Mitihani Katika Maisha

Darius RR

Member
Feb 5, 2019
21
75
Kwenu Wanafamilia wa JF

Ninatafuta kazi sehemu yoyote ndani ya nchi.

Kazi ninazoweza kuzifanya kutokana na uzoefu wa nilikopita kikazi na nilivyosoma:-
  • Uhasibu (Accountant/Finance Officer)
  • Afisa mikopo (Loans and credit analysis)
  • Ualimu wa masomo yafuatayo; Basic and Advanced Maths, Economics, Accounts na Geography
Hizo ni ambazo nina uzoefu nazo moja kwa moja, nina uwezo wa kufanya kazi nyingine yoyote ikiwa kama nimepata maelekezo na ni kazi ambayo siyo technical sana.

Brief Background:
Kampuni niliyokuwa nafanya kazi iliuzwa, wamiliki wapya wakapunguza wafanyakazi na kubadili uongozi, mimi ni moja ya waliopunguzwa.

Nimekuwa nikitafuta kazi kwa muda sasa lakini soko la ajira ni gumu, baadhi ya kazi nazikosa kwa kigezo kwamba ni low profile jobs, wanahisi sitakaa nao.

Ombi Kwenu:
Kwa yeyote mwenye nafasi ya kazi mahali alipo, au kuweza kusaidia kwa namna yoyote ile ninaomba msaada huo.

Maisha yamekuwa changamoto zaidi baada ya kibanda cha biashara nilichokuwa nafanya immediately baada ya kuacha kazi kubomolewa kwa sababu ya upanuzi wa barabara, hela ya kulipia frem mpya nikawa sina hivyo nikaamua kusukuma mzigo kwa hasara.

Sijakata tamaa bado ingawa maisha siyo rafiki kabisa katika kipindi kama hiki.

Shukrani kwenu.
 

cyrilah

Member
Dec 22, 2018
46
125
Kuna hotel mpya Arusha soon inaweza kufunguliwa ni five star inaitwa melia igugo alafu utume application zako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom