Mjadala kuhusu Mfumo wa Soko Huria na Ongezeko la Wahitimu Nchini - LIVE ON STAR TV

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za Asubuhi Wadau, Jumapili ya leo Jukwaa la Siasa na Uchumi litaangazania Idadi kubwa ya wahitimu kutoka Taasisi mbalimbali Nchini ambao wapo majumbani hawajui nini la kufanya. Tutajadili kusaka chimbuko la tatizo hili,

Je ni sera mbovu
Ni mitazamo isiyokuwa na malengo ya wahitimu
Je ni mfumo wa siasa za Nchi au tatizo limejikita wapi?

Wageni

Grayson Nyakarungu - Mwanaharakati / CDM
Patrobas Katambi - Mwanaharakati
Fortunatus Ntakabanyula - MBA SAUT
Shaaban Itutu - ADC
Dr.Kitila Mkumbo - UDSM

Karibuni kwa Mjadala
 
Tatizo hapa ni kuongozwa na watawala badala ya viongozi. Hawana dila wala ubunifu wa kuongeza ajira au hata kuweka mazingira ya vijana kujiajiri. Jambo la kufanya hapa ni kupata viongozi watakaoweza kutoa dira na mwelekeo na kuwafanya vijana kupata ajra kwa kuweka mazingira na miundombinu bora ili kujiajiri. Pia vyuo navyo vibadili mfumo wa ufundishaji ili wahtimu wawe na mwanga wa kujitengenezea ajira na wao kuajiri watz wenye elimu ya chini yao.
 
Hongera sana yahya kwa kuwa na ujasili wa kuitumia Jf kama kituo cha kupata maoni. Big up Startv..Bip up Yahya
 
Tatizo ni sera mbovu,kama kuna uchumi imara inakuwa rahis hata mtu kujiajiri.....serikal kwa nia na kwa makusudi imesababisha watanzania tuzid kuwa maskini,mtu anamalza chuo anakosa hata mtaji utakaowezesha kujiajiri.
 
Mimi naona tatizo ni serikali yenyewe sababu mfano unakuta inatrain watu ktk fan tofauti afu hijui itawapeleka wapi.Mfano watu wengi wanadahiliwa kusoma BCOM wengiii afu hawajui wanawapeleka wapi, SOCIOLOGY watu wengii afu baadaye wanaenda wapi?? je wanahitajika watu wengi kudahiliwa kiasi cha kuwa na idadi sawa na education. Hata watu walio kazini wanazidi tu kuendelea kuwepo na hawataki kuondoka, mimi naona pia watu kwenye nafasi ambavo hazina degree holder kwanini wasipelekwe hao mfano, watu wamesoma PSPA WAKAWE HATA MAKATIBU TARAFA,KATA badala yake huko kuna watu wanafanya hizo kazi hata upeo wao ni mdogo
 
sera mbovu na mfumo mbovu vyote vinachangia:

kwa mtazamo wa haraka Mawasiliano na ushirikiano kati ya vyuo vya elimu ya juu na serikali au wadau wa ajira ni mdogo mno, Kozi nyingi zinzofundishwa vyuoni pasipo kuzingatia matakwa na mahitaji kwenye soko la ajira.

Kila chuo kinapoibuka kinaibuka na kozi mpya bila kufanya utafiti wa kutosha katika soko la ajira kujua ni product gani inaitajika jambo ambalo linapelekea wahitimu wengi kubaki mitaani pasipo kuwa na ajira maalumu.

Hivyo basi ushirikiano ni muhimu kati ya Taasisi na Serikali kwenye kutengeneza ajira.
 
Tatizo ni sera mbovu,kama kuna uchumi imara inakuwa rahis hata mtu kujiajiri.....serikal kwa nia na kwa makusudi imesababisha watanzania tuzid kuwa maskini,mtu anamalza chuo anakosa hata mtaji utakaowezesha kujiajiri.

tatizo ni mfumo mbovu as well as viongozi
 
Yahya, Mke wangu amemaliza chuo kikuu mzumbe, amefaulu vizuri kwa kiwango cha upper second lakini hadi sasa hajapata ajira, leo mtu akimaliza chuo, kama hajuani na mtu kupata kazi ni almost impossible, na hii ni kwa sababu vyuo vinatoa graduate wengi kuliko soko la ajira linavyoweza kuzalisha nafasi za kazi, mke wangu anajaribu kujiajiri lakini mazingira ya kuanza shughuli binafsi ni magumu sana sana hapa tanzania.

uchumi wetu unafanya vizuri kwenye makaratasi tu, leo uchumi wetu hauwezi kuzalisha ajira, na hii inahusiana na sera mbovu za uchumi.

Siasa ya nchi ina uhusiano sana uchumi wa nchi, mfano mdogo, ukitizama vipindi vya uongozi
1985 hadi 1995 utaona wafanyabiashara walikua na hela lakini mfumuko wa bei ulifika 25%
1995 hadi 2005 mfumuko wa bei ulishuka hadi kufika digit moja.
2005 hadi 2012 mfumuko wa bei umerudi digit 2, inakadiriwa kuwa sasa ni 18% hadi 19.6%.

Unapokua na nchi ambayo haiwezi hata kuhakikisha umeme ambao reliable unazalishwa nchini ni ngumu kwa serikali kama hiyo kuwa na sera za kuongeza uzalishaji katika nchi. Serikali ambayo haiwezi hata kuja na sera nzuri za kodi ni ngumu serikali kama hiyo kujua matumizi yetu ya kodi tuyape kipaumbele kipi, matumizi ambayo yangeweza kuchochea uzalishaji katika nchi
 
tatizo wanasiasa hawasemi kuwa ajira sio serikalini2 lazima watu wajiajiri na wawe wabuni3u
 
Serikali irudishe viwanda vyake,bidhaa za nje zipigwe stop,yani kweli tumeshindwa kutengeneza tooth pick? Tumeshindwa kutengeneza kibiriti? Nyanya maembe yanatoka S.africa wkt sisi tuna lima hadi yanaoza!! Jukumu la ajira lipo mikononi mwa serikali,gov itengeneze apportunity za ajira.
 
Habari za Asubuhi Wadau, Jumapili ya leo Jukwaa la Siasa na Uchumi litaangazania Idadi kubwa ya wahitimu kutoka Taasisi mbalimbali Nchini ambao wapo majumbani hawajui nini la kufanya. Tutajadili kusaka chimbuko la tatizo hili,

Je ni sera mbovu
Ni mitazamo isiyokuwa na malengo ya wahitimu
Je ni mfumo wa siasa za Nchi au tatizo limejikita wapi?

Wageni

Grayson Nyakarungu - Mwanaharakati / CDM
Patrobas Katambi - Mwanaharakati
Fortunatus Ntakabanyula - MBA SAUT
Shaaban Itutu - ADC
Dr.Kitila Mkumbo - UDSM

Karibuni kwa Mjadala


Heshima mbele! Kuna tatizo la msingi katika mfumo wetu wa elimu. Sina tatizo na wingi wa vyuo kwanza havitoshi bado. Nina tatizo na kuongezeka kwa nyuo vikuu bila kuzingatia resources zilizopo katika vyuo husika. Vyuo vyetu sijui kama vitaweza kufundisha watu kufikiri wakati asilimia kubwa ya walimu huko wana Bachelors na Masters degrees? Hilo ni tatizo la msingi.

Pili, Tanzania kuwa na tatizo la ajira siyo stahili yake. We are at the midst of unutilized natural resources to absorb the massive growing rate of unemployed young people in this country. Dr. Kazungumzia ajira **** tatizo la Dunia na Tanzania klazima iwe na tatizo hili, siyo kweli? Marekani na Uingereza wametumia ardhi zao kupatia watu wao ajira, sisi tumefanya nini kutengeneza fulsa za ajira kupitia ardhi yetu? Dr Kitila Mkumbo amejustfy kwamba kiliomo ndo pekee kinaweza kutatua tatizo la ajira Tanzania. Kuna mifano mingi ambayo kimsingi wala hatuitaji kulia tatizo la ajira.

Nawasilisha.
 
Serikali inawajibika 100% kutengeneza mazingira ya watu kujiajiri kwenye sector binafsi. Imefanya nini kutengeneza fulsa za ajira binafsi katika kilimo, viwanda, utalii nk. Hasa mitaji.

tatizo wanasiasa hawasemi kuwa ajira sio serikalini2 lazima watu wajiajiri na wawe wabuni3u
 
vipi kuhusu fursa? zipo? maana vjana tunalaumiwa tunalalama badala ya kujishugulisha.
 
Njia rahisi ya kuongeza ajira ni kuchochea uzalishaji wa bidhaa, kama hata vijiti vya kutolea nyama kwenye meno (toothpick) zinatengenezwa china, tunategemea nini?

Kama nchi ina-import kila kitu kilichopo sokoni, sisi tunanunua hadi vitambaa vya kufuta jasho ni ngumu sana kama nch kuongeza ajira
 
Habari za Asubuhi Wadau, Jumapili ya leo Jukwaa la Siasa na Uchumi litaangazania Idadi kubwa ya wahitimu kutoka Taasisi mbalimbali Nchini ambao wapo majumbani hawajui nini la kufanya. Tutajadili kusaka chimbuko la tatizo hili,

Je ni sera mbovu
Ni mitazamo isiyokuwa na malengo ya wahitimu
Je ni mfumo wa siasa za Nchi au tatizo limejikita wapi?

Wageni

Grayson Nyakarungu - Mwanaharakati / CDM
Patrobas Katambi - Mwanaharakati
Fortunatus Ntakabanyula - MBA SAUT
Shaaban Itutu - ADC
Dr.Kitila Mkumbo - UDSM

Karibuni kwa Mjadala
Yahya mimi naona vijana hawaandaliwi katika hali ya kujitegemea zaidi bali wanaandaliwa kwamba wakimaliza tu vyuo wataajiriwa hasa na serikali, sasa wakikosa kuajiriwa na serikali au watu binafsi wanaduwaa wajue la kufanya kutokana na wigo wao mdogo wa ajira.
Mimi nafiriki wakati umefika kuwa mfumo wetu wa elimu ubadilike, uwaandae vijana kukabiliana na tatizo la ajira kwa kuwa wabunifu wa mambo mbalimbali badala ya kusubiri kuajiriwa
 
Hakuna injection au stimulation ya kukuza middle class kupitia SMEs ambazo mara nyingi ndio muajiri mkubwa kwa wenzetu walioendelea. Kazi za kutoa huduma ndo zingeanza kuboreshwa, kwa maana ya mifumo wa kuzitambua na urahisi wa kupata mitaji. Then tungeenda kwene kilimo na ukuzaji viwanda. Nafikiri tuko kwene right track kwa kujenga mabarabara na kuwafikia watu vijijini..tatizo letu lingine kubwa ni kuwa hakuna simultaneous efforts kuelekea roadmaps, mwingine utakuta anasema kuna upungufu wa wataalamu fulani - mwingine anasema hana ajira, mwingine anasema mazao yanamuozea hana pa kuyapeleka-wengine wanasema wana njaa au bei kubwa za mazao etc etc. hakuna coordination
 
for the case of Africa especially Tanzania our leaders decide to make us poor if we wil have a leader who wil look the interest of Tanzania we wil move one step ahead because most of the decision are based on normative economics so if we have leaders who lack political and human willingness probably we wil be moving backward.
Gays blv capital is not realy the problem becoz even if money is there,creative and qualified people are there and there is no political wilingnes what u think?
 
vyuo kuwa vingi sio tatizo tatizo ni kwamba wahitimu wake wanapohitimu wanapata kazi jibu ni kwamba kazi hazipo vijana wanabaki wanalandalanda tu mitaani kwa hiyo tatizo ni mfumo maana hakuna maandalizi mema kwa wahitimu ili waweze kupata ajira pindi wanapohitimu masomo yao.
 
Tatizo si mfumuko wa bei tu jamani..tatizo pia katika vyuo vyetu wahadhira hawana utaalam wakutosha katika kuhakikisha wanawapatia wanachuo elimu itakayowafanya wajiajiri wenyewe..Kuna chuo kimoja hapa Tz sitaki kukutaja...wahadhiri wengi wana degree ya kwanza wanawafundisha wanachuo wanaochukua degree hiyo hiyo ya kwanza..sasa wewe unategemea nini...??? Kupeana ajira pia kwa kujuana pia ni tatizo..unaweza ukamaliza chuo uko competent kweli kweli..unakwenda kwenye interview kumbe walishamwandaa mtu wao..Interview ni kiini macho tu!! Swalehe Sadiki Swea Arusha.
 
Back
Top Bottom