Mitihani ya kitaifa ya Ualimu kusahihishwa kidigitali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, leo Aprili 18, 2022 amekagua na kuridhishwa na majaribio ya Mfumo wa Kidijitali wa Usahihishaji Mitihani ya Kitaifa ya Ualimu ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na kujionea Mfumo huo unavyofanya kazi, Prof. Mkenda amesema kukamilika na kufanya kazi kwa mfumo huo kutasaidia Serikali kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika wakati wa usahihishaji wa mitihani ya kitaifa.

Waziri huyo amesema ameridhishwa pia kuona mafunzo kwa vitendo ya wasahishaji na wakaguzi wakati wa mchakato nzima wa usahihishaji wa mitihani na wahakiki wa ubora wa usahihishaji wake.
Mkenda.jpg

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) akifuatilia kwa makini namna Mfumo wa kidijitali unavyofanya kazi wakati wa ukaguzi wa majaribio ya usahihishaji mitihani kwa kutumia Mfumo huo yaliyofanyika katika ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania.

"Nimeambiwa Mfumo huu wa usahishaji mitihani ya Ualimu unatarajiwa kuanza rasmi kutumika mwaka huu kwa kusahihisha mitihani ya ualimu ya vyuo vyote na mwakani utaendelea katika hatua nyingiine ya kusahihisha mitihani ya kidato cha sita na tayari waalimu na wakaguzi wameandaliwa na kupatiwa vifaa husika," amesema Waziri Mkenda.

Mkenda amesema mfumo huo ni wa kwanza katika Afrika na umeandaliwa na vijana wa Kitanzania ambao ni wataalamu kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ambapo amesisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuiona NECTA inafanya shughuli zake zote kidijitali ifikapo 2025.

Waziri Mkenda ameongezea kuwa kwa kutumia mfumo huo Serikali itaokoa zaidi ya Shilingi bilioni 37 kila mwaka pamoja na kupunguza mlolongo mkubwa wa usahihishaji wa mitihani.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema wametengeneza mfumo huo kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita na maelekezo ya Waziri ya kuona namna bora ya kuandaa mifumo ya kijiditali ambayo inaweza kutumika katika kusahihisha mitihani pamoja na shughuli nyingine za Taasisi hiyo.

Dkt. Msonde amesema kuwa wataalamu wa TEHAMA wa Baraza hilo walianza kazi ambayo imeleta matokeo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ambayo unafanyiwa majaribio ili uweze kutumika kusahihisha mitihani ya Ualimu mwaka huu.

"Kwa Mfumo huu tunaendelea kufikia azma ya Wizara yetu ya kuwa na mifumo ili kuendesha shughuli zote kidigitali na kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita la kuwa na uchumi wa kidigitali na kwetu sisi tumeamua shughuli zote za mitihani kuwa za kidijitali ifikapo mwaka 2025," amefafanua Dkt. Msonde.

Chanzo: Malunde
 
Waziri wa elimu Prof Mkenda amesema mitihani ya kitaifa sasa itaanza kusahihishwa kidigitali ili kuwa na uhakika kwamba kila mwanafunzi anavuna alichopanda kwa haki kabisa.

Source: ITV habari
 
Naona hapo wanafunzi wanalazimishwa kukariri kwa namna fulani, lazima kwenye majibunya mitihani yao wahakikishe wanaandika exactly jibu lile walilofundishwa na mwalimu darasani.

Naamini hata wakiandika jibu walilosoma kwenye kitabu, kama vitabu viko tofauti, wakija na majibu tofauti kwenye swali lile lile wamefeli, atakaekuwa na jibu sahihi ni yupi hapa?

Masomo ya kujieleza sio kama hesabu, mwalimu ndie anatakiwa aangalie uelewa wa mwanafunzi wake kwenye swali husika kupitia majibu yake, aone namna mwanafunzi wake alivyojibu, sio hesabu kila siku inajulikana 1 + 1=2 duniani kote.
 
Pongezi kwa NECTA kwa mafanikio hayo makubwa, hakika huo ni mfumo mzuri zaidi.
 
Naunga mkono hoja, Nina miaka zaidi ya 15 kwenye ualimu lakini sijawahi kwenda marking, bila mchongo huendi, Kuna mwalimu kaajiliwa nyuma yangu yeye keshaenda Mara tatu.

Hapa kituoni kwangu Kuna walimu wawili tu ,huwa wanaenda, Sasa unabaki kujiuliza Hawa walimu walisoma vyuo gani ambavyo viliwafanya wawe mahili katika kufanya marking ya mitihani!!?

Bora kukosa wote, kuliko keki ya taifa kuliwa kimchongo
 
Naunga mkono hoja, Nina miaka zaidi ya 15 kwenye ualimu lakini sijawahi kwenda marking, bila mchongo huendi, Kuna mwalimu kaajiliwa nyuma yangu yeye kehaenda Mara tatu.

Hapa kituoni kwangu Kuna walimu wawili tu huwa wanaenda, Sasa unabaki kujiuliza Hawa walimu walisoma vyuo gani ambavyo viliwafanya wawe mahili katika kufanya marking ya mitihani!!?

Bora kukosa wote, kuliko keki ya taifa kuliwa kimchongo
Hii ndo inaitwa "Unyama unyamani".
 
Kwa wenzetu hata mitihani hufanyika online tu ukimaliza kila kitu kiko calculated na matokeo yako unapata on the spot.

Hao waliokataa ni wapenda paperwork pia wanajua hapo watakosa per diem za kwenda kurundikana mwezi mmoja na ushee kufanya marking.
Kwetu lazima watafute mwanya wa kupiga
 
Kwa wenzetu hata mitihani hufanyika online tu ukimaliza kila kitu kiko calculated na matokeo yako unapata on the spot.

Hao waliokataa ni wapenda paperwork pia wanajua hapo watakosa per diem za kwenda kurundikana mwezi mmoja na ushee kufanya marking.
Yes, Kuna siku nipo kwa mzungu hapahapa mkoani tumekaa nje kibarazani akaniambia mwanae yupo ndani anapiga Pepa la shule ipo UK.
 
Naunga mkono hoja, Nina miaka zaidi ya 15 kwenye ualimu lakini sijawahi kwenda marking, bila mchongo huendi, Kuna mwalimu kaajiliwa nyuma yangu yeye keshaenda Mara tatu.

Hapa kituoni kwangu Kuna walimu wawili tu ,huwa wanaenda, Sasa unabaki kujiuliza Hawa walimu walisoma vyuo gani ambavyo viliwafanya wawe mahili katika kufanya marking ya mitihani!!?

Bora kukosa wote, kuliko keki ya taifa kuliwa kimchongo
Fanyen kazi nje ya ualimu wakuu,haya majungu achaneni nayo.
 
Back
Top Bottom