Mjadala: Enzi za Kikwete ndoa zilikua shida, ushapata kufikiria enzi za Magufuli itakuwaje?

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,700
Poleni sana akina Dada maana nyie ndo special engines za ndoa ukweli usiopingika. Kwenye theories za ndoa kuna uhusiano mkubwa sana wa uchumi wa muoaji(husband). Uchumi huu wa scarcity kali sana waoaji tuna changamoto nyingi kiasi kwamba priority ya ndoa inawekwa mwisho huko, jinsi mlivyotuzoesha bills zote lazima tulipe mwenyewe,kodi ,school fees za watoto,shopping wenyewe na matoleo yote ya simu wenyewe.

Safari hii option labda tuliyokua nayo vijana wa mjini ni kuzaa tu na nyie ,hata na wewe kama unaona umri unasonga na ndoa bado nakushauri usikose yote hata mtoto? na wewe brother hata mambo yako yatapokaa sawa usisite kumuoa single mother sio yeye alisababisha.

Na hata walio kwenye ndoa poleni sana hiki ndo kipindi cha kuthibitisha kiapo chako kama kilikua genuine ,wake hawatacompensate kwa Kucheat na wanaume hawatakimbia ndoa zao.

Yani hizi enzi busara isipotumika kuna uwezekano wa kutokea pattern za ajabu sana za relationship na marriage kama uchumba sugu, single fathers and mothers, marriage without children, one night stands, watoto wa mtaani. Matokeo yake kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kijacho kuwa katili sana kwa kukosa malezi ya wazazi wawili ( spiritual point of view) kwani njia PEKEE ya kulea watoto ni familia ambayo ni natural institution imeandikwa kwenye dini na ethics pia.

Mnakaribishwa katika mjadala wakuu
 
Sasa unaoa mwanamke wa kumpa kila kitu, jilaumu mwenyewe. Maisha yamebadilika.
 
Back
Top Bottom