MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,268
WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.
Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.
Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.
"Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha," anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.
Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.
Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.
Wakati haya yakitokea ndani ya UKAWA, Rais Kikwete ametoa siku nyingine 60 za nyongeza kwa Bunge Maalum la Katiba ili kukamilisha kazi waliyopewa wabunge wa bunge Maalum la Katiba.
Rais Kikwete alisema, "Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo," alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.
"Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine," alibainisha.
Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.
"Wakishindwa kutupa katiba katika muda tuliowapa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni," alisema bila kufafanua zaidi.
Chanzo: Habarileo.