Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 990
Mliosoma gazeti la RAIA MWEMA la leo kuna article ya ndefu pg. 08 yenye headline isemayo BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.
Ukihesabu utaona kuwa article ina paragraph 31. Siwezi kukopi paraghraph zote bali nakopi ya 20 na 21 kama ifuatavyo:
20:
..Kuna uvumi umeenezwa kuwa Waziri Mkuu ameomba kupumzika asiwemo katika Baraza jipya (linalosukwa upya). Inadaiwa kuwa Mzee Pinda amesisitiza kuwa asifikiriwe kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anadai amechoka na kuwa yupo tayari kusaidia kwa njia nyingine..
21:
..Inasemekana wametumwa watu kadhaa kumwomba Mzee abadili uamuzi wake huo na kwamba atapewa timu bora zaidi ambayo haitampa kazi kuiongoza....
Nasisitiza, thread haina matatizo yoyote kwani nimekopi wanachokisoma mtaani kupita gazeti hili, RAIA MWEMA wana mtindo ikipita siku moja wanaweka kwenye website yao na tukijifanya tunaiogopa kwa kui-move au kuifuta basi hatutawazuia forum zingine wawe wa kwanza kuishadidia mjadala bila uoga.
SOURCE: RAIA MWEMA
DATE: MAY 02, 2012
PAGE: 08
... endapo Prof Lipumba atakubali kujiunga na hili li baraza la mawaziri uozo la CCM hakika nitamdharau milele na kutilia wasiwasi utashi wake na kazi ya usomi wake pia!!!!!!!!
Acheni CCM kimalizie uchafu wake wote kama walivyouanza mara baada ya Mwalimu Nyerere kufa ili hukumu ya walalahoi kwa chama hiki hivi karibuni isije ikasambaa hata kwa vyama ambavyo havihusiki na uhandisi wa UFISADI wote wanaolifanyia taifa hili.
Ili Prof Lipumba aweze kuingia kwenye baraza la mawaziri itabidi ajiondoe CUF na kujiunga CCM. Katiba ya sasa haitoi mwanya wa serikali ya mseto.
Kweli JF kuna vilaza,
Hebu niambie wapi katiba inambana rais kuteua mpinzani kuwa waziri?
Katiba inatamka bayana kwenye waziri mkuu tu kuwa atoke kwenye chama chenye uwakilishi mkubwa sio kwa mawaziri
Kama hujui kaa kimya, maana mnatuboa jamvini.
Prof Lipumba ni mwenyekiti wa chama cha siasa (CUF), sasa atakuwa kwenye baraza la mawaziri kama mwenyekiti wa CUF au kama nani? Hapa naongelea serikali ya mseto, na hata Zanzibar waliweza kuunda serikali ya aina hiyo baada ya kufanya marekebisho kwenye vifungu vya katiba.