Mitumba bei ya Jumla; Wapi naweza kupata mitumba Grade A

Honest One

JF-Expert Member
May 12, 2017
235
274
Habar za asubuhi wadau,mi mgeni kidogo hapa Dar.Baada ya kukaa muda wa miaka 2 bila ajira,imenibidi nitoke kijijin nije huku Dar ninunue mitumba ya Grade A ili niipeleke huko kijijini kuuza.Mtaji wangu ni laki tatu.Ninaomba mnielekeze wapi naweza pata mzigo.Hapa nilipofikia kwa ndugu wanadai hawajui hayo mambo kwa kuwa wana kazi za maana kwa hiyo inabidi niangaike mwenyewe.Ushauri wenu pia nitaupokea,naomba tusaidiane jamani
 
ukipata leta mrejesho nasi tujifunze. zingatia taarifa mahsusi: hali ya duka la muuzaji, lugha yake (ukarimu), maelezo nacelimu yake kwako juu ya biashara husika, viwango vya ubora wa bidhaa, bei zake, usafiri, faida uliyopata vs ulivyotarajia, je kuna ulazima wa kusafiri hadi dar kuchukua mzigo/ hakuna uwezekano wa kutumiwa, changamoto, funzo lako juu ya mradi huo, ushauri wako kwa vijana na kundirika wanaoogopa kuthubutu kujaribu biashara. hakika JF haijawahi kuwa na choyo; naamini utatusaidia
 
Nitaleta mrejesho kaka,mimi sina roho mbaya pia.Malengo yangu nikishapata mtu mwaminifu atakuwa ananitumia mzigo mimi nikiwa zangu mkoani
 
Grade A nenda mtaa wa Kongo opposite na nyuma ya DDC kariakoo uliza MACHATA. Utapata japo nina mashaka kama utapata kwa laki tatu. Grade A si mchezo, shati moja unauziwa 15,000 unadhani bale itakuwa bei gani?

Ila fika ndo sehemu ya kukusanya uzoefu na data
 
Back
Top Bottom