Mjadala: Serikali ya Tanzania kuchukiwa na idadi kubwa ya vijana wake. Tatizo la msingi ni nini?

Wengi wana akili za kubet na ni mtaji wa wanasiasa...uwezo wao wa kufikiria ni mdogo sana..
 
Labda kwa sababu Serikali haijatimiza ila Ahadi ya kutoa Million 50 kila Kijiji.!!! Hata Hivyo Ubaya Unavuma kuliko Wema.
 
Serikali iliyopo madarakani ndio nchi yenyewe hiyo. Najua utabisha. Wao ndio wanadhamana ya ulinzi wako, chakula na maji yako, elimu na welfare yako kwa ujumla.
Wewe kama hujui uliza uambiwe, umeleta thread sasa naona unadandia gari kwa mbele... Serikali na nchi vitu viwili tofauti .. Nchi yangu ni Tanzania. Tanzania ilivyokuwa chini ya uongozi wa Nyerere, ni tofauti na Tanzania ya Mwinyi, Jakaya na zaidi sasa ndiyo tofauti mmmnnooo chini ya serikali hii ya sasa. Mimi Mtanzania naipenda saaana, tena Mimi nikwambie ni Mzalendo hasa lakini siyo lazima niipende serikali hii. Isitoshe sikiliza kuwa Mzalendo siyo lazima uipende serikali iliyopo madarakani. Naipenda nchi yangu lakini ikiwa serikali iliyopo madarakani inaenda inatupeleka siko nitaipendaje hiyo serikali. Katiba inasema no body is above the law.. Iweje mtu leo avunje mchana kweupe sheria namba 5 ya vyama vya siasa!! Hakuna Uhuru wa kutoa ama kupokea maoni, hakuna Uhuru wa kukutana na nasisitiza siyo kwamba katiba/sheria zinakataza Nooop ni mtu mmoja tu anazuia utekelezaji wa sheria/katiba. Nitaipendaje serikali hiyo!!! Tuache UNAFIKI tunakokwenda siko. Way forward.. Tuseme nooo. Tusiombe bali tuitake katiba ya Warioba. Tuache ukondoo

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Wewe sasa utakuwa mchochezi, unachochea tu,unachochea tu.Lakini uchochezi ukienda mbaliii utaambiwa unawashwa washwa.
 
Wewe sasa utakuwa mchochezi, unachochea tu,unachochea tu.Lakini uchochezi ukienda mbaliii utaambiwa unawashwa washwa.
 
Wewe sasa utakuwa mchochezi, unachochea tu,unachochea tu.Lakini uchochezi ukienda mbaliii utaambiwa unawashwa washwa.
 
Our government (under the green party) is unjust, unwise and do not adhere to national constitution, principles of democracy and the rule of law.


Hzo ndyo sabb japo ni ngum kumeza hasa kwa wasaka tonge
 
Na mimi kwa kuwa ni Mzalendo waache waseme NAWASHWA waache waseme lakini sitaacha kusema kwa sababu napenda niione Tanzania yangu yenye NEEMA siyo Tanzania yenye madeni yasiyolipika. Sitaki Tanzania itakayotengwa kidipromasia. Sitaki Tanzania ambayo watu wake 65% ambao ni vijana hawana mapenzi na nchi yao. Sisi wakati tunamaliza mafunzo ya JKT, na wakati ule mafunzo ni mwaka mmoja siyo wiki 6 walizoenda akina Zitto na Halima Mdee, mwaka mmoja; vijana uliwaona wakiwa na ari KUU ya kuitumikia nchi. Hali ile leo ipo wapi!!! Vijana wapo mitaani, wamepigika, wametulia kwa shiiida, wanasiasa hao wa upande ule, eti tuna "amani" Jamani amani ni tunda la HAKI ya Mungu. Mtu kukaa kimya siyo lazima saaana kuwa ana amani. Ametulia hatujui yaliyo moyoni mwake. Amani inatoka ndani ya mtu, huwezi kuiona kwa macho, maana siyo kila anayekenua meno,, kuwa eti anacheka.
 
Picha hapo chini zinaonesha jitihada za serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika kusaidia wahanga wa ajali ya bus la wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent iliyotokea wilayani Karatu katika mkoa wa Arusha.

View attachment 527790

View attachment 527792

Licha ya juhudi zote hizi bado vijana wanatukana sana serikali yao? Tatizo ni nini hasa?

Gharama zote za mazishi kuanzia jeneza, mochwari, usafirishwaji wa miili mpaka majumbani mwa wafiwa, the government paid all these, but guys hawapo thankful kabisa? Kila siku ni matusi na kejeli kwa nchi yao, kwanini?

Ina maana hakuna jema serikali inalofanya hata kustahili sifa?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Viongozi wenu wanajituma sana kuwahudumia kadri ya uwezo wao na hali ya uchumi wa nchi. Learn to be thankful hata kwa vitu vidogo kama hivi.

Najua nitatukanwa, kukejeliwa na kuitwa najipendekeza na kila aina ya jina, lakini tatizo la msingi ni lipi kati ya vijana na serikali yetu ya Tanzania?

Nothing is easier than blaming others for your own problems. Hakuna jambo rahisi kama kulalamikia serikali kwa matatizo yako wewe mwenyewe.

Nawasilisha.
Unajitekenya mwenyewe unacheka mwenyewe bavicha mna vituko hapo na wewe utapewa viti maalum kwa utafiti wako uchwala labda vijana wa hai
 
Taabu wengine tulizoea kukaa vijiweni pesa zikitukuta hapo na kutamka unatujua sisi akina nani nenda popote.
 
Bora ujisemehe kwa nafsi yako kama labda unaipenda au unaichukia serikali.
Ila mm kwa upande wangu kama kijana nnaipenda mno serikali yangu na pia nnafurahia kazi nzuri inayofanya kutuletea maendeleo. Napia nnaiunga mkono kwa asilimia zote

Hahahaaa! Mkuu nimekuelewa sana...Ila avatar yako imenishtua kidogo..hahahaha
 
Vijana wengi wanaomaliza masomo na kukosa ajira ni bomu ambalo serikali inaliandaa bila kujijua...
+kufungwa mgodi wa bulyankulu ajila2000.+precission air kupunguza ajila watu136.+watumishi hewa elfu 19 na ------.hata kichaa lazima akuchukie
 
Mbona matusi kila siku humu JF kwa Serikali? Sisi vijana nani ameturoga?
- Hivi kijana anawekewa vikwazo vizito, anaishi kama yuko kwenye moto unategemea nini. Serikali haina mpango wowote na vijana, kila inakowaona inawachukulia kama majambazi.
- Ajira wananyimwa kwa makusudi tu au wanawekewa mazingira mazito ya kupata ajira
- Vijana hawapewi mikopo, wanazurula tu wakisema wawe machinga wanapigwa mabomu kama majambazi
- Wakitaka wafanye biashara rasmi wanakabwa na TRA, TFDA, NEMC, OSHA wakati hata mradi haupati faida yoyote na hawapati TAX HOLIDAY yoyote
- Kwa mazingira hayo unategemea VIJANA wasupport serikali wakati imeweka Juhudi kubwa ya kuua ndoto zao ?
 
+kufungwa mgodi wa bulyankulu ajila2000.+precission air kupunguza ajila watu136.+watumishi hewa elfu 19 na ------.hata kichaa lazima akuchukie
For your information hao waliochishwa Kazi watazalisha ajira,
Suppose baadhi wakaanzisha gereji kama ni Fundi, baadhi wakaanzisha maduka ya vifaa vya ujenzi au magari, baadhi wakaamua kuwa maconsultants, na wengine wakaamua kuwa hata wakulima wa kisasa(Namaanisha trekta nk)

Mbona watamultiply hizo ajira.

Msiwe na akili mgando za kimaandamano maandamano, ulimwengu wa Leo ni kuwa creative especially unapokuwa na mtaji.

Watu wengi Migodini kutokana na uncertainties washajenga kwa hiyo wako standby kwa lolote.
 
Back
Top Bottom