Mitihani hii ya maisha

Mitihani hii ya maisha

Hardwaycomes

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2018
Posts
370
Reaction score
494
Nina 50,000 tu ghafla nimepokea taarifa tatu zote zinataka pesa, nitoe kwa nani na nimuache nani?

1. Mama mzazi anahitaji pesa aweze kuhudhuria msiba wa mke wa kaka yake

2. Mtoto wangu anatakiwa kulipiwa nauli ya shule (school bus),muda umefika

3. Ninamsomesha mtoto wa kaka yangu (alishafariki) hivyo nilibeba jukumu la kumsomesha kuyajenga maisha yake, anaumwa na amelazwa hana pesa ya matumizi

Nitatue lipi na niache lipi?
 
Okoa uhai kwanza mengine baadae!

No. 3
 
No 3 ndio muhimu sana uhai wa mtu muhimu sana
 
Iyo mbona rahisi Sana.Namba3,2,1sio muhimu Sana nawala haina dhambi....kufa ni faradhih na kuuzulia mazsh nisunah.okoa uhai wamtu Kwanza maana ugonjwa nisunah ila matibabu nifaradhi ata Kama ungekuwa haujaachiwa nandugu yako kwakua nbnadamu mwenzio inakulazmu kumsaidia
 
Nina 50,000 tu ghafla nimepokea taarifa tatu zote zinataka pesa, nitoe kwa nani na nimuache nani?

1. Mama mzazi anahitaji pesa aweze kuhudhuria msiba wa mke wa kaka yake

2. Mtoto wangu anatakiwa kulipiwa nauli ya shule (school bus),muda umefika

3. Ninamsomesha mtoto wa kaka yangu (alishafariki) hivyo nilibeba jukumu la kumsomesha kuyajenga maisha yake, anaumwa na amelazwa hana pesa ya matumizi

Nitatue lipi na niache lipi?
Kaka mbona jibu ni rahisi saan. Hapo pitia comment za watu then fanya wengi wape🙏
 
Tatua ufinyu wa vyanzo vyako vya mapato.

Wakati mwingine matatizo mengi yangeweza kutatuliwa bila kuonyesha lipi tatizo muhimu kuliko lingine.

Maisha yanahitaji suluhisho (kutatua matatizo).
 
Okoa uhai wa mgonjwa then hayo mengine yatafuata tu....
 
Mbona 50 hela ya kutosha kabisa mkuu. Anza na 3. Inategemeana ni kiasi gani anataka. Unaweza kujiumiza kichwa kumbe wanataka 20000 tu kwanza. Mother mpe 20. Wewe bakia na ten. School kwa mtoto kawapange tu,utawapa katikati ya wiki hii. Pole
 
Hapo cmple tuu.
Maza anaambiwa ukwe tu bila shaka ataelewa.

Wenye shule yao wanapigwa sound tu hakuna namna.Waki mind basi dogo anabaki nyumban au kama vp house girl atampeleka kwa daladala.

Komaa na mgonjwa hiyo ndio no. 1
 
Back
Top Bottom