SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
TAHOSA ni chama cha walimu wakuu wa shule hasa za Sekondari. Moja ya kazi zao ni kutunga mitihani ya majaribio kwa wanafunzi, yaani hii mitihani inayoitwa “Mock Examinations” au kwa kifupi kilichozoeleka “mock”.
Shida yangu ninayowaeleza watanzania hasa sisi ambao ni wazazi wa wanafunzi ni jinsi TAHOSA na halamashauri zinavyoendesha mitihani hii ya mock.
Kabla ya kulieleza tatizo lao tueleze kwanza utaratibu wa utungaji wa mitihani unavyokuwa.
Mtihani au “examination” maana yake kipimo kinachopima kama mwanafunzi ameelewa yale aliyofundishwa. Hivyo Baraza la Mitihani (NECTA) humpima mwanafunzi kwa mitihani kwa topic zote za sekondari.
Mtihani wa NECTA unapotoka huwa ni November kwa form 4. Hii maana yake ni kwamba NECTA inatoa mtihani baada ya ratiba yay a ufundishaji kuwa imeisha yote.
Vilevile mwaka mmoja kabla ya mtihani NECTA huwa wanayo format ya mtihani utakavyokuwa na wanaisambaza kwa wananchi wote muione, siku hizi kuna intenrnet ukiitaka unaipata kwenye simu yako.
Sasa je tatizo la mtihani wa mock ni nini? Mtihani wa mock ni mtihani unaofanywa mwezi wowote kabla ya kumaliza syllabus.
Mwaka jana D’Salaam walifanya mtihani mwezi July na mwaka huu Mock inafanywa mwezi May. Hii maana yake mtihani wa mock unafanywa wakati syllabus haijaisha.
Tatizo la kwanza la walimu wakuu hapa nchini na TAHOSA yao ni kwamba hawajawahi kutangaza forma ya mitihani ya mock kama wenzao NECTA wanavyofanya.
Matokeo yake ni kwamba wazazi, walimu na kila mmoja hujui wanatunga kuishia wapi.
Kilicho cha uhakika ni kwamba mwanafunzi atakuwa amefundishwa syllabus yote ya form 1 mpaka form 3. Lakini mwezi May 2023 unaana ikiwa ni wiki ya 15 ya masomo. Ukichukulia somo la Mathematics linaloongoza kwa kufeslisha wanafunzi huo mwezi May hiyo wiki ya 15 maana yake mtoto ndiyo kwanza yuko katikati ya topic ya 3 kati ya topic nane za form four.
Sasa ukitunga topic mtihani wa mock yenye swali la topic ya nne hadi ya nane kiukweli utakuwa hujui ni nini maana ya mtihani na hiki ndicho wanachokifanya hawa TAHOSA kwenye hii mitihani yao ya mock.
Wanatunga mtihani bila kuwa na guideline kwamba watunge wapi waishie wapi kama wenzao NECTA. Sijawahi kuona guideline yao ya utungaji wa mitihani.
Hii maana yake wote TAHOSA na walimu wote hapa nchini wanaipokea tu mitihani wanawatwisha watoto wetu wakati kumbe topi zenyewe hata hazijafikiwa.
TAHOSA na walimu wote hapa nchini hawapaswi kuwa wajinga kiwango hiki. Mtihani ni kipimo cha kupima alichjifunza mwanafunzi. Sasa unampa mtihani una maswali ambayo hajajifunza huo ni upimaji wa aina gani. Hiki ni kituko maana hakuna upimaji wa namna hiyo kokote duniani.
Hivyo, TAHOSA warekebishe hali yao kwa kufanyayafuatayo. Watoe guideline inayoeleza wazi kwamba mithiani yao ina cover kuanzia eneo fulani hadi fulani la syllabus.
Hili linatakiwa kuzingatia syllabus inasemaje kuhusu idadi ya vipindi katika kila somo na hivyo kufikia mwezi May itakwe wazi ni topic gani zinaletwa kwenye mock.
La sivyo, kama TAHOSA itaendelea hivi kuchomoa maswali hata ya topic za mwisho basi itaishia kuwa hina maana na mitihani ya mock itakosa heshima.