Mjadala unaoendelea EA Radio kuhusu mavazi na mitindo

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
26,265
2,000
Naskiliza EA Radio muda huu. Zembwela na wenzake studio wanajadili kushamiri kwa mahusiano holela miongoni mwa vijana, pia wanazungumzia tabia ya vijana kupenda kulelewa na majimama.

Mgeni mualikwa ktk kipindi anazungumzia uvaaji wa VIKUKU kwa wadada huku wakiwa hawajui tafsiri halisi ya utamaduni huo kutoka huko ulikotoka.

Zembwela ameenda mbali zaidi na kutoa ushuhuda kuwa ana jamaa yake Amsterdam amemuelezea kuwa kuna rangi za mavazi mtoto wa kiume hatakiwi kuvaa.

Zembwela anasema Mwanaume hutakiwi kuvaa nguo za rangi kama pink na zambarau. Zembwela amesema mtoto wa kiume kuvaa nguo ya pink, ikatokea UKASHIKWA TAKKO usilalamike!

Mjadala unaendelea sasa hivi EA Radio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom