Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mbunge wa igunga,rostam aziz amesema dawa ya mchungaj mwasapile haitibu
source-jamboleo

mwambie amtafute mheshimiwa Mrema ampe full hbr kuhusu hiyo dawa ndo atajua km inatibu au la!!!!!!mrema anakwambia c unaona ht nimeanza kutakata...........
 
Nimeona baadhi ya viongozi wa dini na kisiasa wakimkashifu mchungaji masapile kwamba dawa yake haiponyi. Askofu Kakobe, Mchungaji Mwingira, Rostam Aziz ni baaadhi yao.

Mimi kwanza nashindwa kuwaelewa hawa wanaopinga kwamba dawa yake haiponyi.
1. KUNA MTU ALIEKULAZIMISHA KWENDA LOLIONDO?
2. UMELAZIMISHWA KUAMINI KWAMBA DAWA YAKE INAPONYA?

WEWE KAMA HUAMINI KAA KIMYA HUNA HAJA YA KUKASHIFU. Kwa akina Kakobe hainipi shida sana kwani wao naona Babu ni threat kwao. Ila nawashauri wawe tu wastaarabu.
 
mwambie amtafute mheshimiwa Mrema ampe full hbr kuhusu hiyo dawa ndo atajua km inatibu au la!!!!!!mrema anakwambia c unaona ht nimeanza kutakata...........

Aidha, mwambie hilo ni suala la imani zaidi sasa yeye kama hana imani ni yeye tu ambaye hatapona. Asiingile uhuru wa watanzania. Kama Serikali imetoa idhini hilo suala liendelee, ni nani huyo anayepingana na Serikali?? Kama mtu anapinga awe na hoja madhubuti, iliyofanyiwa utafiti na vielelezo tosha sio kuingiza siasa na chuki binafsi. Watu wote wale wanaoenda kwa Babu sio wajinga, lazima kuna kitu. WENGI WAPE, USIPOWAPA, WATACHUKUA WENYEWE.
 
imani ya rostam aziz ni pesa na wizi wa mali za nchi ....... hawezi pona
 
Low thinkers utawafahau tu. Chuki zao zipo kila mahali, Hayo ni mawazo yake Rostam, si kila kitu mnakipeleka katika siasa. Mnona tunaambiwa Lowassa nae kapata kikombe na ametoa magari na nauli za kuwapeleka wapiga kura wake kwa babu?

Zaidi ya yote, mbona Kadinari PENGO wa RC, MWINGIRA wa EPHATA, KAKOBE wa FGBF, Askofu MUSHI wa KANISA HALISI LA AFRIKA na Gazeti la ANNUR wote wamemponda Babu? Kakobeamemuita Babu kuwa ni wakala wa Shetani na Mwingira amemlaani Babu!

Si kila kitu ni siasa. Kama hamuwezi kufikiri deeply, hameni JF

Utahama wewe humu JF, usiejua mwelekeo wa dunia unaenda wapi? Very low thinker..

Kwa sisi tulioona ndugu zetu wamepona,siwezi kuona watanzania wakipotoshwa na vidampa kama wewe na bosi wako ra. Kama hamna la kuongea ni vema mngekaa kimya,kuliko kutoa ushuzi wenu haf hadharani sasa

Jambo usilolijua n kama usiku wa giza,kaeni kimya punguzeni viherehere! Zaidi ya hapo ndio tunapokuja kuona ni mambo ya maslahi zaidi, kama vile kakobe amekosa waumini! Sasa ra hospitali zake zimekosa wagonjwa,nk nk. Na wewe kidampa Kauza umetumwa kwa njaa zako, nk

Nyie madogo punguzeni Munkari. Mtakuja pasua screen zenu kwa kutokwa mapovu ya hasira badala ya kujibizana kwa hoja.....
 
Wakati anampeleka mbona hakuwaambia wananchi kama kweli ana nia nzuri!NDESAMBURO anawaambia na kuwasaidia wananchi wake yeye jee?
 
ndugu, labda utusaidie ni nini maana ya uhuru wa kutoa maoni? kwani huyo babu ni nani hadi watu wasimtolee maoni?

mitume na manabii walitolwa maoni, sembuse yeye?

acha kila mtu awe huru kutoa anaochoona ni sawa, ili mradi hawamkashifu wala kumkufuru Mungu

Glory to God
 
Huyu Jamaa na ufisadi wake hata kama akienda hakika hatapona....Hebu atupe ushahidi wa nani kaenda kwa Babu akapata kikombe na hajapona.
 
BlueBalaa (sijui ina maana Chelsea?) Naungana nawe kuwe kuwa hao wote ni wafa maji wameona kwao kumedoda sasa wanatafuta namna ya kumkandia Babu. Washindwe na walegee hakuna sababu ya kudharau jitihada au maono aliopewa Babu. Mpeni muda na tafuteni mengine ya kwenu sio kujihangaisha na ya Loliondo. Mmekwama kiaina.
 
Hili jitu kwanza kulijadili humu nasikia kichefuchefu.tangu lini jizi likawa na imani kama hiyo bila kutubu na kuiamini injili.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Hawa wachungaji wengine kama Kakobe, Mwingira na wengineo wanaona kuwa sababu kubwa ya kupata idadi kubwa ya waumini walionao ni kutokana na hao waumini kutafuta tiba mbadala (neno la Mungu) kuwaponya maradhi yao; hivyo kutokana na babu kutibu maradhi kwa njia ambayo ni rahisi bila kumlazimisha mtu kuokoka na dawa kufanya kazi kwa muda mfupi na kutolewa ushuhuda wa kweli ambao ni tofauti na wa kwao wa kupanga, wanaona inakula kwao.

Makelele yote wanayotoa ni katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhodhi hisa ya soko lao (Market Share) katika suala zima la makanisa ya Kipentekoste. Kuna madhara makubwa wameyaona kibiashara zaidi. Kwani kama jamaa zao wakienda kupata tiba halafu wakapona kutakuwa hamna haja ya kuendelea kwenda kwenye makanisa yao. Kwani hata babu anawaambia kama umepona katoe sadaka kwenye nyumba yako ya ibada. Hii ni dalili kuwa wale waumini watarudi kwenye imani zao za awali kabla ya kwenda kwenye hayo makanisa ya Manabii.

Waumini watakuwa wanawashitukia hawa manabii, kwani kwa kipindi choote walichokuwa wakihudhuria ibada kwenye hayo makanisa ya Manabii kwa matumaini ya kupona lakini lah na kwa kikombe cha uzima wamepona... Wengi watawakimbia na hivyo wao (Manabii) kukosa "market share".

Kwa upande mwingine babu ameongeza changamoto kwenye nyanja ya tiba. Hata wale waliokuwa wakifanyia utafiti baadhi ya magonjwa wanapigwa na butwaa ni vipi hiki kikombe kinatibu. Lakini wanasahau kuwa kila jambo wanalofikiri kuwa ni njia muafaka ya kupambana na magonjwa kuwa ni kutokana na elimu waliyoipata kwa mapokeo. Ila babu amekuja na njia ambayo ni mapinduzi kwenye nyanja ya Tiba.

Mtu unapotoa maoni na kusema kuwa kikombe cha uzima kithibitishwe kwa njia za kisayansi naomba nitoe angalizo. Hizo njia za kisayansi ni zipi? Maabara ? Kwani hizo njia zilitokea wapi? Hayo yalikuwa ni mawazo ya watu katika kipindi chao ambapo nao walionekana kama wanafanya miujiza. Hivyo kwa hili la babu, mimi nina imani kabisa kuwa tunaishi katika historia. Baada ya kipindi, muda, wakati fulani tutapata jibu ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Wahenga walisema "Muda utasema".

Tumwache babu aendelee kutoa tiba. Tujaribu kufanya tafiti tuweze kujua ni nini hasa kinachojiri. Tusiongee tu kwa kuketi kwenye computer zetu na kutoa maoni bila kufanya tafiti na kupata takwimu sahihi.

Nawasilisha.
 
Huyu Jamaa na ufisadi wake hata kama akienda hakika hatapona....Hebu atupe ushahidi wa nani kaenda kwa Babu akapata kikombe na hajapona.

anadai mjomba wake alikunywa hajapona
'ndugu zangu wananch wa igunga,mimi mjomba wangu hasan mnamfaham karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nying wa kisukari.ameshakunywa dawa hyo lakin mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa,hyo dawa inaponyesha nini?'Mwananch ndo limemnukuu,uk 3
 
Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo

Tuesday, 15 March 2011
Shija Felician, Igunga


WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.


Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... "Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?"


Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.


Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.


Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.


Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.


Chanzo: Mwananchi - 16/3/2011
 
Sasa mbona swahiba wake amekwenda kupata kikombe na kuhamasisha wapiga kura wake kwenda kupata kikombe. Au hawakujadiliana kabla?
 
hao ndugu zake na yeye mwenyewe wakapungwe mashetani kwanza then waende kwa babu. sababu nyingine ni laana toka kwa mungu mmetuibia saaaana nyie skina rostam
 
Mrema kapigwa na kisukari zaidi ya miaka 30 na sasa uso wake unang'aa, jana TBC1 katoa ushuhuda, Sasa huyu rostam na ndugu zake hawana imani na hawamjui Mungu ndio maana hawawezi kupona kwa babu, ukiwa na imani utapona kama wengine waliopona.
 
Back
Top Bottom