Mizengo Pinda Amepwaya Sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengo Pinda Amepwaya Sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaldinali, Oct 11, 2012.

 1. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu

  Nilikuwa nimekaa natafakari utendaji kazi na ufanisi wa X-PM's wetu wa hivi karibuni specifically Sumae, Lowassa na Pinda. Specifically nikizingatia uwezo wao wa kubuni mipango kabambe ya kuendeleza taifa na kusimamia utendaji wa serikali. Kwa masikitiko makubwa mishale yote ikawa inaonyesha kuwa FISADI Lowassa amewazidi sana sana Sumae na Pinda. Uzaifu wa Sumae kwakiasi fulani unafichwa na uwezo mkubwa wa mtu aliyefanya nae kazi (Mkapa).

  Huyu Fisadi EL licha ya kufanya kazi na JK lakini bado alishaini sana kiutendaji. Mzee Pinda yeye kwakweli sioni jambo lolote la maana analofanya kwenye hiyo ofisi. Amezidiwa sana-hiko cheo ni kikubwa sana kwake.Labda ukuu wa mkoa ndio ungemfaa. Kiutendaji naweza kumlinganisha na Aliyewai kuwa rais wa Zanzibar Mzee Idris Abdul Wakil. Pinda na Wakil ni watu waliokalia tu hizo ofisi huku ofisi zikijiendesha zenyewe based on the system, structure and regulations that are in place.

  Pinda hasimamamii lolote, hana ufanisi wala creativity ya kuweza kutatua matatizo yoyote ya wananchi. Kukitokea tatizo lolote kubwa sasa hivi hakuna mtu yeyote atakaemfikiria Pinda kama kiongozi atakaekuja na kuleta ufumbuzi. For the most part watu watamfikiria Magufuli, Mwakyembe au Kagasheki.

  Ni kwanini huyu mzee yuko hivi? Hali hii ni kwaajili ya yeye mwenyewe alivyo au ni matokeo ya kufanya kazi na JK. Mbona EL alifanya kazi na JK lakini alishaini?
   
 2. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]Waziri Mkuu Asiye Waziri Mkuu-Jenerali Ulimwengu April 25, 2012

  NCHI inapitia kipindi tete, kipindi ambacho kinashuhudia maswali mengi yakiruka kutoka kila upande huku kukiwa hakuna majibu yanayoeleweka. Halitakuwa kosa kuieleza hali hii kama hali ya mkanganyiko wa kitaifa. [/FONT]
  [FONT=&amp]Hivi majuzi niliandika makala katika mlolongo wa safu hii iliyosema kwamba "kupotea tulikopotea ni kupotea kukubwa." Hali tuliyo nayo leo hainipi sababu ya kudhani kwamba hali yetu ya upotevu imebadilika sana, isipokuwa tu kwamba watu wengi zaidi wametambua kupotea kwetu ama wameamua kukupigia ukunga, kusema kwamba hata wao wameuona upotevu huo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Wiki iliyopita, bungeni, tumepata ushahidi mwingine kwamba watawala wetu wameshindwa kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya. Baadhi yao wamebanwa na wabunge ambao bila shaka wamesukumwa na hasira za wananchi dhidi ya utawala wa ubadhirifu, wizi, kutokujali, na upuuzi. Katika sakata tulilolishuhudia bungeni, mojawapo ya sababu za malumbano yale ni taarifa za ubadhirifu serikalini (kutoka kwa CAG na kwingineko) ambazo serikali inaonekana kutokuwa na uwezo wa kuzishughulikia.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kusema kweli, sura iliyojitokeza wiki hii iliyopita ni kwamba hatuna serikali inayofanya kazi kama serikali, bali tuna mkusanyiko wa maofisa waliokabidhiwa ofisi mbalimbali ambazo wanazitumia kadri wanavyojua wao na wala hawana udhibiti wa kati (central control). [/FONT]
  [FONT=&amp]Kila mmoja anasema anavyotaka, na katika kusema huko tunagundua kwamba katika ofisi yake anatenda anavyotaka pia, na hana ofisa mwandamizi wa kumwelekeza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Walichotuonyesha watawala wetu wiki iliyopita ni taswira ya mkanganyiko mkubwa na wa kutia wasiwasi kwa ye yote anayethubutu kufikiri kidogo. Nchi hii haijakabiliwa na janga kubwa la ghafla katika miaka ya karibuni. Hatujakabiliwa na vita, mafuriko makubwa wala milipuko mikubwa ya magonjwa ya kutisha. Tuthubutu kujiuliza, je, iwapo tungekabiliwa na mojawapo ya majanga kama hayo, wale tuliowaona na kuwasikia bungeni Dodoma ndio tungewaamini kwamba wangetuongoza kuishinda dharura hiyo? Wale?[/FONT]
  [FONT=&amp]Nasema hapana. Tulichokishuhudia ni msamabaratiko ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii, serikali iliyoparaganyika, mawaziri wenye kauli za kitoto, wakuu wa serikali wasiokuwa na maamuzi, waziri mkuu kivuli asiyekuwa waziri mkuu, na mkuu wa nchi mtoro.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hapo juu nimewapa pole wale walioteuliwa katika tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hii ni kwa sababu namheshimu sana Joseph Warioba, kama ninavyowaheshimu baadhi ya wajumbe wa tume yake. Ningependa Warioba, ambaye tunajua sote ni mtu makini, afanikiwe nasi tupate manufaa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Katika wiki zijazo nitaieleza ‘pole' yangu, lakini nianze tu kwa kusema kwamba, katika kazi ambazo zinaweza kufanywa na tume hiyo katika muda mfupi iliyopewa ni kuangalia nafasi ya waziri mkuu asiye waziri mkuu, anayefanya kazi chini ya mkuu wa nchi asiyekuwapo, na anayewasimamia mawaziri asiowasimamia na wanaofanya shughuli zao binafsi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hivi tunaelezaje kwamba inafikia hatua ya wabunge (bila kujali vyama) wanachukua uamuzi wa kufanya jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia yetu, kama kusukuma hoja ya kutokuwa na imani na serikali kwa sababu mawaziri wachache wanaoonekana wameboronga hawataki kuondoka hata pale wanapotakiwa kufanya hivyo na chama chao bungeni, halafu waziri mkuu hana kauli na bosi wake yuko ughaibuni?[/FONT]

  [FONT=&amp]Kama nilivyosema kuhusu ofisi ya CAG asiye CAG, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri mkuu asiye waziri mkuu? Niliwahi kuijadili mada hii katika safu hii yapata miaka miwili iliyopita, nikieleza ‘schizophrenia' ya ofisi hii. [/FONT]
  [FONT=&amp]Nilieleza kwamba katika mojawapo ya mazoezi ya kuunda serikali katika miaka ya sabini, Mwalimu Nyerere alimteua Edward Sokoine kuwa waziri mkuu, na akaulizwa na waandishi wa habari kwa nini anamteua waziri mkuu wakati Katiba haitaji ofisi hiyo.[/FONT]
  [FONT=&amp]Jibu la Mwalimu lilikuwa ni kwamba, kweli, Katiba haikusema kwamba kutakuwa na waziri mkuu, lakini pia Katiba haikutamka kwamba hakutakuwa na waziri mkuu, na kwamba waziri mkuu ni waziri kama mawaziri wengine isipokuwa yeye yuko kidogo juu ya wenziwe. ‘Schizophrenia.' [/FONT]

  [FONT=&amp]Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa "shughuli za serikali bungeni" lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga "Shut up!," hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.[/FONT]
   
Loading...