wanayaelewa mazingira

  Mjadala unategewa kuendelea wiki ijayo


  nawasilisha
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa taharifa nzuri sana..
   
 4. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Huo ni ukweli!lkn inabidi kusimama imara katika mabadiliko ya katiba ili kumpunguzia mamla rais!Tuungane pamoja kubadilisha haya kupitia katiba mpya
   
 5. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Aksante kwa taarifa nzuri.
   
 6. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Mswada huu hapa anatakakusoma fungua hapa View attachment 61783989-Constitutional-Review-Bill-Revised-2.pdf [video] Scribd[/video]

  Sisi kwa upande wa zanzibar tutaukataa tena huu mswada bado una mitego mingi sana,haujatupa fursa za kweli kwa upande wetu zanzibar.

  Sehemu ya kwanza
  Masharti ya utangulizi
  Kifungu cha 2 kinahitaji marekebisho kwani kina kwenda kinyume na katiba ya watu wa Zanzibar hivyo kifungu hicho kina hitaji kisomeke kama hivi ifuatavyo:-
  Sheria hii itatumika Tanzania bara{Tanganyika} na mara baada ya baraza la wawakilishi la Zanzibar kuridhia sheria hio na kupitishwa na baraza hilo na kupata Baraka toka kwa rais wa Zanzibar na kua sheria hio inaweza kutumika Zanzibar .
  1-3 tafsiri inahitajika pia marekebisho :-
  Maana yake ni sheria ya msingi ,ilioandikwa na kukubaliwa na wananchi { neno isio andikwa liondolewe, ni udikteta au niseme uimla nahii ni hatari kwenye utawala bora} ambayo itaweka mifumo ya utawala katika mataifa ya Tanganyika {Tanzania bara } na taifa la Zanzibar , kwa kuainisha misingi ya mataifa hayo yalioungana, ambayo jamii italazimika kuifuata katika mgawanyo wa madaraka , na majukumu ya mihimili mikuu ya dola kwa kuainisha miundo ya serikali bunge, baraza la wawakilishi,na mahakama. “endeleza”
  KUHUSU KURA YA MAONI.sehemu hii isomeke kura itayo pingwa na wananchi ifutwe neno iliopingwa na wananchi. Kwani kuainisha tayari imeshapingwa kimandishi ya kisheria inamaana lolote lile litakaloamuliwa itakuwa sawa hata kama hio kura haito fanyika panahitajika pawe definite and very understandable juu ya maamuzi ya hio kura ya maoni.
  SURA HAPA PIA NIKOSEO SEHEMU HII INAONYESHA NI SEHEMU YA PILI WAKATI NI SEHEMU YA KWANZA BADO “In contents”
  2 Rais maana yake pahitajika pia marekebisho kidogo:-
  Rais maana yake ni rais wa jamuhuri ya Tanzania na rais wa Zanzibar kama ilivyo ainishwa katika katiba zetu mbili.
  .
  SEHEMU YA TATU.
  Utendaji wa tume:-
  5 pana suali hapa ninani atakae shauriana na kukubaliana na rais wa Zanzibar ?
  “Precise” 5 KINACHO AINISHWA HAPA NI UTENDAJI WA TUME.
  Hivyo basi pana hitajika pawe very clear na parekebishwe pawe panafahamika kwa uwazi zaidi” Tume baada ya kushauriana na kukubaliana na rais wa serikali ya jamhuri na rais wa Zanzibar,na kwa ushauri wa mwanasheria wakuu wa serikali ya jamhuri ya Tanzania na mwanasheria mkuu wa Zanzibar na kwa kuzingatia hali ya kijamii…………………..
  6-1 neno Tanzania Zanzibar liondoke na lije neno Zanzibar
  7-3 wajumbe watateuliwa kwa amri itayo tangazwa na magazeti ya serikali mbili ya jamhuri ya Tanzania na SERIKALI YA ZANZIBAR.
  9-2-(b) uwepo wa serikali bunge , baraza la wa wakilishi na mahakama.
  9-2-(d) uwepo wa serikali ya mapinduzi Zanzibar ni makosa kama mkataba wa muungano.
  unavyo elekeza badala yake IWE” UWEPO WA SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR (Kama mkataba wa muungano unavyosomeka)
  SEHEMU YA NNE.
  Baada ya kifungu cha 4 d kifunge cha 4-e kuwepo katiba ya uhuru wa jamhuri ya watu wa Zanzibar.
  4-f kuwepo sheria na kanuni baada ya mapinduzi Zanzibar .
  4-g hati halali ya muungano wa jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
  4-h katiba ya mpito ya jamhuri ya muungano Tanganyika na Zanzibar .
  Hii ni sehemu yakwanza mimi nimeona ni mapungufu.
  Wasalaam
   
Loading...