Mjadala: Kwanini vichaa hawaugui ovyo?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,863
Kichaa anaweza kutembea ovyo tu na kuokota chochote anachokiona hata jalalani na kula lakini huwezi kusikia akilalamika tumbo linauma sasa jaribu wewe ambaye upo normal uone kama hujahamia toi...What is the reason behind?

----------------

 
Nakusauri fanya tafit za kina, cna shaka ktk hili wanaumwa na umaut unawakuta bila shaka br
 
kichaa anaweza kutembea ovyo tu na kuokota chochote anachokiona hata jalalani na kula lakini huwezi kusikia akilalamika tumbo linauma sasa jaribu wewe ambaye upo normal uone kama hujahamia toi...what is the reason behind?

Hii ni myth, tu.
Hawa ni binadamu na wanapata magonjwa kama kawaida.
 
kuna chiz mmoja kitunda anaitwa Ally anamiaka minne hajawahi kuumwa hata mafua
 
Nadhani wote mnaipata ile MAGIC POWDER, dawa ya kuozesha ndevu. Sa kuna kichaa alipita bombani akajaribu kufungua koki akashindwa, akaamua kuchota maji yaliyokua kwenye dishi ambayo huwa taka za magic zinatupwa humo akanywa, na hajadhurika mwenzi wa pili huu.
 
Hii ni myth, tu.
Hawa ni binadamu na wanapata magonjwa kama kawaida.

Hata km ni myth unavosema lkn maradhi hayafichiki na wala hakuna anaeweza kuhimili unapoumwa nijambo lakujiuliza asilimia ya kukutwa wakiumwa ni ndogo wakati kiuhalisia wao walitakiwa waongoze kwanza wanalala mtaani,majalalani kula mbovu lkn wanachukua mda kupata maradhi
 

Ukienda K/KOO kuna watoto watu wanalal nje, kuna watot wa mitaani pia, nao huwakuti wamepanga folen Hospitali lakini si machizi, ishu ni kwamba mwili una develop kinga ukikutana na condtion fulani. Lakini si kwamba hawaumwi..
 
Mwili una tabia ya kujilinda kwa kutumia ulinzi asilia wa mwili (natural body immunity). Na ulinzi huimarika sana kama hautumii kitu chochote kingine cha kusaidia ulinzi asilia wa mwili. Na ulinzi hujengeka zaidi kama adui (vimelea vya magonjwa) wataushambulia mwili mara kwa mara. Chukulia mfano wa jeshi linalopambana na maadui mara kwa mara na lile linalokaa tu kutegemea msaada toka UNO. Ni dhahiri kuwa hili linalopambana mara kwa mara litakuwa imara zaidi.
Vichaa hawaugui kwa kuwa kinga yao ya mwili imeimarika sana kwa kuwa mara kwa mara hushambuliwa na vimelea vya magonjwa. Linganisha pia na mtoto anayekulia kwenye maisha magumu ya kijijini na yule wa mboga saba wa Masaki. Huyu wa kijijini anakunywa maji ya kwenye lambo ama mtaroni ambapo hata ng'ombe anakunywa lakini haumwi tumbo. Huyu wa Masaki akinywa maji ya dawasco yasiyochemshwa na kuchujwa anaugua.
Nawasilisha
 
unazungumzia vichaa gan chief?... mbona Hata humu jukwaan tunao vichaa wengi sana ,wanaugua na kufa pia?
 
Ukienda K/KOO kuna watoto watu wanalal nje, kuna watot wa mitaani pia, nao huwakuti wamepanga folen Hospitali lakini si machizi, ishu ni kwamba mwili una develop kinga ukikutana na condtion fulani. Lakini si kwamba hawaumwi..

Tofautisha baina ya chizi na mtoto wa mtaani. Mtoto wa mtaani anaakili zake akilala anajua vipi ajikinge hata na mbu akilala hukimbilia karibu na jumba za watu tofauti na chizi hana care kabisa kuanzia kula wala kulala huishia kula maembe yaliozaa kabisa na matunda ni shuhuda wa macho yangu kuona hayo kale ww sasa uone kazi au ale mtoto wa mtaani nijambo lakushangaza
 

Nimesha sema clear hapo juu, kuwa ukiwa katika condition flan mwili hulazimika kutengeneza kinga.....hao watoto wa mitaani pia umeona wakilal kwenye net? wakichemsha maji? Wakifua nguo? wamekuw expsoed sana katika mazngira hatarishi mno, ila kwa ujumla ni kuwa wamedevelop kinga after kuwa exposed
 

Umesema vema sana,.
 
Umewahi kuishi na vichaa wangapi ukagundua hili?

Lakini pia kumbuka mfumo wa fahamu uongoza matukio mengi sana ndani ya mwili wa binadamu, hawa tayari ni wagonjwa koz mifumo yao ya fahamu haifanyi kazi vema hivyo pengine siyo rahisi kugundua ni wakati gani wanasumbuliwa na magonjwa mengine.

Mita yako ya maji kama haisomi haimaanishi kwamba maji hayapiti.
 
unazungumzia vichaa gan chief?... mbona Hata humu jukwaan tunao vichaa wengi sana ,wanaugua na kufa pia?

inawezekana wapo wa aina nyingi ila me nazungumzia wale wanaokula kula ovyo sehemu hatarishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…