Mitihani gani kama hii...!

Mitihani gani kama hii...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
540x293_20140115_46cf80720f70bddb96dbeff78a9a66d3_jpg.jpg

Alikuwa akisafiri kwenye barabara kuu akiwa juu ya pikipiki yake. Alikuwa akiendesha kwa wastani wa kilimeta 65 kwa saa. Jambo lenyewe lilitokea ghafla sana. Aligeuka kutazama pembeni mwa barabara na aliporudisha macho barabarani, gari kubwa la mizigo lililokuwa mbele yake lilikuwa limesimama ghafla.

Ilikuwa ni ghafla mno kiasi kwamba hata akili kufikiri ilikuwa ngumu sana. Kwa kutaka tu kuokoa maisha yake mawazo ya nguvu za mwisho yalimjia ambapo aliangusha pikipiki na kuburuzika chini ya gari hilo. Wakati akiburuzika, kifuniko cha tangi la mafuta la pikipiki yake kilifunuka na jambo baya lilitokea.

Moto ulilipuka akiwa bado anaburuzika chini ya gari hilo. Anachokumbuka baada ya hapo ni kupata fahamu wakati akiwa hospitalini. Alikuwa ameungua karibu mwili wote kwa kiwango ambacho hata kupona ilionekana ni suala la Mungu mwenyewe. Lakini yeye hakukata tamaa katu. Alisema kwamba anataka kupona na kwamba ni lazima angepona.

Alipona na kuanza shughuli zake za biashara kama vile hakuwa amepatikana na ajali ile mbaya. Lakini haikuchukua muda kabla hajapambana na kisirani kingine cha maisha. Ilikuwa ni wakati wa safari zake za kibiashara, ambapo ndege aliyokuwa akisafiri nayo ilianguka naye akaponea chupuchupu. Lakini akalemaa kuanzia kiuno kwenda chini. Hakukata tamaa. Alisema anataka kuishi na siyo kuishi tu bali kuishi kwa mafanikio. Alipopona alirudi katika biashara zake kama vile hakukuwa kumetokea jambo lolote baya au la kuvunja nguvu.

Huyu siye mwingine bali ni mfanyabiashara maarufu sana kule Colorado nchini Marekani, William Mitchel, ambaye baada ya mitihani hii mikubwa ya kimaisha alipata ari mpya ya kutafuta mafanikio maishani. Aliendelea kufanya biashara huku akiwa na makovu na ulemavu hadi akafanikiwa kuingia kwenye orodha ya mamilionea wa Marekani.

Bila shaka unafahamu kwamba kwenye maisha huwa tunapitia hatua mbalimbali za mabadiliko kutoka mafanikio kwenda maanguko au kinyume chake na kutoka faraja kwenda visirani au kinyume chake. Kila mmoja wetu ana njia ambayo huchukulia mabadiliko haya. Kuna wakati ambapo huwa tunasema tunajaribiwa, tunapewa mitihani na mungu. Hali hii iko duniani kote na kwa kila binadamu kutegemea tu mazingira ya mitihani hiyo. Wakati huu ni ule ambapo kila tulicho nacho kama ulinzi wetu hujaribiwa. Huu ni wakati ambapo huwa tunayatazama maisha kama yasiyo na haki na yanayoonea au kutazama upande mmoja.

Hiki ni kipindi ambapo imani zetu, thamani ya utu wetu, viwango vya subira zetu na uwezo wa kujizatiti hufikishwa kwenye ukomo, ambao tunadhani hatuwezi tena kuwa na vitu hivyo. Kwa baadhi ya watu, hutumia vipindi kama hivi vya mitihani ya maisha kuwa watu bora zaidi, wakati wengine hutumia vipindi hivi kukata tamaa na kuharibu kabisa maisha yao. Je umeshawahi kujiuliza maishani mwako ni kwa nini baadhi ya watu hutumia mitihani ya maisha kufanikiwa na wengine huitumia kwa kuanguka kabisa maishani?

Ukweli ni kwamba siyo kuwa watu walifanikiwa hawana au hawakupitia mitihani katika maisha, tena huenda wamepitia mitihani mizito kuliko wale ambao hawana mafanikio maishani mwao. Mahali ambapo hakuna matatizo ni kaburini tu, lakini kwenye maisha matatizo ni lazima kwa yeyote.

Kama Mitchel alivyoungua mwili mzima, ilikuwa ni juu yake kuamua kuhusu tukio hilo. Kama angeamua kwamba kuungua kule ulikuwa mwisho wa maisha , mwisho wa kutafuta mafanikio, bila shaka angefia hospitalini au hata kama angepona, angebaki mtaani kuombaomba. Lakini kwake kuungua kule kulikuwa ni changamoto katika kutafuta maana halisi ya maisha. Alijiambia kwamba, mtihani ule wa kuungua haukuwa umempata tu kwa sababu ya kumpata, bali kulikuwa na maana kubwa, kusudi maalum kubwa. Kusudi ambalo linalenga kwenye kubadili maisha yake kwa mafanikio makubwa zaidi.

Ni wangapi kati yetu ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huchukulia mitihani hiyo kama mwisho wa maisha yao. Huanza kuchanganyikiwa na hata kuamua kujiuwa? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huanza kuwanyooshea kidole wengine kwamba ndio wamewasababishia matatizo hayo kwa kuwaloga au kwa njia nyingine? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huamua kuingia katika ulevi ili kupoteza mawazo? Bila shaka ni wengi, wengi, wengi sana, pengine ukiwemo na wewe…………….

CC:
Eiyer, Ennie, charminglady, MankaM, Munkari, Tina, miss chagga, miss neddy, lara 1, Neylu, FaizaFoxy, EMT, BAK, Ruttashobolwa, Kaizer, Nyani Ngabu, The Boss, Kiranga, Chocs, Preta, marejesho, MwanajamiiOne, AshaDii, King'asti, Husninyo, snowhite, Fixed Point
 
[h=2]Motivational Story About W.Mitchell On Overcoming Adversity[/h]"What if at age 46 you were burned beyond recognition in a terrible motorcycle accident, and then four years later were paralyzed from the waist down in an airplane crash? Then, can you imagine yourself becoming a millionaire, a respected public speaker, a happy newlywed and a successful business person? Can you see yourself whit e water rafting? Sky diving? Running for political office?

W. Mitchell has done all these things and more after two horrible accidents left his face a quilt of multicolored skin grafts, his hands fingerless and his legs thin and motionless in a wheelchair.

The 16 surgeries Mitchell endured after motorcycle accident burned more than 65 percent of his body, left him unable to pick up a fork, dial a telephone or go to the bathroom without help. But Mitchell, a former Marine, never believed he was defeated. "I am in charge of my own spaceship," he said. "It's my up, my down. I could choose to see this situation as a setback or a starting point." Six months later he was piloting a plane again.

Mitchell bought himself a Victorian home in Colorado, some real estate, a plane and a bar. Later he teamed up with two friends and co-founded a wood-burning stove company that grew to be Vermont's second largest private employer.
Then four years after the motorcycle accident, the plane Mitchell was piloting crashed back onto the runway during takeoff, crushing Mitchell's 12 thoratic vertebra and permanently paralyzing him from the waist down. "I wondered what the hell was happening to me. What did I do to deserve this?"

Undaunted, Mitchell worked day and night to regain as much independence as possible. He was elected Mayor of Crested Butte, Colorado, to save the town from mineral mining that would ruin its beauty and environment. Mitchell later ran for Congress, turning his odd appearance into an asset with slogans such as, "Not just another pretty face."
Despite his initially shocking looks and physical challenges, Mitchell began white water rafting, he fell in love and married, earned a master's degree in public administration and continued flying, environmental activism and public speaking.

Mitchell's unshakable Positive Mental Attitude has earned him appearances on the "Today Show" and "Good Morning America" as well as feature articles in Parade, Time, The New York Times and other publications.

"Before I was paralyzed, there were 10,000 things I could do," Mitchell says. "Now there are 9,000. I can either dwell on the 1,000 I lost or focus on the 9,000 I have left. I tell people that I have had two big bumps in my life. If I have chosen not to use them as an excuse to quit, then maybe some of the experiences you are having which are pulling you back can be put into a new perspective." You can step back, take a wider view and have a chance to say, "Maybe that isn't such a big deal after all."

Remember: "It's not what happens to you, it's what you do about it."

Motivational Story About W.Mitchell On Overcoming Adversity
 
Water can never sink the ship,unless it enters
 
uwiiiii mim sijui kama ningekuwa hai looo!!! mungu ni wa ajabu
 
Safi! Mtazamo chanya juu ya maisha
When life gives you lemons...make lemonade! 🙂🙂🙂
Nimeipenda hii ...........

When life gives you lemons...make lemonade!
 
Mtambuzi heshima yako.Mbona hujaniita kwenye huu uzi mkuu
Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kukata tamaa. Ukikata tamaa na kila kinachokuzunguka kinakata tamaa. Ukiwa unajenga nyumba na ukakata tamaa kuwa hutaimaliza na kweli hiyo nyumba itakuwa gofu kwako hutaimaliza. majaribu naamini ni sehem ya maisha na unapopatwa na jaribu lolote hata liwe baya kiasi gani ni mwanzo mpya wa kusonga mbele bila jeraha la moyo wala kukata tamaa.
 
Last edited by a moderator:

Kaka niwie radhi niliku overlook.
Naamini umepata busara za jioni.............
 
Pamoja sana mkuu Mtambuzi
Nimepata busara za jioni na ujumbe murua kabisa ambao ni muhimu sana kwamaisha ya sasa mkuu ambapo tunapitia mitihani mingi sana ya maisha
 
Last edited by a moderator:
Ujumbe mzuri sana,matatizo yetu yanatakiwa yawe ngazi yakupandia juu.
 
Ni kwa Neema tu!
Ee Mungu nipe ujasiri wa kusimama tena niangukapo.
Ninavyojijua mie nilivyo,nisingeinuka baada ya kuungua ajalini!!
Mungu anakupa mtihani unaouweza,alijua anaweza ndio maana akampitisha mapito yote hayo.
 
somo zuri sana Mtambuzi katika hawakati tamaa kirahisi ni mimi
hakuna mafanikio yasiyo na misukosuko
 
Last edited by a moderator:
somo zuri sana Mtambuzi katika hawakati tamaa kirahisi ni mimi
hakuna mafanikio yasiyo na misukosuko

Nakujua sana miss neddy uko hivyo ila naogopa kukusifu maana wahafidhina hawakawii kunizulia kwamba ni mbinu zangu za kukutongoza..... LOL
 
Last edited by a moderator:
540x293_20140115_46cf80720f70bddb96dbeff78a9a66d3_jpg.jpg

Alikuwa akisafiri kwenye barabara kuu akiwa juu ya pikipiki yake. Alikuwa akiendesha kwa wastani wa kilimeta 65 kwa saa. Jambo lenyewe lilitokea ghafla sana. Aligeuka kutazama pembeni mwa barabara na aliporudisha macho barabarani, gari kubwa la mizigo lililokuwa mbele yake lilikuwa limesimama ghafla.

Ilikuwa ni ghafla mno kiasi kwamba hata akili kufikiri ilikuwa ngumu sana. Kwa kutaka tu kuokoa maisha yake mawazo ya nguvu za mwisho yalimjia ambapo aliangusha pikipiki na kuburuzika chini ya gari hilo. Wakati akiburuzika, kifuniko cha tangi la mafuta la pikipiki yake kilifunuka na jambo baya lilitokea.

Moto ulilipuka akiwa bado anaburuzika chini ya gari hilo. Anachokumbuka baada ya hapo ni kupata fahamu wakati akiwa hospitalini. Alikuwa ameungua karibu mwili wote kwa kiwango ambacho hata kupona ilionekana ni suala la Mungu mwenyewe. Lakini yeye hakukata tamaa katu. Alisema kwamba anataka kupona na kwamba ni lazima angepona.

Alipona na kuanza shughuli zake za biashara kama vile hakuwa amepatikana na ajali ile mbaya. Lakini haikuchukua muda kabla hajapambana na kisirani kingine cha maisha. Ilikuwa ni wakati wa safari zake za kibiashara, ambapo ndege aliyokuwa akisafiri nayo ilianguka naye akaponea chupuchupu. Lakini akalemaa kuanzia kiuno kwenda chini. Hakukata tamaa. Alisema anataka kuishi na siyo kuishi tu bali kuishi kwa mafanikio. Alipopona alirudi katika biashara zake kama vile hakukuwa kumetokea jambo lolote baya au la kuvunja nguvu.

Huyu siye mwingine bali ni mfanyabiashara maarufu sana kule Colorado nchini Marekani, William Mitchel, ambaye baada ya mitihani hii mikubwa ya kimaisha alipata ari mpya ya kutafuta mafanikio maishani. Aliendelea kufanya biashara huku akiwa na makovu na ulemavu hadi akafanikiwa kuingia kwenye orodha ya mamilionea wa Marekani.

Bila shaka unafahamu kwamba kwenye maisha huwa tunapitia hatua mbalimbali za mabadiliko kutoka mafanikio kwenda maanguko au kinyume chake na kutoka faraja kwenda visirani au kinyume chake. Kila mmoja wetu ana njia ambayo huchukulia mabadiliko haya. Kuna wakati ambapo huwa tunasema tunajaribiwa, tunapewa mitihani na mungu. Hali hii iko duniani kote na kwa kila binadamu kutegemea tu mazingira ya mitihani hiyo. Wakati huu ni ule ambapo kila tulicho nacho kama ulinzi wetu hujaribiwa. Huu ni wakati ambapo huwa tunayatazama maisha kama yasiyo na haki na yanayoonea au kutazama upande mmoja.

Hiki ni kipindi ambapo imani zetu, thamani ya utu wetu, viwango vya subira zetu na uwezo wa kujizatiti hufikishwa kwenye ukomo, ambao tunadhani hatuwezi tena kuwa na vitu hivyo. Kwa baadhi ya watu, hutumia vipindi kama hivi vya mitihani ya maisha kuwa watu bora zaidi, wakati wengine hutumia vipindi hivi kukata tamaa na kuharibu kabisa maisha yao. Je umeshawahi kujiuliza maishani mwako ni kwa nini baadhi ya watu hutumia mitihani ya maisha kufanikiwa na wengine huitumia kwa kuanguka kabisa maishani?

Ukweli ni kwamba siyo kuwa watu walifanikiwa hawana au hawakupitia mitihani katika maisha, tena huenda wamepitia mitihani mizito kuliko wale ambao hawana mafanikio maishani mwao. Mahali ambapo hakuna matatizo ni kaburini tu, lakini kwenye maisha matatizo ni lazima kwa yeyote.

Kama Mitchel alivyoungua mwili mzima, ilikuwa ni juu yake kuamua kuhusu tukio hilo. Kama angeamua kwamba kuungua kule ulikuwa mwisho wa maisha , mwisho wa kutafuta mafanikio, bila shaka angefia hospitalini au hata kama angepona, angebaki mtaani kuombaomba. Lakini kwake kuungua kule kulikuwa ni changamoto katika kutafuta maana halisi ya maisha. Alijiambia kwamba, mtihani ule wa kuungua haukuwa umempata tu kwa sababu ya kumpata, bali kulikuwa na maana kubwa, kusudi maalum kubwa. Kusudi ambalo linalenga kwenye kubadili maisha yake kwa mafanikio makubwa zaidi.

Ni wangapi kati yetu ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huchukulia mitihani hiyo kama mwisho wa maisha yao. Huanza kuchanganyikiwa na hata kuamua kujiuwa? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huanza kuwanyooshea kidole wengine kwamba ndio wamewasababishia matatizo hayo kwa kuwaloga au kwa njia nyingine? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huamua kuingia katika ulevi ili kupoteza mawazo? Bila shaka ni wengi, wengi, wengi sana, pengine ukiwemo na wewe…………….

CC:
Eiyer, Ennie, charminglady, MankaM, Munkari, Tina, miss chagga, miss neddy, lara 1, Neylu, FaizaFoxy, EMT, BAK, Ruttashobolwa, Kaizer, Nyani Ngabu, The Boss, Kiranga, Chocs, Preta, marejesho, MwanajamiiOne, AshaDii, King'asti, Husninyo, snowhite, Fixed Point

Nguvu ya kunia haiwezi kushindwa na chochote na maisha bila changamoto yanakuwa kama hayana maana vile, ni lazima tukutane na changamoto na tumiize akili kuzikabili na kuzitatua ndio akili hupanuka na kukua zaidi
Hii topic ni kichocheo chanya chenye kuleta chagizo la matumaini na faraja kwa wale walio kwenye shida na waliokata tamaa!!!
 
Last edited by a moderator:
Nakujua sana miss neddy uko hivyo ila naogopa kukusifu maana wahafidhina hawakawii kunizulia kwamba ni mbinu zangu za kukutongoza..... LOL

hahahaha baba ngina si unawajua vijana wa dot com wakiona unawazidi mbio hawakosi visingizio lol
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom