Hivi hakuna chombo chochote cha kufuatilia aina ya matangazo ambayo makampuni wanayaandaa kabla hayajatangazwa kwa umma?
Ilipokuwa ikiitwa TIGO hawa jamaa walituletea msemo kwenye tangazo lao usemao: JAZA UJAZWE. Huu msemo una ukakasi wa kihuni/kingono.
Sasa wamejibadili jina na kuwa Mixz by Yas. Jina tu ni la kihuni halafu wanatuletea msemo kwenye tangazo lao usemayo: IKIINGIA TU, GOLI! Maana yake nini kama si uhuni na ungono tu??
Serikali iwaangalie hawa wahuni wanatuharibia maadili!