Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,221
Morogoro Road
Jangwani
Picha chache kuonyesha yaliyotokea jana yanadhihirisha kuwa kuna sehemu tumelala.
Mvua hiyo kubwa inaelekea imeonyesha udhaifu mkubwa wa miundombinu ya maji jijini Dar es salaam.
Kwa miongo ya miaka, Halmashauri za Jiji na Serikali kuu zimeendelea kupuuzia namna ya kuijenga na kuihudumia kwa matengenezo ya mara kwa mara miundo mbinu ya Jji hili la DSM.
Mto Msimbazi pamoja na ukaribu wake baharini akini hakuna kabisamtaalam wala mwanasiasa anyefikiria kuuchimba mto huu ili uweze kuhimili sehemu kubwa ya maji ya mvua ya Jiji la DSM.
Wenzetu wazungu, kwa aibu inabidi tuwarejee maana sisi pamoja na kuwa na Planners, wahandis wazuri, lakini uwezo wao wa kufikiri ni kufikia tu ukurugenzi na kupnda ma V8 na hawana wanaofikiria zaidiya hapo.
Wazungu kwao mito yote iliyopitia katikati ya Jiji, inakuwa ndio kupona kwa Jiji, iwe London-Thames, Washington-Potomac, Japan, Misri, Khartoum na kwingineko.
Sisi wataalam wetu wamelaniwa?
Kwa nini hawchukui hatua mahsusi ya kurasimisha njia za maji kisheria na ili iweze kuhudumiwakama barabara zinazopewa umuhimu?
This cant go on!!
Hali hii haiwezi kuendelea kama nusiness as usual.