Mizimu Kama Chanzo Cha Matatizo!

Mizimu Kama Chanzo Cha Matatizo!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,939
“MIZIMU KAMA CHANZO CHA MATATIZO”

Duniani yapo matatizo ya aina mbalimbali, matatizo hayo yote yana namna ya kuyaondoa. Unapokuwa umekosea namna ya kuliondoa tatizo lililokupata unaweza ukajikuta unakuwa sehemu ya tatizo hilo. Unatakiwa kufahamu kwamba kila tatizo linalotokea lina chanzo chake, ukifanikiwa kufahamu chanzo cha tatizo basi unakua umefanikiwa kuliondoa tatizo.

2wafalume 2:19-

Inawezekana unatatizo lakini hajaamua kufahamu chanzo chake umekuwa akihangaika na tatizo hilo muda mrefu bila kulitatua.

Tumeona vyanzo vya matatizo kwenye maisha ya watu
i. UCHAWI – Uchawi umekuwa chanzo cha matatizo ya watu wengi.
Kumbukumbu la torati 14:10-11

ii. ROHO YA KUKATALIWA
Isaya 53:
Roho ya kukubalika ikiwa ndani ya mtu anaweza kupata kitu lakini ukiwa na roho ya kukataliwa unakua na mazingira magumu

iii. MAPEPO AU MASHETANI

iv. MIZIMU YA UKOO NA MATAMBIKO
Kwa kawaida kila ukoo una taratibu zake, kuna mambo mengi yanafanyika kwenye ukoo lakini ni ya kishetani

2Wakorintho 6:14

Kwa mfano tunamuona Gidioni kwenye Biblia, Gidioni aliletwa duniani kwa ajili ya makusudi ya Mungu lakini baba yake alikuwa mchawi. mizimu ya baba yake ikawaimemkamata Gidioni ili asiende alikotakiwa kwenda.

Mungu hakumwambia Gidioni ajitenge na ukoo au familia yake bali alimwambia abomoe madhabahu ya baba yake.

1Petro 1:18
Kuna tamaduni ambazo watu wamezipokea na hawajui maana zake, mfano mtu anachaguliwa kuwa kiongozi wa ukoo lakini hajui maana yake, kumbe amekabidhiwa mizimu ya familia.

Mila za ukoo na matambiko.

Mitambiko ya ukoo ni makubaliano ambayo watu wanaingia kwa ajili ya ukoo, Mungu hakumwambia Gidioni ajitenge na ukoo au familia yake bali alimwambia abomoe madhabahu ya baba yake ili awe huru yeye na watu wake.

Mizimu ni nini?

Kimsingi mizimu ni majini au mapepo ambayo yanatawala familia. Kuna baadhi ya familia mizimu inaheshimiwa sana. Na matambiko yote yanayofanyika kwenye ukoo ni ibada za mizimu/wafu.

Mizimu hii inaweza kuvaa sura ya mtu yakamtokea mtu kwa uhalisia wa binadamu flani hata akatenda mambo kama ya mtu yule. (Mtu anakufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu) mtu aliyekufa hawezi kutokea duniani tena bali wanaotokea ni mashetani aina ya mizimu. Maana mtu akifa tu hukumu yake inaanza.

Tabia za mizimu.

Mizimu ni roho ambazo zinachukua uhusika wa watu waliokufa na huwa zina sifa ya kupenda kuabudiwa na kutambikiwa kama Mungu, mizimu inapenda kuheshimiwa.

Roho hizi zikiabudiwa sana zinaingia kufanya mikataba na watu. Kabla ya injili kuenea watu walikua na imani zao na walikua na miungu wao ambayo walikuwa wanaiomba na kutoa sadaka kwayo. Wanaiomba mvua na mvua inanyesha, kwahiyo wokovu umekuja juzi miaka mia iliyopita kwahiyo bado kuna muunganiko wa wewe na mizimu ile ndiomaana tunajifunza ili ujitenge nayo na kuacha kabisa kujiungamanisha na taratibu zao kwa jina la Yesu.

Kama Mungu alivyo na utaratibu wake wa madaraka na shetani naye amejiendeza kwa utaratibu kama huo, kama ni maafaa kuna mashetani wanahusika na idara hiyo.

Utaona Isaka alipoona umri wake umeenda sana akamwita mwanae Esau akamwambia nenda kalete mawindo nile nikubariki, na ndugu yake alipoleta kabla Esau hajarudi baba yake akamwambia mbona umewahi? Akajibu Mungu wangu amefanikisha.

Kumbe kuna mambo lazima Mungu akufanikishe ndio upate, kuna utajiri au Baraka ambazo Mungu ndiye anafanikisha na Baraka hizi huwa hazina majuto. Chochote kitokacho kwa Mungu ukipata umepata maana Mungu ndiye anayefanikisha.

Petro alikuwa mvuvi siku moja alikwenda kuvua usiku kucha hakupata samaki lakini Yesu alipokuja akataka kumuonesha kuwa yeye anaweza kufanikisha hata kwenye uvuvi, Yesu anaweza kumfanikisha mtu kila mahali iwe ni kwenye biashara, iwe ni kwenye masomo Yesu anafanikisha, haangalii umesoma au hujasoma Yesu ukitaka akufanikishe anakufanikisha kweli kweli.

Petro kwa taratibu za uvuvi alikuwa haamini kuwa mchana anaweza kupata samaki lakini Yesu akamwambia shusha nyavu zako kilindini, Petro akasema kwa neno lako nitashusha, aliposhusha nyavu zilijaa mpaka akawaita na marafiki zake wamsaidie kuvua. Yesu akikubariki anakubariki pamoja na marafiki zako.

Mizimu au mapepo ni shetani yule yule anayeabudiwa kwenye ukoo au makabila.

Shetani anaitwa (Mwizi).

Yohana 10:10

Shetani na mungu wa dunia hii.

2 Wakorintho 4:4

Kutoka 1:8

Siku zote anayekutega ana hofu juu yako, anaona una nguvu kuliko yeye. Lakini saa yako imeandaliwa na Bwana ili utoke kwenye mtego waliokutega kwa jina la Yesu. Kila mtu ana saa yake Mungu awemuwekea aanze kazi. Unapokuwa umefanikiwa sio kwamba wewe umewahi sana bali ilikuwa ni saa yako.

Wagalatia 4:4

Saa yako ikifika hakuna anayeweza kusimama mbele yako kukuziua. Jambo la Kimungu likizuiliwa ndio linazidi kukua zaidi kuenda kwenye utimilifu.

UKWELI KUHUSU MIZIMU
Mizimu ni Malaika walioasi kutoka Mbinguni.

Ufunuo wa Yohana 12:4

Mizimu ni wapelelezi wa familia – kazi yao ni kupeleleza mambo yote ya familia ili waimiliki.

Mizimu ni wasimamizi wanaotoa taarifa.

Mizimu hufanya kazi kupitia wafu – ndio maana Mungu amekataza ibada za wafu (ibada wa wafu ni ibada ya kishetani) baada ya kufa ni hukumu. Arobaini ni ibada ya wafu, kukata nywele kwenye msiba ni ibada ya wafu, kusafisha makaburi ni ibada ya wafu usifanye hivyo mtu wa Mungu maana umeshapita mautini na kuingia uzimani.

Kama kuna mtu unataka kumuombea aokoke muombee aokoke kabla hajafa, akishakufa sio mwenzako tena hata ukilia usiku kucha. Mizimu inafanya kazi kwa kupitia waganga wa kienyeji.

Mizimu inaweza kutunza taarifa za ukoo au kabila.

Mathayo 18:10

Kila mtu ana malaika wake, ambaye anatoa taarifa zake kwa Mungu.
Malaika ni wasimamizi, kila mtu ana msimamizi wake ambaye anaitwa malaika.

Matendo ya Mitume 12:15

2Timotheo 2:16

Kila mtu ana malaika wake.

2Peto 2:27

Ndio maana baadhi ya mila na makabila mtoto akizaliwa wanamuingiza kwenye ukoo, unakuta wanachukua kitovu, nywele na kucha na baadae mtoto anapewa na jina la babu au bibi wa ukoo(mambo ya huyo babu/bibi yanaambatana naye bila wao kujua kama alikua tasa mtoto naye anakua tasa, na yule malaika wa Mbinguni anakua hawezi kuanya kazi sababu mtoto amemilikishwa kwenye ukoo).

Mtoto anapokabizidhiwa kwenye ukoo anapewa na mzimu wa kumlinda yule malaika wa Mbinguni anakuwa hana nguvu juu yake. Unakuta mtoto anapewa jina la ukoo mara nyingi sio kwa ajili ya upendo bali ni kwa ajili ya mizimu. Watu wengi wanafanya hivyo bila kujua.

Kwenye utaratibu wa kitaalamu, unaweza kupima nguo,au damu au nywele ukajua DNA(vinasaba) vya mtu. Sasa kuna watu wengine kuna vitu vyao iwe ni nguo au nywele au damu vipo kwa mganga wa kienyeji na ndio chanzo cha matatizo yao lakini hawajui japo wameokoka wanampenda Yesu hawafanikiwi kwasababu hiyo, mpaka wabomoe madhabahu zilizowashikilia kwenye koo na familia.

Ndio maana kuna baadhi ya vitu havikubaliki kwenye ukoo, mfano kula nyama, kula mayai, kunywa maziwa, kujenga nyumba ya bati, mizimu yao haikubali mtu afanye mambo kama hayo. Kuna mizimu mingine inasimamia dini, unakuta mwanadini lakini ni mchawi wa kutupa, anatumia dini yake kujificha aonekane mtakatifu.

Dini ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu bali wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu.

Matambiko ni utaratibu wa utekelezaji wa mizimu. Ndio maana sasa mizimu inakuwa inasimamia biashara ya mtu kwa sababu kuna mikataba ya damu.

Mikataba – ni makubaliano au mapatano
Mwanzo 21:27
1Wafalme 15:19
Mizimu inayokumiliki na kukusimamia haiwezi kuondoka kwasababu kuna mikataba (mpaka utakapovunja mkataba nayo).

2Wafame 11:17

MASHARTI YA MIKATABA
Yeremia 44:17 -18 -19 & 25

Kuna watu wameingia kwenye ufalme wa Mungu lakini hawawezi kutofanikiwa kwa sababu kuna mbambo hawajayaachia. Kama kuna mambo ambayo ya kichawi ulifanya na unahisi ndio yamekushikilia unashindwa kuendelea mbele tafuta mtumishi wa Mungu mweleze upate msaada, ukikaa kimya utaangamia.

Madhabahu ni daraja linalounganisha ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa Mwili.

- Kuna mambo yanafanywa kwenye madhabahu ili kuunganisha viumbe wa Rohoni na viumbe wa Mwilini. Cha kufanya ni kuzivunja madhabahu inayokuunganisha nao.
Bomoa madhabahu zilizokushikilia kwa jina la Yesu na utakua huru. Amen

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Vyakula vya kula. Ugali ni chakula,wali ni chakula,ndizi ni chakula,nyama,samaki matunda n.k.
Yote ni ubatili mtu.
Nnapita tu ni mahubiri ya leo.
 
Umejieleza vizuri, Lakini bado hujafahamu tofauti kati ya malaika na mzimu.
Malaika ni roho aliyeumbwa na MUNGU. Na malaika ana uwezo tofauti na malaika wengine. Malaika hana mwili, bali huweza kujivika mwili wa muda anapotaka kuwasiliana na mwanaadamu.
Vile vile malaika anaweza akawasiliiana na Mtu kupitia mawazo. ( anaweza kumuona malaika na ukaongea naye ana kwa ana Lakini ni kupitia mawazo na halisi.
Malaika wapo wema na waovu vile vile.
Jini, ni muunganiko wa malaika waovu zaidi Roho ya mmoja. Wanaweza kuwa wawili au zaidi.
Mzimu, ni Nafsi ya Mtu aliyezaliwa na mwanamke, akaishi duniani akafa , roho ikatengana na mwili, na makao yake ni mahali wanapoishi wafu wote wakisubiri hukumu Siku ya mwisho.
Tazama kitabu cha Samweli kisha cha Sauli na mchawi wa Endori alivyopandisha Nafsi ya samweli ikaongea na Sauli, na alipewa majibu halisi kuhusu kushindwa kwake, na hata kifo chake pamoja na watoto wake. Mizimu sio mashetani. Ni Nafsi za walioishi wakafa wanaishia kuzimu, mahali wanapoishi mizimu.
Mtu anapokuwa amepagawa na mizimu, huwa vigumu sana kumtenga nayo, mpaka aikatae mizimu hiyo yeye mwenyewe, na huwa kuna vitu vilivyomfungamanisha aviangamize mojawapo ni jina la kitovu.( analopewa mara baada ya kuzaliwa.).



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejieleza vizuri, Lakini bado hujafahamu tofauti kati ya malaika na mzimu.
Malaika ni roho aliyeumbwa na MUNGU. Na malaika ana uwezo tofauti na malaika wengine. Malaika hana mwili, bali huweza kujivika mwili wa muda anapotaka kuwasiliana na mwanaadamu.
Vile vile malaika anaweza akawasiliiana na Mtu kupitia mawazo. ( anaweza kumuona malaika na ukaongea naye ana kwa ana Lakini ni kupitia mawazo na halisi.
Malaika wapo wema na waovu vile vile.
Jini, ni muunganiko wa malaika waovu zaidi Roho ya mmoja. Wanaweza kuwa wawili au zaidi.
Mzimu, ni Nafsi ya Mtu aliyezaliwa na mwanamke, akaishi duniani akafa , roho ikatengana na mwili, na makao yake ni mahali wanapoishi wafu wote wakisubiri hukumu Siku ya mwisho.
Tazama kitabu cha Samweli kisha cha Sauli na mchawi wa Endori alivyopandisha Nafsi ya samweli ikaongea na Sauli, na alipewa majibu halisi kuhusu kushindwa kwake, na hata kifo chake pamoja na watoto wake. Mizimu sio mashetani. Ni Nafsi za walioishi wakafa wanaishia kuzimu, mahali wanapoishi mizimu.
Mtu anapokuwa amepagawa na mizimu, huwa vigumu sana kumtenga nayo, mpaka aikatae mizimu hiyo yeye mwenyewe, na huwa kuna vitu vilivyomfungamanisha aviangamize mojawapo ni jina la kitovu.( analopewa mara baada ya kuzaliwa.).



Sent using Jamii Forums mobile app
Vema
 
Back
Top Bottom