Mitihani ifanyike na matokeo yatolewe huku.......

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
[h=6]Nashauri mitihani ya masomo ya dini isahihishwe huko huko misikitini na makanisani na wawekeane maksi watakazo kama ni 100% sawa kama ni 0% poa pia matokeo wapeane hukohuko ktk nyumba za ibada.Maana Sioni faida yake kuwa chini ya Baraza la Mitihani la Tanzania Wakati ni somo lao na Mungu wao.Tutilie maanani kuwa Serikali ya Tanzania haina dini.

Ama mwaonaje hili wadau
[/h][h=6]:target:[/h]
 
Naona umekurupuka. Nchi zote duniani zina mitaala ya masomo ya dini pia kuna vyuo vikuu vingi sana duniani vinavyotoa shahada za masomo ya dini. Baraza la mitihani lipo kwa mujibu wa sheria hivyo kuwezesha matokeo ya masomo ya dini kutambuliwa kisheria. Sasa mitihani ya dini ikisahihishiwa kwenye nyumba za ibada matokeo yatakuwa hayana maana sana.
 
Nashauri mitihani ya masomo ya dini isahihishwe huko huko misikitini na makanisani na wawekeane maksi watakazo kama ni 100% sawa kama ni 0% poa pia matokeo wapeane hukohuko ktk nyumba za ibada.Maana Sioni faida yake kuwa chini ya Baraza la Mitihani la Tanzania Wakati ni somo lao na Mungu wao.Tutilie maanani kuwa Serikali ya Tanzania haina dini.

Ama mwaonaje hili wadau


:target:
Tatizo ni ufelishwaji wa makusudi kwa wanafunzi wa Kiislamu sio usahihishaji! soma vizuri madai yaliyoandikwa na Mufti Simba.
Somo la Kiislamu ilikuwa ni kama "bahati mbaya" tu kwa NECTA kugundulika, yaangaliwe na masomo mengine.
Ushauri wako ungeeleweka tu kama ungelenga kuliengua baraza la mitihani, kuboresha mfumo mzima unaotumika na makatili wote waliohusika na hiyana hii ya kuwanyima watoto wa Kiislamu elimu miaka kwa miaka wachukuliwe hatua.
Vinginevyo inaonyesha kama vile machungu na maumivu ya ufelishwaji hayajawahi kukukuta!
 
Back
Top Bottom