PutinV
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 1,046
- 1,651
Salamu wakuu,
Baada ya kutazama baadhi ya filamu na tamthilia mbalimbali zinazo husu au zinazo husisha mapigano (filamu inaweza ikawa na lengo fulani lakini mapigano yakawepo kwa kiasi kidogo sana) nikajikuta naangukia kwenye filamu yenye kisa kimoja cha binti mwenye uwezo wa juu katika matumizi ya upanga, alikuwa akiitwa Cheok Sa Gwang, the last official successor of Goksan swordmanship (TV series character). Yap ni kweli ukoo wa Goksan upo huko Korea hadi leo lakini sina uhakika kama wana swordmanships au tekniki zao za kutumia upanga. Hapa unaweza kujiuliza swali na je hawa watu na technique zao wapo? Au wamewahi kuwepo?
Miyamoto Musashi pia anajulikana kama Shinmen Musashi-no-Kami Fujiwara no Genshin au MUSASHI SENSEI.
Sanamu ya Musashi Sensei
Musashi Sensei alizaliwa katika jimbo la Harima huko Japan mwaka 1584, wakati ambapo Japani ilikuwa katika hali ya machafuko na Vita. Alizaliwa wakati ambapo mashujaa wajulikanao kama samurai walikuwa wakihitaka zaidi.
Wakati wa Musashi Sensei, ilikuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kubadili jina lake mara kwa mara kulingana na anavyokua, wakati wa utoto wake Musashi Sensei aliitwa Shinmen Bennosuke na alianza kupokea mafunzo ya kupigana kwa upanga kutoka kwa baba yake Shinmen Hirata Munisai akiwa na miaka kumi na tatu.
Wakati wa Musashi ilikuwa ni hamu ya kila mpiganaji na mtumiaji wa upanga kujihusisha katika mapambano mbali mbali ili kupata umaarufu na kujenga jina katika jamii na ndivyo ilivyokuwa kuwa kwa Musashi ambaye alianza kujihusisha katika mapambano hayo katika umri wa miaka 13 na alipokuwa na miaka 16 alimshinda shujaa mwingine maarufu kwa kipindi hicho, Tadashima Akiyama.
Vijana wa Kijapani katika pambano la kutafuta sifa.
Mwaka 1600 vilizuka vita maarufu katika historia ya Japan, vita vya Sekigahara ambavyo vingeamua hatima ya Japani kwa karne tatu zilizo fuata. Ni katika vita hivi, mtu maarufu kwa kina la Togukawa Ieyasu alifanikiwa kushika madaraka na kuwa Shogun (Kiongozi wa kijeshi mwenye madaraka ya juu zaidi) wa Japani. Hapa ndipo kilianza kipindi kijulikanacho kama Edo period (1603-1868) katika historia ya Japan. Musashi Sensei aliishi ujana wake katika kipindi hiki kigumu cha Edo na alipigana katika upande wa Ukita Hideie wakati wa vita vya Sekigahara ambapo Ukita alishindwa vibaya na Togukawa hivyo ikamlazimu Musashi kukimbia baada ya vita kuisha akihofia uhai wake.
Baada ya kukimbia mwaka 1603, Musashi alielekea Kyoto na Mwaka 1604 alipigana mapigano matatu muhimu katika historia yake ya upiganaji. Safari hii Musashi hakuwa anampiga mapambano ya mchezo mchezo bali mapambano ya kufa na kupona. Katika mapambano yote matatu alipigana na wanafamilia wa familia maarufu ya Yoshiaka amabayo ilikuwa maarufu kwa kutoa wapiganaji maarufu na wenye weledi mkubwa. Familia ya Yoshiaka ilikuwa ikimiliki chuo cha mafunzo ya upiganaji kwa kutumia upanga.
Mapambano mawili ya kwanza kati ya mapambano matatu alipigana na kuwashinda mtu na kaka yake Seijuro na Denshijiro na hapa ndipo wanafamilia na wafuasi wote wa familia ya Yoshiaka walipo anza kupata wasiwasi kuhusu Musashi na kumuona kama tishio. Pamoja na kupoteza mara mbili mapambano yaliyopita, familia ya Yoshiaka haikutaka kukubali kupoteza kwa mpiganaji asiyekuwa na jina (wakati huo wapiganaji walikuwa wakitambulika kwa majina ya vyuo walivyo jifunzia au walimu walio wafundisha lakini Musashi hakuwa na jina kwani maisha yake yalikuwa yamevurugika kutokana na kukimbia kwake) hivyo wakaandaa pambano la tatu la kulipiza kisasi ambapo Musashi angepambana na Matashichiro, mtoto wa Seijuro aliyekuwa na umri wa miaka 13 wakati huo. Safari hii familia ya Yoshiaka na wafuasi wao wote wakiwemo wanafunzi wa chuo chao walikuwa wamejipanga kuhakikisha Musashi 'hachomoki' kwa namna yoyote ile. Wakati wa pambano la kufa na kupona, wafuasi na wanafunzi wa chuo cha Yoshiaka walipo ona Matashichiro amezidiwa waliamua kuvunja sheria za pambano na kuamua kuingilia pambano ambalo lilikuwa haliwahusu! Lakini hii haikuwa kikwazo kwa Musashi ambaye alipigana na kuwashinda zaidi ya wapiganaji sitini wenye panga. Wapiganaji wote sitini walio ingilia pambano hilo waliuawa akiwemo na Matashichiro na huu ndio ulikuwa mwisho wa ubabe wa familia ya Yoshiaka katika utaalamu wa kutumia upanga na mwanzo wa historia ya shujaa Musashi Sensei.
Jiwe la ukumbusho kulienzi pambano la Musashi dhidi ya familia ya Yoshiaka.
Kwa miaka iliyofuata Musashi Sensei alianza kuzunguka nchini kote akiwa kama Musha Shugyo (Musha Shugyo ni jina alilo itwa shujaa aliyekuwa akitembea sehemu mbalimbali huku akitafuta mapambano na kujifunza mambo mbalimbali) na katika kipindi hiki alipata mapambano na washindani wengi sana walio taka kupata sifa kwani habari za ushujaa wake dhidi ya familia ya Yoshiaka zilikuwa zimetapakaa nchi nzima.
Musha Shugyo
Katika kipindi hiki akiwa kama Musha Shugyo, Musashi alipambana mapambano mengi lakini mapambano maarufu kati ya hayo ni haya yafuatayo:
>Alipambana na ma-monk wa hekalu la Hizoin walio kuwa maarufu katika utaalamu wao wa kutumia Yarijutsu (aina fulani ya mikuki) na kuwashinda.
>Alipambana na Muso Gonnosuke mwanzilishi wa tekniki au style ya Jojutsu Shindo Muso Ryu. Kifupi baada yaa kupambana na Musashi na kushindwa (haijulikani kwanini hakumuua), Muso ndipo alipo gundua style ya Jojutsu na kurudi kuja kupambana na Musashi kwa mara ya pili ambapo pambano lao liliisha bila kupata mshindi!
Muso Gennosuke
>Alipigana na mtu hatari sana, Shishido Baiken mtaalamu wa kutumia kusarigama, silaha ambayo inaundwa na mnyororo wenye chuma chenye makali na chenye umbo la mundu (sickle) kwa mbele na kipande kizito cha chuma kwa nyuma. Kifupi hii silaha ni ngumu sana katika kutimia na pia ni ngumu kupambana na mtumiaji wa silaha kama hii lakini Musashi alimshinda Shishido.
Silaha ya Shishido Baiken.
PAMBANO DHIDI YA KOJIRO.
Pamoja na mapambano yote hayo pambano maarufu zaidi la Musashi lilikuwa dhidi ya Sasaki Kojiro mwaka 1612 mwanzilishi wa shule ya mapigano ya Ganryu pia alikuwa samurai maarufu kwa kipindi hicho! Uwezo mkubwa aliokuwa nao Kajiro unamfanya awe mmoja wa ma-samurai maarufu wa muda wote. Kojiro alikuwa amejifunza kutumia upanga kutoka kwa mwalimu (master) maarufu kwa kipindi hicho, Toda Seigen kutoka shule ya Chujo Ryu.
Hadi sasa Kojiro anatajwa kama mmoja ya wapiganaji wa upanga bora zaidi kuwahi kutokea.
Wakati huo Kojiro alikuwa mwalimu katika shule ya Hosokawa Tadaoki na Musashi aliomba pambano na Kojiro kupitia kwa Nagaoka Sado ambaye alikua rafiki mkubwa wa Kojiro.
Pambano lenyewe lilipiganiwa katika kisiwa cha Funajima. Siku ya pambano Kojiro aliwasili mapema lakini Musashi alichelewa na alifika baada ya saa mbili (kwenye Kiswahili hakuna masaa mawili) na kumkuta mwaka mpinzani wake akimngoja, bila kunena lolote pambano lilianza ambapo Musashi alimshambulia kwa nguvu sana Kojiro. Inasemekana upanga wa Kojiro ulikuwa mrefu sana ambao ulimpa 'advantage' ya kumshambulia adui akiwa mbali lakini haikuwa shida kwa Musashi alijiandaa vyema kwani alikuja na kasia alilo tumia wakati alipofika na mtumbwi kisiwani hapo. Wakati wa pambano Kojiro alimpiga Musashi pigo ambalo Musashi alikwepa lakini aliishia kuchanwa kidogo usoni kwa ncha ya upanga mrefu wa Kojiro, Palepale naye Musashi alimpiga Kojiro kwa kasia alilo kuwa nalo, pigo lililo mdondosha Kojiro chini. Wakati Kojiro akiwa chini alijaribu kukata miguu ya Musashi alikwepa kwa kuruka juu kisha akampiga kwa nguvu nyonga ya Kojiro tendo lililo pelekea kifo cha Kojiro.
Sanamu katika kisiwa cha Funajima kuenzi pambano la Musashi na Kojiro.
Baada ya pambano la Kojiro, Musashi alikua anaelekea kutimiza umri wa miaka 30. Kwa mujibu wa kitabu chake maarufu cha THE FIVE RINGS, Musashi anasema pambano dhidi ya Kojiro lilimuathiri sana kisaikolojia huku likimuacha na maswali mengi. Anasema alikuwa akijiuliza sana kuwa ni kwanini alipata ushindi katika mapambano yote hayo aliyo pigana? Je ni kwa sababu ya nguvu zake? Au wapinzani wake walikuwa dhaifu sana? Au labda ulikuwa ni mpango wa Mungu?
Basi Musashi aliamua kusafiri sehemu mbali mbali ili kutafuta majibu ya maswali aliyokuwa akijiuliza kwa muda mrefu na ndivyo aliyokuja na style yake ya Niten Ichi Ryu.
Baada ya kipindi hiki Musashi alikua ni zaidi ya shujaa kwani alikuwa amejikita katika zaidi katika sanaa kama uchoraji, uchongaji, uchoraji wa ramani za majengo na ushairi.
Mwaka 1621, Musashi alipigana pambano jingine lakini safari hii halikuwa pambano la kufa na kupona basi ilikuwa ni katika harakati za kuipa umaarufu style yake ya upiganaji ya Hyoho Niten Ichi Ryu ambapo mpiganaji hutumia panga mbili, mmoja ukiwa mfupi kuliko kawaida. Mpinzani wake katika pambano hilo alikuwa Miyaki Gunbei ambaye alikua mwepesi sana katika kushambulia kwake lakini mara zote hizo Musashi alikwepa ndipo alipo amua kumchoma Musashi Kwa ncha ya upanga wake lakini Musashi alifanikiwa kuzuia kwa kutumia upanga mdogo kisha akamuwekea shingoni Miyaki upanga mrefu uliokuwa mkono wa kulia wa Musashi kuashiria Miyaki amepoteza pambano hilo. Baada ya kuona hivyo Miyaki alianza kulia na kumuomba Musashi awe mwalimu wake.
Musashi Sensei na staili yake ya Hyoho.
Musashi Sensei hakuoa wala kupata watoto wake mwenyewe bali alijitolea kuwalea watoto wawili Mikinosuke na Iori ambao pia baadaye walikuja kuwa wapiganaji maarufu.
Mbali na kuwa shujaa, siku zote Musashi anachukuliwa kama mwalimu, mtu mwenye busara hekima na uhuru, mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza watu.
Pia nafahamu wengi mtauliza kama jamaa alikuwa wanted ilikuwaje akasafiri nchi nzima bila kusumbuliwa au kukamatwa? Ni hivi, huko Japani ni heshima sana kuwa shujaa na mashujaa waliheshimika sana kwa kipindi hicho hivyo Musashi alipokea ofa nyingi za kujiunga kwenye vikosi vya baadhi ya watu wakubwa serikalini, hadi wakati wa kufariki alikuwa akiishi kwenye kasri la kigogo huko Hombu Dojo.
Musashi Sensei alifariki dunia tarehe 19 May 1645, kifo kilicho sababishwa na kansa ya mapafu.
Kaburi la Musashi Sensei
Kama alivyo omba kabla ya kufa kwake alizikwa akiwa amevaa vazi la kijeshi la yoroi na kuzikwa katika kijiji cha Yuji.
Vazi la yoroi.
Ukipenda kujua zaidi juu ya huyu jamaa 'shujaa mwenye maono' tafuta kitabu chake cha five rings.
-
Je na sisi hatuna mashujaa wapiganaji wa kuwaenzi kama wenzetu wanavyo fanya, Afrika Kusini wanawaenzi Shaka Zulu na majenerali wake Mgobozi na Mdlaka bila kumsahau Mzilikazi. Korea Wanamuenzi jenerali wao kipenzi Kim Yushin. Tunahitaji kuwaenzi mashujaa wetu pia japo wanasema "Histo remember kings and not soldiers" lakini hata soldiers wana haki yao.
Much respects,
Sf