Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,101
Ni hv nimeamka zangu mapema nikasema Leo Nina buku 6 acha nikanunue nyama nipike nile gheto nipumzike kula ugali na Mayai!basi wakati nimefika tu sokoni nakutana na koloni langu(Japo nilishampa Uhuru kitambo)nikampa hai kwa mbali na kumpotezea kimtindo! Kumbe ananifuatilia kwa nyuma bila ya Mimi kujua kabla ya kuanza kununua nyama nikaona ninunue nyanya kwanza ili nikampige sound muuza nyama apunguze bei sasa wakati naanza kuchukua nyanya akafika yule koloni akaanza na yeye kuchukua nyanya,vitunguu,karoti na vitu vingine vingine vidogo na kumwambia muuzaji kwamba nitalipa mimi!nikataka kumwambia mimi sina hela akaniambia wakati ule wakati nadate naye sikuwahi kumpa hata shilingi!mzee mzima nikabaki nimeduwaa tu mara demu huyo akaondoka zake!kupiga mahesabu amechukua vitu vya buku tatu!ndio hapo nikahairisha mpango wa kununua nyama nikaamua tu nilipe deni la watu sasa hv nipo gheto nakula ugali na kachumbari! Wanawake mnavyofanya sio fair
