Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 4,953
- 6,071
Nimekaa na kutafakari sana juu la hili jambo, Shaffi Dauda ameweza kufanya vitu vingi Sana kwenye mchezo wa soka hapa nchini,
Nakumbuka mwaka 2014 aliweza kubuni soka la ufukweni wakishirikiana na TFF pamoja wadau wengine kama Boniface Pawasa na wengineo
Mashindano yalishirikisha vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu jijini Dar es salaam, hakika ulikua ubunifu wa hali ya juu sana, nami nina medali ya mshindi wa pili wa fainali ile ya kwanza ya beach soccer
Shaffi huyu huyu amebuni ndondo cup, zamani tulizoea kucheza mitaani lakini haikua na nguvu kubwa kama sasa, tumeona ndondo cup imeweza kuwatoa wachezaji kadhaa na wengine wapo timu ya taifa
Wengi walioko katika shirikisho la soka hawana vision na huu mchezo, tunataka watu ambao watatuvusha kutoka hapa kwenda hatua nyingine nzuri zaidi
Ile sehemu wameunda kikundi chao cha kugombea kiasi kwamba hawataki baadhi ya watu washike zile nyazifa, tunataka maendeleo ya mpira na tutayapata kama tutakua na watu sahihi katika nafasi hizo
Najua kuna wengi wanamchukia huyu jamaa lakini hii haiondoi mazuri yote aliyofanya kwenye michezo hapa nchini,
Kama kweli tunataka kupiga hatua kwenye mchezo huu pendwa basi hatuna budi kuweka watu sahihi katika nafasi sahihi, mtu kama Ali Mayay anafaa sana kuongeza lile shirikisho inasikitisha waliopiga kura hawakuona umuhimu wake,
Simfahamu Shaffi hata kidogo lakini naona ni mtu ambaye ana ubunifu mkubwa kwenye soka, yule ni fursa na hatuna budi kuitumia