The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Asili yake inahusishwa na tamasha la zamani la jamii ya Waselti lililoitwa Samhain, ambalo lilikuwa likiadhimisha mwisho wa msimu wa mavuno na mwanzo wa majira ya baridi.
Hata hivyo katika kipindi cha sasa jamii nyingi duniani zimebadili maana na kila moja kuja na maana yake kulingana na mitazamo ya kitamaduni na imani za watu wa jamii husika.
Kwa sasa haloween husherehekewa kwa:
1) Kuwakumbuka wafu Katika baadhi ya tamaduni, siku hii huhusishwa na kumbukumbu za watu waliokufa.
2) Roho na ulimwengu wa mizimu. Kuna imani za kizamani kwamba wakati huu ni mpaka kati ya ulimwengu wa walio hai na wafu huwa mwembamba.
3) Mavazi ya kutisha. Watu hasa jamii za mataifa ya western hasa Marekani na canada huvaa kama mizimu, wachawi, au mashetani na viumbe wengine wa kutisha.
4) Maboga kuchongwa na kuwekwa taa au mishumaa (Jack-o'-lantern) kama alama maarufu ya Halloween.
5) Kiburudani; Watoto huenda nyumba kwa nyumba kuomba peremende (Trick or Treat) hasa kwa mataifa ya wenzetu.
Ingawa kihistoria, ina mizizi katika baadhi ya mila za kipagani za Waselti, lakini Halloween ya sasa kwa watu wengi ni siku ya burudani na utamaduni wa kijamii usiokuwa na maana kubwa.