Mjadala - polisi ifikishwe mahakamani dhidi ya mauaji ya raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala - polisi ifikishwe mahakamani dhidi ya mauaji ya raia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 4, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Watanzania wenzangu, binafsi naona upo umuhimu wa Idara ya haki za binadamu ya Chadema na wakereketwa wengine kuifungulia mashtaka polisi mahakamani, kwani tukio la Iringa lina ushahidi tosha ambao ndio pa kusimamia kujenga hoja, na katika hili naona vyombo vya habari vimeguswa kwa kuondokewa na mmoja wapo katika tasnia yao.

  Bila hatua hiyo, kwa vile utawala umepanga hayo yatokee, basi mchezo utaendelea na hatimaye mabomu hayo ipo siku yatatua na kusambaratisha viongozi wa siasa wa upinzani na wanaharakati wengine. Ni maoni ya ndoto yangu, lazima tuamue na hatua ichukuliwe.

  Tundu Lisu alivyosema kuhusu yaliyotokea Morogoro,
  leo yametokea tena Iringa kukiwa na ushahidi usiopingika,
  • sababu tunazo,
  • uwezo tunao,
  • haki tunayo,
  kilichobaki ni utoshelezwaji na utekelezaji wa kisheria ukamilike na iwasilishwe kwenye mhimili wa Mahakama kupata haki yetu tunayostahili kulindwa na polisi badala ya polisi kugeuza raia ni uwanja wa kujizoesha kulenga shamba.


  Nawasilisha.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi naungana nawe katika hoja hii, kwani kusononeka tu, kulalamika tu hakutatusaidia wakati adui akifurahia ushindi kwa alichokusudia, ndio unaweza kuona wanaotuhumiwa kuhusika nyuma ya pazia wanazidi kuswindika pamba masikioni mwao kana kwamba hawajui kilichojilia wakati ndio wimbo wa vyombo vya habari kila kukicha.

  Hatua muhimu inahitajika kuchukuliwa mara moja kama ulivyodokeza kwamba Tundu Lisu aliongea katika Mkutano wa Morogoro baada ya raia moja pia kuuawa na polisi kwamba Kamanda wa "Polisi Morogoro atatafutwa na wanasheria awe amevaa magwanda au ameyavua," Mwisho wa kumnukuru Tundu Lisu. Tunasubiri utekelezaji wake.

  Mahakamani ni mahali pekee ambapo wapenda mageuzi na wenye kulinda himaya zao ushindani wa kisheria utakapoweza kuchukua mkondo wake, pale hakuna kumtazama mtu usoni na hata wenye kifumbo haruhusiwi kuingia nacho, ni kama alivo na pamba zake tu na hapa mabishana na hoja za kisheria zinaposhindaniwa. Mnakumbuka Mkapa alivyonyooshwa na maswali ya wanasheria, haijalishi wewe nani, mkuu pale ni hakimu aliyekalia kiti cha 'Litostrotos,' kwa kiyahudi 'Gabata.'

  Hili la kukaa meza moja nao ni sawa na kuzidi kuwaabudu, na kitakachofanyika pale ni wao kutoa maagizo zaidi ya utekelezaji wa malengo yao dhidi ya wanyanyaswa. Ndicho kilichotokea Leo Iringa. Wakati Chadema wanakatazwa mikutano, CCM inafanya mkutano mkubwa upande mwingine wa nchi kufungua kampeni za kisiasa wakati kote wanafanya sensa.

  Nakubaliana nawe CS, kama alivyofanikiwa Mchungaji Mtikila kuiburuza serikali mahakamani na kushinda kesi kadhaa, kuna haja kwa Chadema kujipanga kisheria kwani wanao wataalamu wengi tu katika fani hii na kuweza kuibwaga serikali, kwani serikali inatumia zaidi vitisho kuliko sheria inayoongoza nchi na mara kadhaa hufanya mambo kinyume cha Katiba ya nchi.
   
Loading...