Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Kwa kuzingatia kasi, utendaji na 'utumbuaji majipu' wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Magufuli, ahadi yake ya 'sitawaangusha' bado iko imara? Vipi kuhusu chama chake cha Mapinduzi hakitamkwamisha na kufanya atuangushe watanzania?
Binafsi, Rais Magufuli na Serikali yake wameanza na wanaendelea vizuri hasa katika kushughulika na kuongeza mapato ya Serikali. Ingawa sioni sahihi sana kufuta posho zote za vikao. Vipo vikao yapasa kurejeshewa posho zake. Mfano, vikao virefu na vile vya juu katika Taasisi. Ilipaswa kuwekwa malipo ambayo hayatazidi kiasi fulani kitakachowekwa.
Kufutwa kwa posho zote, kwa mtazamo wangu unaozingatia hali halisi ya nchi ilipo, kutashusha morali ya kufanya vikao vya kikazi. Wahusika wengi muhimu watakuwa wakiwasilisha udhuru tu vikaoni. Kuhusu kutumbua majipu, Serikali haipaswi kuwa na huruma ya kisiasa. Kila anayehusika ashughulikiwe ipasavyo.