Mjadala : Tunasubiri nini kumpa nafasi Shaffi Dauda kuongoza TFF?

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,947
6,057
Nimekaa na kutafakari sana juu la hili jambo, Shaffi Dauda ameweza kufanya vitu vingi Sana kwenye mchezo wa soka hapa nchini,
Nakumbuka mwaka 2014 aliweza kubuni soka la ufukweni wakishirikiana na TFF pamoja wadau wengine kama Boniface Pawasa na wengineo
Mashindano yalishirikisha vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu jijini Dar es salaam, hakika ulikua ubunifu wa hali ya juu sana, nami nina medali ya mshindi wa pili wa fainali ile ya kwanza ya beach soccer
Shaffi huyu huyu amebuni ndondo cup, zamani tulizoea kucheza mitaani lakini haikua na nguvu kubwa kama sasa, tumeona ndondo cup imeweza kuwatoa wachezaji kadhaa na wengine wapo timu ya taifa
Wengi walioko katika shirikisho la soka hawana vision na huu mchezo, tunataka watu ambao watatuvusha kutoka hapa kwenda hatua nyingine nzuri zaidi

Ile sehemu wameunda kikundi chao cha kugombea kiasi kwamba hawataki baadhi ya watu washike zile nyazifa, tunataka maendeleo ya mpira na tutayapata kama tutakua na watu sahihi katika nafasi hizo

Najua kuna wengi wanamchukia huyu jamaa lakini hii haiondoi mazuri yote aliyofanya kwenye michezo hapa nchini,
Kama kweli tunataka kupiga hatua kwenye mchezo huu pendwa basi hatuna budi kuweka watu sahihi katika nafasi sahihi, mtu kama Ali Mayay anafaa sana kuongeza lile shirikisho inasikitisha waliopiga kura hawakuona umuhimu wake,
Simfahamu Shaffi hata kidogo lakini naona ni mtu ambaye ana ubunifu mkubwa kwenye soka, yule ni fursa na hatuna budi kuitumia
 
Shafii kumbe upo jf na ww mkuu? Username yako ya ajabu
 
Katika Ubunifu na utekelezaji sina shaka shafii ni mtu sahihi Tatizo lake ni mnazi wa Yanga aliyepitiliza hafichi mapenzi yake jambo ambalo si zuri kwa kiongozi
Kwani Karia na Kidau sio wanazi wa Simba kupitiliza?au Malinzi na Tenga sio Yanga?mbona ni viongozi na wengine waliwahi kuwa viongozi wa Tifuatufua hiyo sio sababu
 
Mchambuzi wa soka kwenye media sio management ya soka, wenye kumbukumbu mnajua kuwa baadhi walishampendekeza Dr. Rick apewe ukocha wa Taifa stars!
Shafi anafit sana hapo alipo na ndio maana mchango wake unaonekana dhahiri. Ukimuuliza anaweza kukueleza kwa usahihi ni nani (akina nani) anastahili kuongoza mpira wa Tanzania au hata ni structure gani itumike.
 
Kama anafanya vema hapo alipo aendelee tu kufanya vema hapo hapo alipo.. ?, kwani hawezi kuendelea kubuni mpaka awe kiongozi ?
 
Back
Top Bottom