Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Asante sana Mwelewa.Pia kuna baadhi ya ndugu zangu wameenda huko.Watu wengi wanasema kuwa wamepona.
 
Kwa muda sasa habari zimetapakaa kuhusu tiba ya magonjwa sugu inayopatikana huko Loliondo wilaya ya Ngorongoro. Dawa hiyo inasemekana ni ya kunywa na unalipa sh mia tano tu. Anayetibu hataki chochote zaidi.

Wanasiasa mbalimbali wanaenda huko kutibiwa. Tiba hiyo haina TBS wala TFDA hawaijui.

Ikatokea ikawekwa tone la sumu, tutakuwa na janga la taifa. Namkumbuka mtu aliyeitwa Kibwetere.

Sina tatizo na suala kwamba imani yako inaponya ila in the unlikely event something goes wrong as it usually does at least I said.

Kama tungekuwa na viongozi na si wanasiasa wangekuwa wametoa tamko na maelekezo. Tatizo letu nchi imejaa wanasiasa. Na wao wanaenda huko kutibiwa. Kama kuna aliyepona atujulishe.

Jana kuna mgombea Ubunge mmoja ameniambia kuna daktari amemueleza kwamba kuna wagonjwa wawili wa HIV wameenda kunywa hiyo dawa ila nao its worse!
 
kweli wewe mpiga promo namba moja.

KAMA WATAKA NA WEWE KWANINI USIENDE KIMYA KIMYA.
 
CRrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaaap
 
Kama kweli huyu Mganga wa Loliondo anatibu tena kwa gharama naffu hivyo, waache watu wajaribu bahati zao, maana gharama za matibabu katika hospitali za Umma si mnazifahamu? HAZINA DAWA.
 
Kaka wa arusha nina shida kubwa ya kisukari. Nitafikaje kwa huyo mganga nikifika arusha?. Naomba msaada nina shida kubwa ya kisukari iko juu 32, nataka nimwone huyo mzee na mtumishi wa mungu

Kama huwezi kufika hata hapa JF waweza pata msaada mimi hapa nipo nahitaji watu wachache kama ww imani ikijengeka nitaanzisha jukwaa la matibau hapa hapa ila sharti uje utoe ushuhuda...ok for you tiba ni hivi kaa leo jioni chunguza mambo yako tangu ulipo pata sukari je mwanzo kitu gani kilikuumiza sana moyo wako...then samehe wote walio kukosea, jisamehe mwenyewe kubali kuwa kuna mambo huyajui sawa sawa lakini yeye aliyekuumba ajua vyote baada ya hapo omba msamahaa kwa Mungu kwa yote uliyokosea kubali kuwa utakuwa tayari kuongozwa na roho mtakatifu, omba uvuvio wa roho mtakatifu then after all jiambie mwenyewe kwa sauti kwamba una mkiri Yesu kuwa bwana na mwokozi wako. Amini imesha kuwa hivyo huta feel the same day but as you proceed itakuwa for realy inside you!

Hatua ya pili sema maneno haya kwakupigwa kwake Yesu mimi nimepona sukari huna mamlaka juu ya mwili wangu tangu sasa nakuamuru katika Jina la Yesu toka ndani ya mwili wangu kwani mwili wangu ni hekalu la roho mtakatifu na siyo nyumba ya ugonjwa wa sukari...Say it seven times...You are healed in Jesus name! Nenda kapime kula chakula chako unachokipenda monitor your level of sugar....Then come back and confess for others also to benefit from my service okay!
 
Kwa wale waliopo Arusha kuna magari yanatoka stand adi hapo kwa mchungaji. Nauli ni elfu sitini kwenda na kurudi. ANGALIZO: kwa wale wenye magari binafsi barabara ni mbaya sana. Gari za kufaa ni landcruse,landrover na yote ya aina hiyo. Ukiwa Arusha city watu wanaonda ni wengi so njia ya kwenda utafahamu.

isije ikawa dill na wenye vyommbo vya usafiri maana nauli utafikiri unatoka mza kwenda dar
 
Inasemekana hata mkwere na makamu wa raisi nao wamepata matibabu ya huyo mzee
 
sitaki kuwa wa mwisho kuamini kuwa daw ya ukimwi imepatikana. Mwaka 1997 alitokea mama mmoja huko bukoba kwa madai hayo hayo ya kutibu ukimwi walisema alikufa kwa siku 3 akafufuka. Akasema kaoteshwa na mungu dawa ya ukimwi. Yeye alikuwa anatumia majani matatu tofauti unapanguswa mdomoni mara tatu afu unaambiwa kapime na hata ukimgonga muathirika hupati ngoma. Ila mpaka sasa kuna jamaa zangu nawafaham wameishatangulia mbele ya haki kwa kwa ugonjwa huu huu. Na walilambishwa hayo majani. Walihudhuria watu kibao hadi vingozi wa serikali wakati huo. Umaarufu hauji hivi hivi jamani.
 
Hii habr njema! Serikal hawajalisikia hili wamuwezeshe kuwasaidia watanzania au wwanajifanya hawajui km kawaida yao coz wao wanaenda tibiwa ughaibuni!
 
Hii habari nimeipata leo kwa mtu ambaye mama ake mzazi alienda last week na alikuwa anasumbuliwa na canser na alikuwa akakatwe mguu kutokana na kidonda alichokuwa nacho kwa muda mrefu bila kupona,na kwa mujibu wa huyo jamaa anasema mama ake huyo kwa sasa kidonda kinakauka kabisa na yupo fit kabisa,maumivu yote anasema yameisha kabisa.......
 
Jumapili alfajiri yaliondoka magari zaidi ya 10 kupeleka wahitaji wa tiba hiyo!!!!
Kuna jamaa napiga nae mzigo hapa ofisi anasema yeye alimpeleka kid wake na amepona kabisa!!!

Vipi kama serikali ikaingilia kati.
Kwa kupitia wizara ya Afya wamtembelee na waingie nae contract. Basi asafirishwe aje aweke makao yake Muhimbili. kwa kuanzia Wamkabidhi Wodi ya Mwaisela.
Atakuwa anafanya pia round kule Ocean Road kwenye kansa.
Nadhani utakuwa mkataba mzuri kuliko yote ktk historia ya Tanzania huru!

Just attempting to think.
 
Vipi kama serikali ikaingilia kati.
Kwa kupitia wizara ya Afya wamtembelee na waingie nae contract. Basi asafirishwe aje aweke makao yake Muhimbili. kwa kuanzia Wamkabidhi Wodi ya Mwaisela.
Atakuwa anafanya pia round kule Ocean Road kwenye kansa.
Nadhani utakuwa mkataba mzuri kuliko yote ktk historia ya Tanzania huru!

Just attempting to think.

haiwezekani kuhama....alipoelekezwa na roho ni huko Loliondo...usonjoni......hata sisi watu wa Arusha tulipenda sana asogee sogee hata hapo Mto wa Mbu....kwenda Loliondo si ishu ndogo...lakini habari ndio hiyo....lipa elfu 70 za usafiri, dawa sh 500....hili ni fumbo la imani....Tafakari
 
Sasa tunaipata vipi sisi tuliombali jamani tusaidieni kwabla hatujaumbuliwa na magonjwa,
Saidia baba!
 
Sasa tunaipata vipi sisi tuliombali jamani tusaidieni kwabla hatujaumbuliwa na magonjwa,
Saidia baba!

ndugu yangu Shupaza...hii dawa siwezi kukuletea mimi au mtu yoyote yule....ni lazima akupe yeye mwenyewe kwa mkono wake....hata mfanyakazi wake akikupa haifanyi kazi, hata mkewe...lazima awe yeye....so hapo kwenda Loliondo kutakuwa kunakuhusu
 
184898_10150127998979345_817319344_6216663_1540231_n.jpg
 
Back
Top Bottom