Mizigo mizito ya kufeli kwa maisha

May 18, 2023
27
38
Watu wamekuwa ni wa kudidimizwa na mizigo ya kufeli kwao Kulingana na maisha yao hatimaye kukata tamaa na kupoteza kabisa nguvu ya kuthubutu katika miasha.

Leo basi kama mwana jamii kwa mtazamo wako au maoni yako katika makosa au kufeli kwa watu unatoa maoni gani wanapo anguka katika maisha.

Maana watu wamekuwa ni wa kukata tamaa sana na kuto kuendelea kusubutu katika maendeleo ya maisha .

"MAKOSA HAYAJA KUWA FUNZO KWA WATU WENGI BALI YAMEKUWA .......?"

1689099039680.jpg
 
Maneno ya kutia moyo,Ila ni maneno tu! Watu hawakati tamaa kwa kupenda tu, Mambo yanakuwa mazito,fulsa, ni finyu, kitaani unaambiwa ajira hakuna, Mara utasikia tamisemi hawatoi tena ajira za, ualimu mpaka mwakani, lakini chini kwa chini, kuna watu wanaajiliwa kwa kupigwa simu Moja tu, 2000,nilikosa, nafasi, ya jeshi, hapo nipo kitaa mwaka mzima! Na ka degree kangu, nimeishatembeza bahasha Sana, zikichakaa, nanunua nyingine, sasa Leo 2023! Ugumu utakua kiasi gani?
Let's be brutal blunt, bongo/afrika ni ngumu kama jiwe, ajira hakuna, zimebaki, kazi,za, kubangaiza ili tusife tu,
 
Kila kukicha,changamoto zinaongezeka. Njia pekee,ingekuwa kukabiliana nazo. Ila sasa,jamii inayokuzunguuka,badala ya kuwa chanzo cha faraja,bali ni chachu ya kuferi.
Utu umeisha. Watu walikuwa wanashikana mikono na kushirikiana. Huyu anaaweza hiki,yule anaweza kile,huyu hajui,lakini akielekezwa atafanya hiki.
Imeenda mbali zaidi,mtoto haoni umhimu wa wakubwa au wazazi. Mtoto hana sapoti ya faraja toka kwa wazazi na wakubwa. Wenye familia ndo usiseme. Bora kukesha baa kuliko kurudi nyumbani,kwenye familia ulioyoianzisha.
Mtoto anakulia katika mazingira ya kigaidi,kwa hivyo anaona ataishi kimtindo.
Wenye majukumu ya kuelimisha wenzao,wameshahamia kwingine.
Kuna mada leo ilikuwa inaongelea mzazi alomjeruhi mwalimu: huyo,walimu wenzie wakiona hivyo,wanasubiri tu mshahara,mengine mtajua wenyewe. Mwishoe ni kizazi,maadiri na maarifa ni zero.
Hicho hicho ndo kinaenda kuwalea na kuwahudumia wadogo zao.
Si kazi ndogo,lakini kila mmoja angeshikilia nafasi yake na kutimiza wajibu wake,pengine ingewezekana.
 
Vizuri poa sana kwa maoni yako haya..? Hii limekuwa ni changamoto kubwa Africa hasa Tanzania maana ndo tunaona kwenye jamii zetu hapa. Sasa thamani ya mkubwa haipo kila mtu anajiangalia kibinafsi kushikana mkono huku ktk jamii zetu ni azipo tena angalau walifanikiwa zamani kidog hii hali ina pelekea maisha kuwa magumu kila siku wazazi wabovu awakuachii misingi itakayoo kusaidia bali ni maneno makali na kukutamkia laana tu . Maisha yamekuwa yakilimbikizwa na mizigo tu na serikali yetu ajira wanapeana kidungu tu ila kusaidiana katika jamii zetu akupo kabisa . Kila mtu anajiangalia kibinafsi .
 
Back
Top Bottom