Mizani ya ufisadi: CCM bado ina kazi ya kujisafisha, muda wa kushangilia bado uko mbali sana

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kwakuwa sitaki mabishano nitakwenda na nadharia mbili. Kwanza, nitachulia, sitaki tubishane hapa kwakuwa hakuna yeyote kati yetu aliyethibitisha wala wao kukanusha, kuwa waliotajwa Mwembeyanga mwaka 2007 kama Mafisadi wa nchi hii ni mafisadi kweli. Mafisadi 11.

Waliotajwa ni Rostam, Chenge, Lowassa, Rutabanzibwa, Yona, Mramba, Kikwete, Mkapa, Balali, Karamagi na Mkono. Kati ya hao, mmoja ni Marehemu-Balali. Wawili wamefungwa jela-Mramba na Yona. Wawili ni Marais wastaafu-Mkapa na Kikwete. Mmoja aligombea Urais kupitia CHADEMA-Lowassa. Mmoja ni Mbunge-Mkono.

Kivyama, hadi naandika hapa, 10 ni wa CCM na mmoja ni wa CHADEMA. Ni 10 kwa 1. Nasema bila kutafakari mara mbilimbili kuwa hao 11 ndiyo, hadi leo, wanamiliki na kuziendesha siasa za nchi hii na hata nchi yenyewe. Ndiyo hasa 'wenye nchi'. hadi hapo, kama ni mizani ya ufisadi, CCM ina uzito zaidi. CCM ni chafu zaidi ya CHADEMA yenye mmoja tu-Lowassa.

Nadharia ya pili,katika kashfa mpya ya Stanbic Bank, wanatajwa watu mbalimbali kuhusika. Wanatajwa waliokuwa Mawaziri kwenye Serikali iliyopita, Maafisa wa TRA na hata mtoto wa Waziri wa Serikali iliyotangulia. Pia, wapo maafisa wa benki na kampuni inayohusishwa na kashfa hiyo. WanaCCM wanaopenda mambo rahisirahisi na kufichaficha ukweli, wanamng'ang'ania Awale na kuwaacha wengine. Ni kwakuwa wengine ni wa CCM?

Nasema kuwa mizani ya ufisadi bado ina uzito mkubwa kwa CCM. Kama chama tawala, hatupaswi kushangilia kuushinda ufisadi. Bado tuna safari ndefu. Tumuunge mkono Rais Magufuli katika mapambano yake dhidi ya ufisadi lakini tukumbuke wajibu wetu kichama kupambana na ufisadi chamani. Hatuna muda wa kupindisha ukweli na kuvunga kuwa hatuna makandokando na uvundo wa ufisadi.

Tuache chongo kuliita kengeza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Nani wa kumuunga mkno humo chamani kwenu??

Kikwete?? Kinana?? Nape?? au nani..

Wazee wenye hekima zao kama Mwandosya washajikataaa, wanajua chama linanuka..

Cha muhimu JPM akatae kuchukua rungu la chama kama Mwenyekiti, yeye abaki kuiongoza serikali na afanye political lobbying kwa kufanya coalition na ukawa kimya kimya ili wabunge wa ukawa wamuunge mkono bungeni, na baadhi ya wabunge wa CCM hasa wale wasio na majina nao wamuunge mkono Bungeni

Hii vita japo ni ngumu ila inapiganika............
 
Kama Mbowe na Lissu walishindwa kufanikisha kazi ya kumsafisha Lowassa na genge lake baada ya kulipwa kwa kazi hiyo, wewe kijana wa Bavicha utaiweza?

Kinachofurahisha, kushangaza na kusikitisha, CHADEMA ya sasa inajidai kwa kuwa na mafisadi wachache ukilinganisha na CCM. Chama ambacho hakijapewa hata Dola kinajilinganisha kwenye ufisadi na chama kilichoko kwenye dola kwa miaka zaidi ya 50.

Kabla hawajapewa serikali, tayari wana mafisadi, wakipewa hiyo serikali itakuwaje.

Ni aibu kwa chama cha siasa ambacho hakiwahi kupewa nchi kuanza kujivunia kuwa na mafisadi wachache.

Kwa fikra za aina hii, haishangazi wapiga kura wengi wameamua kuchagua zimwi likujualo...

Kazi uliyopewa inazidi uwezo wako kiakili, kifikra na kimtazamo.
 
Ndio umeandika nini? Uwezo wako unatia shaka sana. Umeshindwa kuona mantiki ya mtoa mada? Basi huna hadhi ya kujadili, ni sawa na kujadili maandishi ya kichina usiyoweza kuyasoma
 
Sawa lakini huyo mmoja ndo king fisad sawa na wengine 20 kwa alivyofisadi
 
Ndio umeandika nini? Uwezo wako unatia shaka sana. Umeshindwa kuona mantiki ya mtoa mada? Basi huna hadhi ya kujadili, ni sawa na kujadili maandishi ya kichina usiyoweza kuyasoma
Utawezaje kuelewa nilichokiandika wakati uwezo wako kifikra haukuruhusu?
 
Kama Mbowe na Lissu walishindwa kufanikisha kazi ya kumsafisha Lowassa na genge lake baada ya kulipwa kwa kazi hiyo, wewe kijana wa Bavicha utaiweza?

Kinachofurahisha, kushangaza na kusikitisha, CHADEMA ya sasa inajidai kwa kuwa na mafisadi wachache ukilinganisha na CCM. Chama ambacho hakijapewa hata Dola kinajilinganisha kwenye ufisadi na chama kilichoko kwenye dola kwa miaka zaidi ya 50.

Kabla hawajapewa serikali, tayari wana mafisadi, wakipewa hiyo serikali itakuwaje.

Ni aibu kwa chama cha siasa ambacho hakiwahi kupewa nchi kuanza kujivunia kuwa na mafisadi wachache.

Kwa fikra za aina hii, haishangazi wapiga kura wengi wameamua kuchagua zimwi likujualo...

Kazi uliyopewa inazidi uwezo wako kiakili, kifikra na kimtazamo.
Ccm ni wezi na hizo mbio za magufuli ni za sakafuni
 
Una tatizo la kurespond negatively bila kufikiri au kutafakari kila analopost Mzee Tupatupa
 
Kama unadhani nina tatizo, wala lisikusumbue, wewe endelea kurespond positively kwa kufikiri kila analopost huyu kijana wa bavicha/ bush lawyer
 
Ccm ni wezi na hizo mbio za magufuli ni za sakafuni
Nani amekwambia mbio za magufuli siyo za sakafuni?

Nani amekwambia CCM siyo wezi? Hujasoma hili andiko la kijana wa bavicha akijivunia kuwa na mafisadi wachache ndani ya CHADEMA ukilinganisha na CCM?
 
Najitokeza kukupongeza na kukutakia maisha marefu, vilevile kukuombea siku moja uwe mtu mwenye uamuzi wa mwisho hapa nchini(Rais) (japo sijui kama ni nani wewe isijekuwa naongea na rais mstaafu) ili haya uliyoyasema uje uyafanyie kazi kwa kuzingatia kuwa wapiga kura wengi wa ccm ni maskini wa kutupwa (mafukara) ambao wanahitaji kusaidiwa na sio kudhulumiwa.

Mungu yupo,..... umeongea kama siyo wewe wa Lumumba
 
Kama Mbowe na Lissu walishindwa kufanikisha kazi ya kumsafisha Lowassa na genge lake baada ya kulipwa kwa kazi hiyo, wewe kijana wa Bavicha utaiweza?

Kinachofurahisha, kushangaza na kusikitisha, CHADEMA ya sasa inajidai kwa kuwa na mafisadi wachache ukilinganisha na CCM. Chama ambacho hakijapewa hata Dola kinajilinganisha kwenye ufisadi na chama kilichoko kwenye dola kwa miaka zaidi ya 50.

Kabla hawajapewa serikali, tayari wana mafisadi, wakipewa hiyo serikali itakuwaje.

Ni aibu kwa chama cha siasa ambacho hakiwahi kupewa nchi kuanza kujivunia kuwa na mafisadi wachache.

Kwa fikra za aina hii, haishangazi wapiga kura wengi wameamua kuchagua zimwi likujualo...

Kazi uliyopewa inazidi uwezo wako kiakili, kifikra na kimtazamo.

hii ni shida ya kukurupuka, tulia usome na uelewe au humjui mleta mada?
 
Kwakuwa sitaki mabishano nitakwenda na nadharia mbili. Kwanza, nitachulia, sitaki tubishane hapa kwakuwa hakuna yeyote kati yetu aliyethibitisha wala wao kukanusha, kuwa waliotajwa Mwembeyanga mwaka 2007 kama Mafisadi wa nchi hii ni mafisadi kweli. Mafisadi 11.

Waliotajwa ni Rostam, Chenge, Lowassa, Rutabanzibwa, Yona, Mramba, Kikwete, Mkapa, Balali, Karamagi na Mkono. Kati ya hao, mmoja ni Marehemu-Balali. Wawili wamefungwa jela-Mramba na Yona. Wawili ni Marais wastaafu-Mkapa na Kikwete. Mmoja aligombea Urais kupitia CHADEMA-Lowassa. Mmoja ni Mbunge-Mkono.

Kivyama, hadi naandika hapa, 10 ni wa CCM na mmoja ni wa CHADEMA. Ni 10 kwa 1. Nasema bila kutafakari mara mbilimbili kuwa hao 11 ndiyo, hadi leo, wanamiliki na kuziendesha siasa za nchi hii na hata nchi yenyewe. Ndiyo hasa 'wenye nchi'. hadi hapo, kama ni mizani ya ufisadi, CCM ina uzito zaidi. CCM ni chafu zaidi ya CHADEMA yenye mmoja tu-Lowassa.

Nadharia ya pili,katika kashfa mpya ya Stanbic Bank, wanatajwa watu mbalimbali kuhusika. Wanatajwa waliokuwa Mawaziri kwenye Serikali iliyopita, Maafisa wa TRA na hata mtoto wa Waziri wa Serikali iliyotangulia. Pia, wapo maafisa wa benki na kampuni inayohusishwa na kashfa hiyo. WanaCCM wanaopenda mambo rahisirahisi na kufichaficha ukweli, wanamng'ang'ania Awale na kuwaacha wengine. Ni kwakuwa wengine ni wa CCM?

Nasema kuwa mizani ya ufisadi bado ina uzito mkubwa kwa CCM. Kama chama tawala, hatupaswi kushangilia kuushinda ufisadi. Bado tuna safari ndefu. Tumuunge mkono Rais Magufuli katika mapambano yake dhidi ya ufisadi lakini tukumbuke wajibu wetu kichama kupambana na ufisadi chamani. Hatuna muda wa kupindisha ukweli na kuvunga kuwa hatuna makandokando na uvundo wa ufisadi.

Tuache chongo kuliita kengeza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Umeongea ukweli lakini kuna watafuta vyeo humu watakutukana mpaka basi.Magufuli ana mtihani naamini hawezi fauru.
 
kibaraka wa mtaa wa ufipa kinondoni leo umeandika point. naunga mkono. suala la ufisadi ni suala la mfumo ambao kiuhalisia upo ccm. kwa ccm wanakazi ya kufanya kuliokoa taifa hili katika lindi hili la umasikini.

Kwakuwa sitaki mabishano nitakwenda na nadharia mbili. Kwanza, nitachulia, sitaki tubishane hapa kwakuwa hakuna yeyote kati yetu aliyethibitisha wala wao kukanusha, kuwa waliotajwa Mwembeyanga mwaka 2007 kama Mafisadi wa nchi hii ni mafisadi kweli. Mafisadi 11.

Waliotajwa ni Rostam, Chenge, Lowassa, Rutabanzibwa, Yona, Mramba, Kikwete, Mkapa, Balali, Karamagi na Mkono. Kati ya hao, mmoja ni Marehemu-Balali. Wawili wamefungwa jela-Mramba na Yona. Wawili ni Marais wastaafu-Mkapa na Kikwete. Mmoja aligombea Urais kupitia CHADEMA-Lowassa. Mmoja ni Mbunge-Mkono.

Kivyama, hadi naandika hapa, 10 ni wa CCM na mmoja ni wa CHADEMA. Ni 10 kwa 1. Nasema bila kutafakari mara mbilimbili kuwa hao 11 ndiyo, hadi leo, wanamiliki na kuziendesha siasa za nchi hii na hata nchi yenyewe. Ndiyo hasa 'wenye nchi'. hadi hapo, kama ni mizani ya ufisadi, CCM ina uzito zaidi. CCM ni chafu zaidi ya CHADEMA yenye mmoja tu-Lowassa.

Nadharia ya pili,katika kashfa mpya ya Stanbic Bank, wanatajwa watu mbalimbali kuhusika. Wanatajwa waliokuwa Mawaziri kwenye Serikali iliyopita, Maafisa wa TRA na hata mtoto wa Waziri wa Serikali iliyotangulia. Pia, wapo maafisa wa benki na kampuni inayohusishwa na kashfa hiyo. WanaCCM wanaopenda mambo rahisirahisi na kufichaficha ukweli, wanamng'ang'ania Awale na kuwaacha wengine. Ni kwakuwa wengine ni wa CCM?

Nasema kuwa mizani ya ufisadi bado ina uzito mkubwa kwa CCM. Kama chama tawala, hatupaswi kushangilia kuushinda ufisadi. Bado tuna safari ndefu. Tumuunge mkono Rais Magufuli katika mapambano yake dhidi ya ufisadi lakini tukumbuke wajibu wetu kichama kupambana na ufisadi chamani. Hatuna muda wa kupindisha ukweli na kuvunga kuwa hatuna makandokando na uvundo wa ufisadi.

Tuache chongo kuliita kengeza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kama Mbowe na Lissu walishindwa kufanikisha kazi ya kumsafisha Lowassa na genge lake baada ya kulipwa kwa kazi hiyo, wewe kijana wa Bavicha utaiweza?

Kinachofurahisha, kushangaza na kusikitisha, CHADEMA ya sasa inajidai kwa kuwa na mafisadi wachache ukilinganisha na CCM. Chama ambacho hakijapewa hata Dola kinajilinganisha kwenye ufisadi na chama kilichoko kwenye dola kwa miaka zaidi ya 50.

Kabla hawajapewa serikali, tayari wana mafisadi, wakipewa hiyo serikali itakuwaje.

Ni aibu kwa chama cha siasa ambacho hakiwahi kupewa nchi kuanza kujivunia kuwa na mafisadi wachache.

Kwa fikra za aina hii, haishangazi wapiga kura wengi wameamua kuchagua zimwi likujualo...

Kazi uliyopewa inazidi uwezo wako kiakili, kifikra na kimtazamo.

Magufuli hawezi kitu kwa sababu mafisadi yamemuweka ikuu mwenyewe ni fidi rejea nyumba za serikali rioti ya CAG ubadhirifu wa bilioni zaidi ya350
 
Magufuli hawezi kitu kwa sababu mafisadi yamemuweka ikuu...
Lowassa ndiye ambaye angeweza kupiga vita mafisadi. Hebu fanya hivi: zungusha zungusha zungusha mikono halafu ropoka mabadilikooo....
 
umesema.....muda wa kushangilia bado....... sana. natofautiana nawe kwa sababu ccm imeathiriwa na ufisadi kwa muda mrefu. wana ccm tumetukanwa, tumezomewa, tumezodolewa, tumeishi kwa aibu hata watoto wadogo wakakaririshwa ubaya wa ccm na kutukejeli.tulikuwa ktk. mateso mazito, hasa miaka hii 5 ya mwisho ya jk. je,wewe u mgeni tz? je, wewe ni mwana ccm kweli? huyajui haya? ingawaje safari bado ni ndefu, wana ccm tuna kila sababu ya kushangilia kwa sababu we've seen a ray of hope, we've seen light at the end of the tunnel ktk. vita dhidi ya ufisadi. sasa tuna matumaini ccm itarudisha haiba yake nzuri mbele ya jamii. tunaposhangilia tunawaonyesha majemedari wetu walio mstari wa mbele tunafurahia kazi yao, tuna imani nao na kwa kufanya hivyo tunawatia moyo. please jumuika na wana ccm ktk. kushangilia. usiogope.
 
Back
Top Bottom