Mizinga 6 ya nyuki kutoka Tabora inauzwa

Biashara2000

JF-Expert Member
Nov 9, 2013
636
540
Mizinga ya nyuki inauzwa kwa bei nzuri. Mzinga tsh 90000.

Kwa mawasiliano 0758 308193 ipo Dar lakini unaweza ukapangwa utaratibu ikasafirishwa poote ulipo nchini.

IMG_20200129_083516.jpg

IMG_20200129_083401.jpg
 
Mzinga 1unazaliaha asali kiasi gani na kwa mda gani

Katika kila mzinga kuna fremu 10 na kila fremu inakupa kilo 1 ya asali hapa zinapimwaga kwa kilo hivyo kwa mzinga unaweza pata angalau kilo 10 na hii ni baada ya miezi 3. kila kilo huuzwa tsh 12000 hivyo mzinga unakupa kipato cha tsh 120,000 kwa kipindi hicho. Sasa hapo itategemea una mizinga mingapi ili upate zaidi

Kwa mwaka unavuna mara 4

Hivyo kwa mzinga kwa mwaka angalau una tsh 4,800,000
 
Katika kila mzinga kuna fremu 10 na kila fremu inakupa kilo 1 ya asali hapa zinapimwaga kwa kilo hivyo kwa mzinga unaweza pata angalau kilo 100 na hii ni baada ya miezi 3. kila kilo huuzwa tsh 12000 hivyo mzinga unakupa kipato cha tsh 1,200,000 kwa kipindi hicho. Sasa hapo itategemea una mizinga mingapi ili upate zaidi

Kwa mwaka unavuna mara 4
1.2 M X 4

4,800,000 X 10

48,000,000!!

Hakuna masikini dumiani ni ujinga wetu!!!

Yaana Milioni 48 kwa mtaji wa laki 9 ndani ya mwaka mmoja?;??
 
Unajua mtu ukieleza hizi takwimu kuna watu wanadhani ni story au nn. Kila mtu afanye reseach yake mwenyewe kwa wafugaji nk, Tembeleeni wafugaji wa kisasa mjionee wenyewe. Sie wengine watengeneza mizinga lkn pitieni wakulima mjionee watu wanavyotajirika msidhani hizi figures za kupika
 
Katika kila mzinga kuna fremu 10 na kila fremu inakupa kilo 1 ya asali hapa zinapimwaga kwa kilo hivyo kwa mzinga unaweza pata angalau kilo 10 na hii ni baada ya miezi 3. kila kilo huuzwa tsh 12000 hivyo mzinga unakupa kipato cha tsh 120,000 kwa kipindi hicho. Sasa hapo itategemea una mizinga mingapi ili upate zaidi

Kwa mwaka unavuna mara 4

Hivyo kwa mzinga kwa mwaka angalau una tsh 4,800,000
mkuu kama ni simpo kama hivo nenda kafuge wewe upate hizo njuruuu mkuu

cc mng'ato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hili ndilo tarizo letu watz ndio maana hatuendelei. Sasa sijui ni education system yetu au ni malezi, sielewi. Mindset hii ndio inarudisha nyuma sisi watz.

Mtu anadhani kila mtu anaweza fanya kila kitu ndo mindset hii inaleta watu wanaodhani wanajua kila kitu. Ukisema unaumwa kichwa utasikia hiyo maleria, mwingine aah hiyo typhoid yaani hakuna mtu aseme unajua hatujui labda uende hospitali upime uambiwe ni nini. Kuumwa kichwa ni dalili ya magonjwa tofauti tofauti.

Nimeeleza huo mfano wa ugonjwa kuelezea km mfano ktk comment yako. Mi ni fundi naunda mizinga, ndio kazi yangu, wengine watafuga, wengine watakuwa kazi y ni kuuza asali, wengone watakuwa kutumia. Hatuwezi wote fanya kila kitu

Nadhani utakuwa umepata chochote.

Stick with what you know
 
Katika kila mzinga kuna fremu 10 na kila fremu inakupa kilo 1 ya asali hapa zinapimwaga kwa kilo hivyo kwa mzinga unaweza pata angalau kilo 10 na hii ni baada ya miezi 3. kila kilo huuzwa tsh 12000 hivyo mzinga unakupa kipato cha tsh 120,000 kwa kipindi hicho. Sasa hapo itategemea una mizinga mingapi ili upate zaidi

Kwa mwaka unavuna mara 4

Hivyo kwa mzinga kwa mwaka angalau una tsh 4,800,000

Mtu akikupa huu mchanganuo, unatamani mara moja kufanya hiyo shughuli. Lakini hali ahlisi sivyo, muhuzaji akisha kupa mzigo, basi yeye anaweka chake mfukoni, sasa kazi inakuja kwako kuwaka hiyo mizinga. Probabilities ni ndogo sana kupata alicho kuambia, kwani yawezekana:

1: Nyuki wasiingie kwenye hiyo mizinga kwa kwakati

2: Kiwango cha asali utakayo pata kwenye huo mzinga kikawa chini ya alichokisema

3: Usivune hiyo asali mara 4 kwa mwaka kama alivyosema

4: Soko la asali lisiwe rafiki kama alivyo sema.

NB:
Ni wazo zuri kuwa mradi wa kuvuga nyuki, lakini mtu hasifanye kwa mihemuko ya kupata pesa baada kushawishiwa na wafanya biashara.
 
Namaingo,DECI,mkojo wa simbilisi,Mayai ya kware,matikitiki maji yanalipa.,.............!
Ha haaa
Hapo kimoja tu ndio kinalipa kama utajua kulima wakati sahihi na kilimo cha maarifa.
Ni matikiti tu tena ukiwa makini mno.
 
Na hili ndilo tarizo letu watz ndio maana hatuendelei. Sasa sijui ni education system yetu au ni malezi, sielewi. Mindset hii ndio inarudisha nyuma sisi watz.

Mtu anadhani kila mtu anaweza fanya kila kitu ndo mindset hii inaleta watu wanaodhani wanajua kila kitu. Ukisema unaumwa kichwa utasikia hiyo maleria, mwingine aah hiyo typhoid yaani hakuna mtu aseme unajua hatujui labda uende hospitali upime uambiwe ni nini. Kuumwa kichwa ni dalili ya magonjwa tofauti tofauti.

Nimeeleza huo mfano wa ugonjwa kuelezea km mfano ktk comment yako. Mi ni fundi naunda mizinga, ndio kazi yangu, wengine watafuga, wengine watakuwa kazi y ni kuuza asali, wengone watakuwa kutumia. Hatuwezi wote fanya kila kitu

Nadhani utakuwa umepata chochote.

Stick with what you know
mkuu wewe kama fundi kwanini unaanza kutoa hesabu za fedha kama mtaalamu wa ufugaji?

nijibu hilo swali ndo nkwambie kwanini nili comment vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akikupa huu mchanganuo, unatamani mara moja kufanya hiyo shughuli. Lakini hali ahlisi sivyo, muhuzaji akisha kupa mzigo, basi yeye anaweka chake mfukoni, sasa kazi inakuja kwako kuwaka hiyo mizinga. Probabilities ni ndogo sana kupata alicho kuambia, kwani yawezekana:

1: Nyuki wasiingie kwenye hiyo mizinga kwa kwakati

2: Kiwango cha asali utakayo pata kwenye huo mzinga kikawa chini ya alichokisema

3: Usivune hiyo asali mara 4 kwa mwaka kama alivyosema

4: Soko la asali lisiwe rafiki kama alivyo sema.

NB:
Ni wazo zuri kuwa mradi wa kuvuga nyuki, lakini mtu hasifanye kwa mihemuko ya kupata pesa baada kushawishiwa na wafanya biashara.
Ni kweli kabisa ulichosema.
Hapo namba 1 nyuki wanaweza kupandikizwa kwenye mizinga sema ni usumbufu na gharama.
Namba 4 soko la asali ni kubwa hasa ukiweza kuzalisha kwa wingi.
Namba 2 & 3 umepatia sana maana hayo mawili hutegemea na mahali ulipoenda kuweka mizinga kama kuna chakula cha nyuki na maji karibu mwaka mzima.
Pia hutegemea na jinsi utakvyotunza na kufuatilia wadudu adui wa nyuki na binadamu wezi wasihujumu mavuno yako.

Ingekuwa unatega mizinga na nyuki wanaingia na kuzalisha asali kirahisi namna hiyo basi huyu mleta hii habari asinge hangaika na shuruba za kutengeneza mizinga na kutafuta wateja badala ya kuweka ya kwake na kwenda kulala nyumbani huku nyuki wakikutengenezea mamilioni.

My take: Hakuna biashara rahisi, hakuna pesa rahisi lazima ufanye kazi hasa.
 
Unajua mtu ukieleza hizi takwimu kuna watu wanadhani ni story au nn. Kila mtu afanye reseach yake mwenyewe kwa wafugaji nk, Tembeleeni wafugaji wa kisasa mjionee wenyewe. Sie wengine watengeneza mizinga lkn pitieni wakulima mjionee watu wanavyotajirika msidhani hizi figures za kupika

Cheating
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom