Mizengwe ilinitoa Chadema-Mwera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengwe ilinitoa Chadema-Mwera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Sep 16, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Salim Said

  KAMBI ya wabunge walioangushwa katika kura za maoni katika vyama vyao na kuamua kutimkia vyama vingine vya siasa na kuwania ubunge imezidi kuwa kubwa.

  Hivi karibuni aliyekuwa mbunge wa Tarime (Chadema), Charles Mwera alijiunga na wanachama wengine waliotimka katika vyama vyao baada ya kuhamia Chama cha Wananchi (CUF) na kuweka bayana kwamba mizengwe na ufisadi ndani ya chama hicho ndio sababu ya yeye kutimkia CUF.
  Anasema mizengwe na ufisadi huo ulitokea wakati wa mchakato wa kuteua wagombea wa ubunge na udiwani watakaopeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.

  Mwera alikabidhiwa kadi ya uanachama wa CUF na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zanzibar ambaye pia ni mgombea mwenza, Juma Duni Haji, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni Agosti 15 mwaka huu.

  “Nakukabidhi kadi hii, ili tushirikiane pamoja katika kutetea haki za wanyonge na kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania na kwa kuwa kadi hii nimeisaini mimi basi saini yangu itabakia milele Tarime,” anasema Duni.

  Akieleza kilichomkimbiza Chadema, Mwera anaweka bayana kuwa, amehama chama hicho kutokana na mizengwe iliyoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.


  Anasema Chadema kinajinadi kwa kupambana na ufisadi na kutetea haki, lakini ndani yake kina mizengwe na ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi wa chama hicho kuwaweka baadhi ya watu madarakani.

  “Chadema kinajidai kupiga vita ufisadi lakini kimejaa mizengwe. rushwa na hongo zilitumika kuhakikisha mimi sirudi kupeperusha bendera ya chama, kwa kweli sikuridhika hata kidogo,” anasema Mwera.
  “Hata nilipokata rufaa, Mbowe alilazimisha rufaa iamuliwe kwa kutumia kura za wazi. Katiba ya Chadema inampa mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa kamati kuu, hivi mtu anajua umemteua atapiga kura ya huru kupinga kura ya wazi,” anahoji Mwera.

  Aliongeza, “Haiwezekani mtu anatuhumiwa kwa rushwa na kuhonga wanachama vitu mbalimbali ili achaguliwe, halafu anahukumiwa kwa kutumia kura ya wazi ndani ya kamati kuu. Hii ni mizwenge iliyotumika kuning’oa.”

  Mwera aliangushwa katika kura za maoni za kugombea ubunge wa Tarime na Mwita Waitara, ambaye amepitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho jimbo la Tarime.

  “Mbowe alikuwa na mgombea wake na alisema kwamba hata kama Tarime itaenda kwa vyama vingine lazima mtu wake apite. Kimsingi haki haikutendeka katika mchakato wa kutafuta wagombea Tarime,” anasema Mwera.

  Anasema baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu akiwamo Profesa Mwesiga Baregu walipendekeza Mwera apewe bendera ya Chadema Tarime lakini Mbowe hakuwa tayari.

  Mwera anasema wananchi wa Tarime na wanachama wa CUF wanatakiwa kutambua kuwa jimbo hilo halitarudi CCM bali litaendelea kubakia katika kambi ya upinzani ili kuendeleza yale aliyoyaanzisha kabla na baada ya mbunge.

  “Nitaipeperusha bendera ya CUF na kuhakikisha kwamba jimbo tunalichukua. Najua nimetoka kwa wapambanaji na nimeenda kwa wapambanaji wengine kuendeleza mapambano. Jimbo la Tarime tulilipata kwa mapambano na CUF,” anasema Mwera.

  Anasema ana uhakika wa kuibuka na ushindi kwa kuwa ni mwanasiasa anayejali matatizo ya wananchi jambo ambalo lilisababisha ashinde katika uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Chacha Zakayo Wangwe.

  “Unajua chama ni njia tu lakini wanaomweka mgombea madarakani si wanachama wa chama husika ni wananchi ambao bado wananihitaji ndio mana nikachagua njia ya kuja CUF,” anasema Mwera.

  Anasisitiza kuwa, ameamua pia kuhama Chadema kwa sababu inafanya makosa yanayofanywa na CCM kwa kuweka wagombea wasiokubalika na kuendeleza uchafu wa ufisadi.

  “Mimi ni mtu wa dini, nina msimamo, hata humu ndani ya CUF hata siku moja sitatumia fedha kutafuta madaraka,” anasema Mwera.

  Mwera anasema anajivunia mabadiliko makubwa aliyoyaleta katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, ikiwa ni pamoja na kufuta hati chafu, kupata sh7 bilioni kama ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya maendeleo na kufanikisha wazee kuweza kuwalipia ada ya shule watoto wao.

  Mkurugenzi wa Mipango wa CUF, Shaweji Mketo anasema wamemfungulia Mwera milango ya kugombea ubunge wa Tarime kwa kuwa kanuni zao zinaruhusu.

  “Huyo aliyeteuliwa na chama kugombea ubunge wa Tarime ndio alikuwa akipiga simu kila siku akitaka nafasi hiyo apewe Mwera na alikubali kabisa kuwa Meneja wake wa Kampeni wa Mwera,” anasema Mketo.

  Akizungumzia kitendo cha Mwera kuhamia CUF, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anasema Mwera alitaka huruma ya Wajumbe wa Kamati Kuu bila ya kuwa na sababu za msingi za kuishawishi, baada ya kuangushwa na wanachama katika kura ya maoni.


  “Sitaki malumbano yoyote na Mwera ambaye si mwana-Chadema tena. Hana njia yoyote ya kunilaumu nadhani anafahamu mchakato wa kupata wagombea ndani ya chama, kama anakubalika na wananchi wa Tarime kwa nini hawakumchagua,” anahoji Mbowe.

  Kuhusu tuhuma ya kuendesha kura ya wazi, Mbowe anasema ndani ya Kamati Kuu ya Chadema mtindo huo ni wa kawaida na hawana cha kuficha.

  “Mwera alikataliwa na wanachama sio mimi, alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na baadaye mbunge. Tunamtakia safari njema CUF,” anasema Mbowe.


  Chanzo:Mwananchi
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hana ubavu huyo. alipata ule ubunge kwa sababu ya vichwa vilivyokuwa vinamnadi. Juzi kwenye mdahalo wa TBC1 alikuwa amevalia kombati za Chadema na kila wakati akitaka kutaja CUF anakosea anasema Chadema. Kifaa cha Chadema, Waitara alikuwa akiflow ile noma! Ngoja Chadema wafike waanze kumnadi uone, mtu mwenyewe kichwa na ananadiwa na vichwa na kwenye jimbo pekee ambako kura ya mtu haibiwi.....patamu hapo, Mwera atakuwa anasimulia tu, niliwahi kuwa mbunge miaka miwili (au pungufu?)
   
 3. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  He is ninconcoop
   
 4. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwenye Mdahalo wa TBC1 Mwera aliokolewa na Shabani Sisu kwa jinsi alivyo endesha kipindi. Sisu aliazuia maswali ambayo yalimlenga Mwera kwa kuwataka wagombea wote wajibu tofauti na alivyofanya kwa Hawa Ng'umbi Ubungo. Kwa mtindo huu alioubuni mwongoza mdahalo umepoteza mwelekeo wa kipindi kwani hata angekuwepo mgombea WA CCM asingepata taabu, kwani hakuna tena maswali mahusisi kwa wagombea husika.
   
 5. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Ndo kashasema.
   
 6. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  ninconcoop:becky: Kiingereza kigumu kumbe.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  na kipindi kitakufa karibuni maana wanazidi kukipunguza maudhui yake.
  Mtu ajibu hoja na si kusaidiwa. Kama yeye ni fisadi, goigoi anapaswa kujibu
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  TO
  Ili usipate shida ya kuanzisha thread nyingine

  Misupu
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ha ha ha umemuwahi kweli
   
 10. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Good umeanza kunielewa
   
 11. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  tandale, mwera amejua haya baada ya kukosa kupendekezwa, kugambania ubunge au ?
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Yes
   
 13. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Everything is now for sale:becky:.
   
Loading...