Wanaotaka kurudi na warudi tunajua washanunnuliwa na manyani wenzao, UKAWA itaendelea kuwepo
ungemuuliza kwanza swali dogo tu, je ana ufahamu wowote kuhusu money laundry ?
Kupitia Bunge la Katiba, wananchi wapenda Taifa endelevu wanazidi kubainishiwa ukweli ulioko ndani ya mioyo na fikra za baadhi ya viongozi kupitia kundi la vyama vya siasa wanaojiita kwa sasa UKAWA.
Waingereza wanasema, Birds of a feather flock together kwa maana kuwa, kwa sasa Bunge la Katiba limewakutanisha vinara wa ubaguzi na wasaka madaraka kwa njia zozote zile kuanzia viongozi wa vyama ambao baadhi yao wamekuwa katika uongozi wa juu wa vyama vya siasa kuanzia 1995 huku wengine wakijaribu kuwaomba wananchi wawaamini na kuwapa ofisi kuu nchini kupitia kura za Urais (Rais wa Tanzania) lakini hawakufanikiwa kwa vile kile ambacho wananchi walikuwa wana wasiwasi nacho kuhusiana na fikra na mitazamo yao kama viongozi wakuu imeanza kudhirika katika bunge Maalum.
Ubaguzi wao umezaliwa ndani ya vyama vyao, ukamea na kuimarika huku baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi ndani ya vyama wakiishia kuwa ni wahanga wa ubaguzi huo. Wengine walifukuzwa na huku wengine wakinyang'anywa madaraka. Kwa sasa ubaguzi unatafuta njia nyingine ya kujipandikiza kitaifa kupitia mchakato wa katiba baada ya kutamalaki ndani ya vyama vyao ili waendeleze nia yao ya kusaka madaraka kwa gharama zozote.
Dhambi ya ubaguzi itawatafuna wao wenyewe na katika dhambi hiyo, hawawezi kufanikiwa kupata kile wanachokitaka kwa nguvu zote. Huwezi kutenda dhambi mbaya kama hii halafu usalimike. Kwa sasa ukweli umeanza kubainika.
Huwezi kufanya ubaguzi na siasa za matukio halafu ufanikiwe. Siyo muda mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao.
Pesa wanazopata baadhi ya viongozi wa UKAWA ili kusaidia harakati zao za kulimega taifa ndizo zitakuwa sumu ndani ya UKAWA.
Muda huwa ni jibu mbadala.
WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.
Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.
Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.
Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha, anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.
Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.
Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.
Wakati haya yakitokea ndani ya UKAWA, Rais Kikwete ametoa siku nyingine 60 za nyongeza kwa Bunge Maalum la Katiba ili kukamilisha kazi waliyopewa wabunge wa bunge Maalum la Katiba.
Rais Kikwete alisema, Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo, alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.
Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine, alibainisha.
Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.
Wakishindwa kutupa katiba katika muda tuliowapa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni, alisema bila kufafanua zaidi.
Chanzo: Habarileo.
Hilo swali lako nitakujibu baada ya uchaguzi 2015Mkuu naomba unielimishe: Hivi UKAWA ni SACCOS, NGO, Chama au kitu gani?
Huyu Mwanadiwani kwa story za kubuni ndiye mwenyewe. Anatujazia server bure. Nafikiria kumpeleka kwenye ignore list yangu kwani sasa nimechoka kusoma uharo wake hapa.
Tiba

Ndugu, wewe uko hapa pia unajadili UKAWA halafu unaanza kulalamika kama wanaJF wengine ndiyo wanajikita katika mambo ya Katiba.
Unatakiwa uanzishe mjadala kama unadhani kuna jambo ambalo ni muhimu katika fikra zako zaidi ya mjadala wa Katiba.
Ndugu, Nidhani hujaisoma habari yote na kama umeisoma yote ungegundua kama hii ni habari kutoka gazeti la kitaifa la Habarileo.Huyu Mwanadiwani kwa story za kubuni ndiye mwenyewe. Anatujazia server bure. Nafikiria kumpeleka kwenye ignore list yangu kwani sasa nimechoka kusoma uharo wake hapa.
Tiba
Ndugu, Nidhani hujaisoma habari yote na kama umeisoma yote ungegundua kama hii ni habari kutoka gazeti la kitaifa la Habarileo.