Mjadala kuhusu Mfumo wa Soko Huria na Ongezeko la Wahitimu Nchini - LIVE ON STAR TV

Vyuo vikuu vinafanya biashara zaidi kuliko kuzingatia ubora wa wahitimu. Serikali imechangia sana kuwepo vya vyuo vikuu visivyokidhi vigezo.

Mathalani hivi karibuni ilitolewa taarifa na TCU kwamba vyuo vikuu vingi hasa vya binafsi havikidhi vigezo, kama wangefuata sheria vyuo hivyo vingefungwa. TCU imekubali kukiuka kwa sheria kwa faida ya nani?

Siasa nazo zinachangia sana kuvuruga mfumo wa elimu kwa viongozi kufanya maamuzi ya kutaka kuwahadaa na kuwafurahisha wananchi lakini kwa kufanya hivyo wanaharibu na kushusha ubora wa elimu, as a result wanakuwa incompetent na ajira kwa watu hawa inakuwa ngumu sana.
 
Ajira ni ngumu sn. Wachina wanakuja kufanya biashara kwetu wanakuja na bidhaa zao kutoka china au wanatumiana na ndugu zao, haihitaji mtaji mkubwa sana, then sisi ndo tununue kutoka kwao tuuze tutaweza shindana kweli?
 
Wa Dodoma.Watanzania ni lazima tufahamu kwamba serikali hii haina mpango na kuwapa ajira vijana ndio maana mabalozi,wakuu wa mikoa na wilaya ni wastaafu,viongozi wanamiliki nafasi nyingi za ajira vijana watapata ajira wapi? mfumo wa elimu haumwandai kijana kujiajiri bali wa kuajiriwa.wasomi watabaki kuwa wakosoaji tu wa sera.
 
Habari za Asubuhi Wadau, Jumapili ya leo Jukwaa la Siasa na Uchumi litaangazania Idadi kubwa ya wahitimu kutoka Taasisi mbalimbali Nchini ambao wapo majumbani hawajui nini la kufanya. Tutajadili kusaka chimbuko la tatizo hili,

Je ni sera mbovu
Ni mitazamo isiyokuwa na malengo ya wahitimu
Je ni mfumo wa siasa za Nchi au tatizo limejikita wapi?

Wageni

Grayson Nyakarungu - Mwanaharakati / CDM
Patrobas Katambi - Mwanaharakati
Fortunatus Ntakabanyula - MBA SAUT
Shaaban Itutu - ADC
Dr.Kitila Mkumbo - UDSM

Karibuni kwa Mjadala


Yahya ninakufuatilia sana,ila naona mmesahu ishu ya pririty ambayo serikali inatoa kwa hawa vijana. tunasomeshwa lakn hawapriotise wanatupeleka wapi. je wanapata uchungu na gharama wanazotumia kusomesha watu ambao baadae wanakuwa unproductive?
 
Ajira ya Nchi hii ni ya kujana na ndiyo maana ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu wanakosa ajira coz wako wanaoajiriwa wkt hawana taaluma ya hicho wanachoajiriwa nacho na kuachwa wale wenye taaluma.
 
jamani waalim hawana tatizo ila tatizo ni serikali, vijana siyo goigoi ila seriakli inatuangusha hawatupi motisha katika yale tunayoyafanya.
 
Ahsanteni sana Wadau kwa michango yenu Asubuhi ya Leo. LakinI pia mniwie radhi kwa kiosk Mary baadhi kutokana na ufinyu wa muda
JF daima
Ahsanteni na wikiend njema
 
Back
Top Bottom