Mjadala wa katiba TBC

Singo Batan

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
292
191
"Katiba tuliyo nayo imeakisi misingi ya Wakoloni wetu sio Utamaduni wetu. "
Prof. Mahalu

"Katiba ya Sasa ilizingatia usalama wa Nchi na maendeleo kwa wananchi wake"
Prof. Lipumba

"Afrika Kusini ina katiba Bora sana, Kenya ina katiba bora pia, Uganda vile vile. Lakini Afrika Kusini ni miongoni mwa Nchi zenye ubaguzi sana. Katiba sio muarobaini wa shida zote" Dkt. Chacha Rioba akimnukuu Prof. Shivji

"Katiba bora inapaswa kuanzia katika nia njema ya wananchi wenyewe. Katiba haitekelezeki kama hakuna msukumo chanya na uelewa wa wananchi, Wananchi wanapaswa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya Katiba. Kama wananchi hawana uwezo wa kuhoji juu ya masuala ya kikatiba, katiba hiyo haina maana kuwepo"
Dkt. Kinunda

"Katiba yaweza kuwa nzuri, lakini utashi wa kisiasa ni muhimu kuliko Maandiko ya katiba yenyewe. Tumeingia katika mfumo wa uchumi wa kati ya ujamaa na ubepari, katiba bora ya huendana na matakwa ya sasa, Katiba ni ya Wananchi sio vyama vya siasa" Mhe. Hamad Rashid (Mkiti ADC)
 
TBCCM? Mjadala wa katiba TBC? Maajabu hayo. Nimestuka. Ni sawa na kusikia mjadala wa kitimoto kwenye msikiti ama kanisa Sabato! Ukisikia kitomoto kinajadiliwa msikitini basi ni mjadala hasi kuhusu kitimoto. Mjadala kuhusu katiba mpya TBCCM ni mjadala hasi - lazima.
 
Back
Top Bottom