Mitihani inayowakabili wanawake: Unapopendwa pale usipopenda....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
ex-couple1.jpg

Linapokuja suala la kupenda kwa upande wa wanawake, kila mmoja anakuwa na vigezo vyake katika kumchagua mwenza hususan kwa sifa za nje. Inaweza kuwa ni maumbile ya mwili kwa maana ya unene, wembembe, urefu, ufupi au yaweza kuwa ni mtindo wa nywele kwa maana ya rasta, afro, nywele fupi zilizokatwa vizuri au yaweza kuwa mtindo wa kunyoa ndevu kwa maana ya kunyoa "O", kufuga mustachi au mzuzu kama beberu.

Kwa kifupi ni kwamba kila mwanamke anakuwa na uchaguzi wake mwenyewe anaouzingatia linapokuja suala la kuvutiwa na mwanaume anayempenda ambapo kama akikutana naye au akimuona… "Damn!" Moyo wake unamlipuka na anajikuta akitamani mwanaume huyo japo amsemeshe.

Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba, mapenzi ni kizungumkuti (Complex) hasa kwa wanawake kwa sababu hawana ujasiri wa kumtongoza mwanaume na kama akithubutu kufanya hivyo kibao kitamgeukia. Nani asiyejua kwamba mwanamke kujitongozesha kwa mwanaume ni kujitafutia muhali? Kwa mwanamke kujitongozesha au kujirahisisha kwa mwanaume ni kutaka kuwekwa katika kundi la malaya au kupewa thamani ya chini, labda tu kama mwanaume huyo atakuwa ana utambuzi wa hali ya juu na anajua thamani ya kupendwa.

Screen-shot-2013-11-06-at-7.21.26-AM-378x414.png

Lakini kama mwanaume ni hayawani basi atamfanyia mwanamke huyo vibweka kwa jinsi atakavyo na kama mwanamke akilalamika atamwambia… "Si ulijipendekeza mwenyewe, huna budi kuishi nitakavyo na kama hupendi au hutaki chapa lapa!"

Naam, hebu angalia sasa jinsi mambo yanavyokuwa ndivyo sivyo. Wakati mwanamke akiwa amejiwekea vigezo vyake katika kuchagua mwenza, haimaanishi kwamba, wanaume wanaokidhi vigezo hivyo wanavutiwa nao kama wanavyodhani, hususan wale wanaume wenye sifa za nje, ma handsome boy, wenye muonekano mzuri kwa nje (Good Personality) au masharobaro ambao kila mwanamke huvutiwa nao pale wawaonapo. Tatizo ni kwamba wanaume hawa wanajua kwamba wanawake wanawababaikia, hivyo nao wanakuwa hawajatulia, ni wanaume wachache sana, narudia tena wachache sana wenye sifa hizo za nje wanaojitambua na wanaojua thamani ya kupendwa.

couple-cheating.jpg

Binafsi nimeshawahi kukutana na hali kama hii, miaka ya nyuma sana wakati nikiwa nimedhamiria kutafuta mwenza baada ya mbilinge zangu za ujanani. Niliwahi kukutana na mwanamke mwenye sifa nizitakazo. Huyu kwangu alikuwa ni mwanamke wa ndoto zangu, nilimpenda kwa dhati na nilitumia mbinu mbalimbali ikiwemo fedha ili kumnasa, hakuonekana kunipenda na nilijikuta mimi nikiwa mtumwa wake. Mwishowe nilikubali matokeo nikachapa lapa ili kumpa nafasi au kuepusha msongamano.

Naamini wanawake wengi hukumbana na mtihani huu, ambapo mwanamke anakutana na mwanaume ambaye humtendea wema na kumuonyesha mapenzi ya dhati huku akimhudumia na kumchukulia kama malkia lakini kwa bahati mbaya mwanaume huyu masikini hakidhi viwango vyake, hana sifa (za nje) azitakazo na hata akimuona moyo wake haushtuki kabisa.

Lakini hata hivyo wapo baadhi ya wanawake pamoja na kwamba hawawapendi wanaume hawa huwatumia kuwachuna watakavyo bila hata ya chembe ya huruma, au kama mwanamke amefunzwa kwao, atamchukulia mwanaume huyu kama wa kupita tu kwa ajili ya mitoko na kula bata na sio wa kudumu naye.

Screen-shot-2013-10-03-at-10.30.12-PM.png

Labda sasa niwaulize wanawake, je unafanyaje unapokutana na hali kama hii? Je unaweza kumpa nafasi mwanaume huyu mwenye muafaka, yaani mwanaume anayeonekana kukujali na kukuthamini ingawa hujavutiwa naye? Je unaweza kubadili msimamo wako uliojiwekea? Au unaweza kujipa muda kusubiri mpaka pale atakapotokea mwanaume wa ndoto zako? Mwanaume ambaye ukimuona tu moyo wako unalipuka kwa mapenzi? (Lakini naamini wote mnajua jinsi jambo hilo lilivyogumu)

Naomba mtafakari………………
 
Mmmh! Binafsi ishanikuta hiyo..unakuta mwanaume anakupenda haswaaa mpaka unaona but kwakuwa hayupo moyoni unamua kujiweka mbali naye tena bila hata kutaka vitu vyake mana ni dhambi + kumpotezea muda!! Bora kumuacha ili akutane na atakayempenda.
 
Bora wewe unaogopa dhambi kuliko wale wanaosema, "Yule wala simpendi ila namchuna tu"

CC: Kongosho, Lisa, Nivea, MankaM, miss wa kinyaru, snowhite, Lady doctor, Preta, marejesho, gfsonwin, cacico, amu, Paloma, DEMBA, KOKUTONA, Heaven on Earth, miss chagga, Asnam, sister, tinna cute, Tina, Ennie,
 
Ujue mzee Mtambuzi ntakuchuna na ww usipoangalia....
 
Mhh kwa kweli will accept ONLY a man naempenda na anayenisisimua,naamini hata kwenye ndoa Mungu anapenda uwe na mume anaeku'drive crazy jmn,sasa usipomfeel hisia za ku'do nae zatoka wapiii,hata kutembea nae itakuwa mbinde nadhani
 
Akiwa na shekeli ntajitahidi kumpa nafasi mengine ntajua baadaye,hii mioyo wakati mwingine inabadili mwelekeo kadri siku zinavyoenda na ikitokea moyo haumdondokei mweh nakusanya vilivyo vyangu.
 
Aagh Mambo ya kusubiri mwanaume wa ndotoni sometimes yanagharimu,sijui nimsubirie mwenye mustachi,o,six pack Aaaagh ntazeekea nyumbani sasa,,,,,,,walahi akija anaeeleweka nafunika kombe mwanahizaya apite
 
Hapa umenigusa Mtambuzi, ilishanitokea mara mbili tofauti yaani kwa wanaume wawili tofauti, mwanaume anakupenda mpaka unaona kama kero vile kwa sababu wewe hayumo kwenye moyo wako, kuna mmoja nilikuwa namwambia kabisa kwamba asipoteze mda wake, lakini yumo tu, anatuma sms hujibu anapiga simu hupokei lakini hachoki, aisee nilipata shida sana, kuna wakati nikawa nasema Mungu nisaidie angalau nimpende hata kidogo kwani nilikuwa nikikutana nae sijui namuonaje jamani,. kweli hii ni mitihani
 
Kulikua hamna haja ya ku quote habari yote ndefu hii madam,unge reply tu wala utamu wetu usingetuharibia
 
ex-couple1.jpg

Linapokuja suala la kupenda kwa upande wa wanawake, kila mmoja anakuwa na vigezo vyake katika kumchagua mwenza hususan kwa sifa za nje. Inaweza kuwa ni maumbile ya mwili kwa maana ya unene, wembembe, urefu, ufupi au yaweza kuwa ni mtindo wa nywele kwa maana ya rasta, afro, nywele fupi zilizokatwa vizuri au yaweza kuwa mtindo wa kunyoa ndevu kwa maana ya kunyoa “O”, kufuga mustachi au mzuzu kama beberu.

Kwa kifupi ni kwamba kila mwanamke anakuwa na uchaguzi wake mwenyewe anaouzingatia linapokuja suala la kuvutiwa na mwanaume anayempenda ambapo kama akikutana naye au akimuona… “Damn!” Moyo wake unamlipuka na anajikuta akitamani mwanaume huyo japo amsemeshe.

Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba, mapenzi ni kizungumkuti (Complex) hasa kwa wanawake kwa sababu hawana ujasiri wa kumtongoza mwanaume na kama akithubutu kufanya hivyo kibao kitamgeukia. Nani asiyejua kwamba mwanamke kujitongozesha kwa mwanaume ni kujitafutia muhali? Kwa mwanamke kujitongozesha au kujirahisisha kwa mwanaume ni kutaka kuwekwa katika kundi la malaya au kupewa thamani ya chini, labda tu kama mwanaume huyo atakuwa ana utambuzi wa hali ya juu na anajua thamani ya kupendwa.

Screen-shot-2013-11-06-at-7.21.26-AM-378x414.png

Lakini kama mwanaume ni hayawani basi atamfanyia mwanamke huyo vibweka kwa jinsi atakavyo na kama mwanamke akilalamika atamwambia… “Si ulijipendekeza mwenyewe, huna budi kuishi nitakavyo na kama hupendi au hutaki chapa lapa!”

Naam, hebu angalia sasa jinsi mambo yanavyokuwa ndivyo sivyo. Wakati mwanamke akiwa amejiwekea vigezo vyake katika kuchagua mwenza, haimaanishi kwamba, wanaume wanaokidhi vigezo hivyo wanavutiwa nao kama wanavyodhani, hususan wale wanaume wenye sifa za nje, ma handsome boy, wenye muonekano mzuri kwa nje (Good Personality) au masharobaro ambao kila mwanamke huvutiwa nao pale wawaonapo. Tatizo ni kwamba wanaume hawa wanajua kwamba wanawake wanawababaikia, hivyo nao wanakuwa hawajatulia, ni wanaume wachache sana, narudia tena wachache sana wenye sifa hizo za nje wanaojitambua na wanaojua thamani ya kupendwa.

couple-cheating.jpg

Binafsi nimeshawahi kukutana na hali kama hii, miaka ya nyuma sana wakati nikiwa nimedhamiria kutafuta mwenza baada ya mbilinge zangu za ujanani. Niliwahi kukutana na mwanamke mwenye sifa nizitakazo. Huyu kwangu alikuwa ni mwanamke wa ndoto zangu, nilimpenda kwa dhati na nilitumia mbinu mbalimbali ikiwemo fedha ili kumnasa, hakuonekana kunipenda na nilijikuta mimi nikiwa mtumwa wake. Mwishowe nilikubali matokeo nikachapa lapa ili kumpa nafasi au kuepusha msongamano.

Naamini wanawake wengi hukumbana na mtihani huu, ambapo mwanamke anakutana na mwanaume ambaye humtendea wema na kumuonyesha mapenzi ya dhati huku akimhudumia na kumchukulia kama malkia lakini kwa bahati mbaya mwanaume huyu masikini hakidhi viwango vyake, hana sifa (za nje) azitakazo na hata akimuona moyo wake haushtuki kabisa.

Lakini hata hivyo wapo baadhi ya wanawake pamoja na kwamba hawawapendi wanaume hawa huwatumia kuwachuna watakavyo bila hata ya chembe ya huruma, au kama mwanamke amefunzwa kwao, atamchukulia mwanaume huyu kama wa kupita tu kwa ajili ya mitoko na kula bata na sio wa kudumu naye.

Screen-shot-2013-10-03-at-10.30.12-PM.png

Labda sasa niwaulize wanawake, je unafanyaje unapokutana na hali kama hii? Je unaweza kumpa nafasi mwanaume huyu mwenye muafaka, yaani mwanaume anayeonekana kukujali na kukuthamini ingawa hujavutiwa naye? Je unaweza kubadili msimamo wako uliojiwekea? Au unaweza kujipa muda kusubiri mpaka pale atakapotokea mwanaume wa ndoto zako? Mwanaume ambaye ukimuona tu moyo wako unalipuka kwa mapenzi? (Lakini naamini wote mnajua jinsi jambo hilo lilivyogumu)

Naomba mtafakari………………

ni ngumu haswa.....kuna wakati huruma sijui inaenda wap......maskin dhambi izi.......Mungu nirehemu mim
 
hapa umenigusa mtambuzi, ilishanitokea mara mbili tofauti yaani kwa wanaume wawili tofauti, mwanaume anakupenda mpaka unaona kama kero vile kwa sababu wewe hayumo kwenye moyo wako, kuna mmoja nilikuwa namwambia kabisa kwamba asipoteze mda wake, lakini yumo tu, anatuma sms hujibu anapiga simu hupokei lakini hachoki, aisee nilipata shida sana, kuna wakati nikawa nasema mungu nisaidie angalau nimpende hata kidogo kwani nilikuwa nikikutana nae sijui namuonaje jamani,. Kweli hii ni mitihani

kwa hiyo ndio umeamua uje kunisemelea huku jf sio...poa tuu yote maisha ila naamini ipo siku utanipenda tuu...lazma niongeze kutafuta "modern ladies best friends" cash money...mpaka utaomba poo...nakupa mwaka mmoja coz next year nitakuwa pazuri sana ndani ya team el tena.... Only time will tell.
 
Bora wewe unaogopa dhambi kuliko wale wanaosema, "Yule wala simpendi ila namchuna tu"

CC: Kongosho, Lisa, Nivea, MankaM, miss wa kinyaru, snowhite, Lady doctor, Preta, marejesho, gfsonwin, cacico, amu, Paloma, DEMBA, KOKUTONA, Heaven on Earth, miss chagga, Asnam, sister, tinna cute, Tina, Ennie,
Unajua nini Mtambuzi, Unaweza ukamwambia mwanaume kwamba humpendi lakini akakwambia naomba unikubalie tu hivyo hivyo maana nakupenda sana nateseka juu yako na ukimwangalia ni kweli anakupenda sana, so unaamua kuwa nae ili kumfurahisha na wewe kitakachokufurahisha ni pesa zake na si kingine maana huna mapenzi nae, ila hapo akubali kuwa mtumwa wa mapenzi kwani inabidi afanye unavyotaka wewe.
 
Ni vigumu sn kumpata MTU mnaependana saw saw.nin kwel kika MTU ana vgezo vyake anataka mwenzi wake aweje lkn nadhani nin vizur jutoongozwa na hisia za mwili turn kwan love na has a mwenzi wa maisha nin zaid ya feelings za nje.hii imekost watu wengi sn kwenye ndoa...ulipenda unene sasa amekuwa mwembamba unamwona wa nin tena nk.mm niliwah kupendwa sn na kijana mmoja wakati huo niko form four,ckumpenda wala kuvutiwa naye kabsa.nilimtesa wa miaka miwili baadae nilimwambia ukweli.aliumia sn lkn alikubaliana na mimi na ananipenda mpaka Leo kwakuwa nilimwambia ukweli.kuwa napokea chochote kutoka kwake.wanaume pia mnakosea,MTU hawez kukupenda kwa kumwaga mahela love inatoka moyon hainunuliwa mtambuzi.UK Iona mwanamke anaependa sn kupokea jiulize Mara nyingi hakuna upendo wa dhati hapo Mzee unaliwa.MTU akikupenda atakuthamini na Kuwa ma huruma juu yako cyo Kuchuna mpaka ngoz.
 
Na wenyewe wana matatizo,wakionyeshwa red alerts hawaelewi ngoja wachunwe hadi ngozi kabisa ili wausikilizie utamu
 
Aagh Mambo ya kusubiri mwanaume wa ndotoni sometimes yanagharimu,sijui nimsubirie mwenye mustachi,o,six pack Aaaagh ntazeekea nyumbani sasa,,,,,,,walahi akija anaeeleweka nafunika kombe mwanahizaya apite

Hahaha. Nimeipenda sana hii Asnam. Yani umeongea straight from the heart! Kwani samahani kuuliza because true gentleman never ask a womans age ila wewe una umri gani?
 
Na wenyewe wana matatizo,wakionyeshwa red alerts hawaelewi ngoja wachunwe hadi ngozi kabisa ili wausikilizie utamu

Kweli binadamu hatuchelewi kusahau,umeyasahau mara hii ya ufoo na Mushi?
Kwanini usijiondoe mapema kabla tatizo halijatunga mimba?
 
Mtambuzi acha tu...huu mtihani siutaki tena Mungu anijalie kilicho changu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom