Mjadala wa Bashite wazidi kutanuka

1.magufuli
2.Bashite
3.Majaliwa
4.
5.
6.
7.....
8.....
9.mama samia
 
Na

Makonda hakupata zero aliyepata zero ni bashite yule wa kolomije misungwi mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa dar. Nampa pongezi maana hata manaume wa dar wote ni vilaza.
Kilaza babako,Je aliyefeli sekondari anawezaje kumudu masomo ya Chuo,Mimi mwanaume wa Dar ndio maana nimekujibu acha UPOYOYO
 
Siamini kama utata wa elimu yake ulikuwa 'siri'. Kuna waliojua ndiyo maana habari imejulikana mapema. Pia siamini kama kitu hulipuka ghafla; kabla ya mvua huwa kuna fukuto na pia kabla ya volcano kuna kufoka Moshi au vumbi, na kabla ya tetemeko pia huwa kuna dalili.

Kweli Makonda ameudhi wengi aliowatuhumu kuhusika na madawa ya kulevya, lakini hapo nyuma alishaudhi watu wengi pia. Kuna tuliochukizwa na kilichotokea kwa Warioba, kuna tuliochukizwa na picha za kufunga viatu na kumbeba mtu fulani! Kuna tuliochukizwa na utumbuaji wa Kabwe, na tuliochukizwa alivyomsemesha afisa ardhi wa manispaa na Mimi binafsi nachukizwa sana na anavyojifanya yeye ni mungu. Kwa kifupi ame create maadui wengi.

Zoezi la kuhakiki vyeti ndio Hilo linaendelea na kuna ambao tayari wameshaathirika. Naamini yeye akuhakikiwa kwa vile kuna taasisi ambazo Zina jukumu la kuhakiki viongozi wa ngazi yake. Lakini kwa vile watu walishamtaja basi taasisi husika zilitakiwa zichukue hatua Mara moja.

Mimi binafsi pamoja na kuchukizwa na mambo yake, nilikuwa natamani Rais achukue hatua stahiki kwa huyu 'kilaza' ambaye anastahili kumuamkia mpaka mesenja wake. Rais anatuaminisha kwamba yeye ni msema kweli, asiyeogopa mtu yeyote na ambaye hatamvumilia mvunja sheria yeyote, lakini kwa hapa, nimepoteza imani na Rais wangu. Nimepoteza matumaini na future yangu na ya watoto wangu. Sijui nchi hii inaenda wapi. Ninachokiona ni chuki zinapandikizwa na ukabila uliopitiliza.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 

Well said Mkuu,...sijui kwa nini watu wanakufa ganzi kwa haka katoto

Kule Colombia, alikuwepo muuza na msambazaji mkubwa wa madawa ya kulevya akiitwa Pablo Escobar, zaidi ya 80% ya madawa ya kulevya yaliyoingizwa US huyu jamaa alikuwa responsible...alikuwa na pesa ya nguvu. Huyu bwana alitumia pesa hiyo haramu kujenga mashule, mahospitali na kusomesha watu kwa kutoa scholarships....hii haikuondoa ukweli kuwa alikuwa mkosaji. Kule Jamaica kuna mtu alikuwa akiitwa Dudu...similary alifanya na alikuwa kama Escobar...sasa hivi yuko Jela kutokana na uovu wake...pamoja na kwamba pesa haramu aliyokuwa akiipata aliitumia kwa jamii yake na kwa starehe zake.

Wandugu tusiondoke kwenye mambo ya msingi na ni very very basic...na hasa kwa watu walioenda shule za uhakika...kukubali uovu wa elimu wa aina yeyote ni kujishushia heshima na kudharau umuhimu wa elimu...shame on us!

Juzi juzi tu...matamko yametoka kuhusu uhakiki wa qualification za watu waliopo mavyuoni...na maofisini....wengine walikuwa wamesha-advance...na waliondolewa...kwanini kwa watu wengine isifanyike hivyo hivyo?

Kama mnampenda sana mtu kuwa kiongozi haina shida....lakini record zake ziwekwe straight...kama mkimsamehe kwa makosa aliyofanya....hilo ni suala jingine...lakini taarifa ni muhimu zikawa sahihi. Hivi tunawafundisha nini watoto wetu tukikubali udhaifu huu?
 
Je wale waliotumbuliwa mchango wao ulikuwa hauonekani?
 
Duh

Bado wanaendeleakuwavuta nyie wafata mikumbo

Ha ha haaaa

Wote hao wameguswa

Mzidi kushangilia

Makonda oyeeeeeeeee
 
Waliosoma naye Sekondary wanamjua kuwa ni Daud Albert Bashite,matokeo yake ya kidato cha nne wanayajua kuwa ni 0,wanajua tangu zamani alitumia cheti cha mtu mwingine kufika hapo alipo,wanajua wanaeelewa,hawkuwahi kusema 7 bu walijua alifanya hivyo kutafuta maisha kama watu wengine wote,walofeli f4 na wakatumis vyeti vya watu wengine wapo wengi,kila mtu akiruhusiwa angalau watano watatajwa wengi mno,

Kinachotokea kwa huyu bwana ni ile dhana ya ukimwaga mboga namwaga ugali,kwamba kwa vile ana mapungufu usiseme mapungufu ya wengine,
 
Ila tumeshaichoka hii hadithi, for real
Ndo tatizo kuubwa Sana linalotukabili watanzania. Nilidhani tutasimamia Bashite ahakiki vyeti vyake mpaka tuujue mwisho. Wafanyakazi wa serikali wamehakikiwa vyeti vyao kwa vitisho bila kujali gharama za waliokuwa mbali ya vituo vyao vya kazi kwa sababu Kama za masomo, kuuguza nk. BASHITE KAHAKIKI VYETI VYAKO
 
Vyeti ni kwa ajili ya muajiri tu...hakuna sheria inayomlamzimisha kiongozi au mtanzania yeyote kuonyesha vyeti mtandaoni.
 
Matokeo tuliyonayo kutoka PAMBA SECONDARY SCHOOL yanaonyesha Daud Albert Bashite Alipata divisheni Zero!
 
Asante sana kwa maelezo ya kweli na mifano hai.
Bado kuna watu ambao hawataki kabisa kuelewa, na wengi wanaelewa ila wanajitia upofu.
 
Umesema vyema kwamba utendaji wake ni Mauro japo kwa hili kwangu no comment.suala la kuhakiki vyeti halihusiani kabisa na utendaji vinginevyo wangehakiki utendaji wa watu na sio vyeti,tunachotaka ni kuondoa double standard kwani wapo watendaji wengi wazuri wameachishwa kazi kwa sababu ya vyeti. Unalisemeaje hilo?
 
Alafu tunaweza kudharau hizi habari zinazo circulate hapa JF, mimi naona ni sahihi na taasisi yoyote ya umma au binafsi inatakiwa kutolea maelezo (clear doubts) kwa habari zilizotokea hapa. wanavyodharau wanaonyesha uwezo mdogo wa kufikiri walio nao.
Mfano, habari za kukamatwa Mh. Tundu Lissu (Mbunge) jana zilianzia hapa kwa yeyey kuongea na umma wa JF. Baadae sote tunajua kilichofuata! Pia reliability ya JF ni ukweli kwamba taasisi za binafsi na za umma ni verified users, mfano TCRA , TPA , NMB Tanzania.
Kwa nini basi serikali au RC asiondoe huu wasiwasi na uvumi kuwa Bashite na Makonda ni kitu kimoja au la!?
 

Hili mkuu nshalisemea kwa mara nyingi sana....hasa kwa watu kama nyie....tunaposema mtu anatumia vyeti ambavyo sio vyake we mean kasomea umakenika but anafanya kazi muhimbili na hana taaluma hiyo,Mjenzi wa makaburi anaenda kujenga madaraja hii ndo haitakiwi...kwa Makonda ni ishu ya kawaida tu....hakunaga sehemu walishaitisha interview ya ukuu wa mikoa au wa wilaya au ubunge,hii ni kuchaguliwa au kuteuliwa tu.Double standard yako haina maana hapa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…