MJADALA:-Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,712
10,205
Nimeonela tuijadili hii sentensi na kuona INA Fanya KAZI kiasi gani maishani mwetu. KWELI KUTUWEKA HURU.
1. Kweli ni nini?

Ni maneno, matendo na Matukio halisi yasiyo na nyoongeza au mapungufu yanayotolewa au kusemwa au kuonyeshwa mahali yanapotakiwa.


2. Uhuru ni nini?
Ni Haki au nguvu ya kuongea, kufanya jambo Fulani, kufikiria kama utakavyo bila kuingiliwa , wala kubughudhiwa na bila kuwa na shaka yoyote.

Je kweli inakuweka huru?
Hapana.
Kwa dunia na maisha ya Leo kweli imekuwa ni balaa, kweli imekuwa ni mkosi,kweli imekuwa bidhaa adimu kupatikana. Kweli inaogopewa na kila MTU.
Ukiongea ukweli utachukiwa (adhabu)
Ukiongea kweli utafukuzwa KAZI (adhabu)
Kama ulifanya kosa Fulani, ukafikishwa mahakamani na ukakiri utafungwa jela au utalipishwa faini (adhabu)
Ukienda nje ya ndoa na ukakiri utaachika (adhabu)

Kweli ni adhabu.
Naomba mawazo yenu ili vidogo yanijenge na kunipa Tumaini na imani ya kuwa mkweli ili niwe huru.

UTAIJUA KWELI, NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU, NAWE UTAKUWA HURU KWELIKWELI.
Haya si maneno ya YOHANA Mbatizaji, ni maneno ya YOHANA Mwinjilisti aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu. Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda zaidi.
Katika wanafunzi wa Yesu huyu jamaa peke yake ndiye aliyeuona uzee. Wengine wote waliuawa wakiwa vijana wakichapa injili.
Katika shuhuda za kufurahisha ni neema kuu aliyokuwa nayo huyu jamaa. unaambiwa ukimpiga ngumi basi yeye hatoumia, na Yale maumivu utayasikia wewe Mara mbili zaidi. Ukimpiga mshale, ule mshale utamgonga yeye kisha kuja kuua wewe.
Huyu jamaa akawa hakamatiki kirahisi, kila MTU alimuogopa. Wakasuka mpango akakamatwa akapelekwa kwenye kisiwa kilichojaa upweke cha Patmos. akakaa huko kwa muda mrefu sana bila ya kula wala kunywa kitu akifanya meditation ambayo hata ndugu yangu mpenda mshana jr hawezi kamwe kufanya, akaona maono mbalimbali ya nyakati za mwisho. Huyu ndiye aliyetabiri Habari za namba 666 The mark of the beast.
Huyu ndio YOHANA a.k.a Bujibuji
 
Back
Top Bottom