Miti shamba/mizizi ina nguvu katika mapenzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miti shamba/mizizi ina nguvu katika mapenzi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Apr 14, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kuna uvumi mwingi sana wakutumia mizizi katika mapenzi? Wapo wengine wana imani kuwa akitumia mizizi anaweza akampata kwa mfano hata mke wa mtu au mpenzi wa mtu kama Nyamayao au Belinda au Mwanajamii......je ni kweli hizi dawa zinafanya kazi na zinauwezo wakukushawishi ukubaliane na matakwa ya huyu mtu katika mapenzi na ukampenda gafla?

  Lipo tena jambo jingine wapo watu wanawake na wanaume wanao wapumbaza waume au wake zao anakuwa haongei kitu mtu mmoja katika familia anakuwa na kibezi anasauti na ndo mwenye maamuzi inasemekana iwa wanalishwa limbwata kwa hiyo mwanaume au mwanamke anakuwa amenywea mpaka watu walio nje na ile familia wanaona kama yule mama au baba kama anaonewa kama ni mwanaume kafanyiwa mzizi mwanamke anaweza akawa anarudi muda anaotaka usiku na kumwachia majukumu yote ya pale nyumbani na mwanaume haongei kitu .

  Ndugu zangu hii mizizi ina nafasi katika mapenzi?
  Je mizizi au mitishamba ina nafasi kubwa katika ulingo wa mapenzi?
  Karibuni nyote tuchangie.

  Fidel80
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  HILI SWALA LIPO SANA,tena sana.na mifano ninayo.msure wangu mdogo mimi kaoa mburu,ANACHANGANYIWAGA MADAWA iliaendelee kumpenda mwanamke,dawa zikiisha HUWA PANACHIMBIKA,hutakaa uamini.  je ni kweli hizi dawa zinafanya kazi na zinauwezo wakukushawishi ukubaliane na matakwa ya huyu mtu katika mapenzi na ukampenda gafla?

  KAKA HII MIFANO NDIO YENYEWE!na kwa mujibu wa thread yako,dada zangu hawa wanaweza kutusaidia sana juu ya hili,maana hili jukwaa NI LAO  MIZIZI INAHUSIKA,na wamasai wengi mizizi INAWAWEKA MJINI.kuna imani kuwa wamasai ndio wataalamu wa dawa za malavidavi,na ma kila kitu.

  ANGALIZO:Hizi dawa ZINA MWISHO WAKE!tena huwa m baya.ni kama kutumia dawa kutafuta utajiri,waulize wakinga watakwambia,anapewa dawa AWE TAJIRI kwa miaka mitano,then ANAKUFA watoto wanaendelea kula bata kitaa,kama hawakusoma NDO HIVYO WANAFUJA MALI HADI COIN YA MWISHO
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi nasubili tu akina Nyamayao,Belinda,Mwanajamii,WOS,Masanilo na wengineo ni kweli mizizi inanguvu katika maswala ya mapenzi?
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Yote ni imani ya mtu tu.Unaweza kupenda au kupendwa kisawasawa bila kuongezea mzizi wala hirizi.Ila inasemekana kuna visaidizi kama alivyosema dgeouf hapo juu kuwa katika makabila mbalimbali au jamii fulani kuna hivyo vitu.Limbwata ni kitu kinaongelewa sana, halafu kuna kifafii ( kwa wambulu),n.k na wako watu - sijui kuhusu wanaume lakini miongoni mwa wanawake wanaamini huwezi kupendwa bila dawa.Na kwa sasa wapo wanaosafiri hadi Nigeria kununua dawa hizo za kuwatight wanaume siyo kwa mapenzi bali waweze kuwachuna pesa zao.Hivyo kina baba/kaka wenye kuonjaonja bila mpango kaeni chonjo mtageuzwa misukule.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145

  Kwa hiyo kama mwanaume alikuwa mkali sana akinyweshwa dawa au mzizi bila yeye kujua anaanza kunywea gafla anakuwa mdogo ndani ya nyumba?
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  EE BWANA EEHH!
  ulivyouliza ni kama umesikia kuwa nimewahi kuona unyweshaji huo na effectiveness yake.
  Kwa kweli sijui, labda tusubiri kama kuna mwenye ushahidi atujuze.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  WOS ngoja tusubuli sasa.....
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dawa za mitishamba zipo tena sana na mara nyingi watu wanaotumia hizi dawa huwa hawajiamini kama ni wanawake au wanaume.
  Na wanawake wengine huwa wanawawekea wanaume wao ambao hawajatulia ili waache ukicheche wa kuwa na wanawake wengi.
  Ila tatizo la hizi dawa huwa zinaisha nguvu mapema yani unatakiwa uwe una renew kila baada ya muda mfano miezi mitatu, sasa hapo usipokuwa mwangalifu ikaisha muda labda ulijisahau utajuta kuzaliwa hali inakuwa mbaya muhusika anabadilika anakuwa mbaya kuliko alivyokuwa mwanzo kwa hiyo utaishi maisha ya wasiwasi.na makabila mengi ya kiafrika yanatumia siyo kula tu, kuoga, aruke mlangoni, kuweka chini ya kitanda anabanwa kila kona ya nyumba atakayoingia hata ofisini kwake ukiweza kuweka unaweka.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Nimeambiwa hapa madhara ya madawa haya yakichuja basi kwisha kazi mtu anabumbuluka ugomvi kila siku hauishi.........
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Nimeshawahi kusikia pia baadhi ya wanawake wa kibongo walio majuu hurudi Bongo kutafuta miti shamba maana mapenzi ya waume zao yanaonekana kupungua!!! Nilishangaa sana lakini ndiyo hivyo tena watu wengine watafanya lolote kwa ajili ya mapenzi
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Desperately searching for love!

  Ziko stori za kutisha on this subject ila si vizuri kuzizungumzia hapa.
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kama alivyosema WOS, hivi vitu vinaendana na imani yako, mfano hai ni kwangu wakati ilipokwaruzana na mr kuna baadhi ya watu wangu wa karibu waliniambia/kunishauri kivyake, mmoja akaniambia mimi nimezidi kuzubaa mjini hapa nitampoteza mume hivi hivi najiona so anipeleke mahali fulani nikatengenezewe dawa ili mr a2lie na acweze kutoka nje daima, iwe ni mimi tu,..akaniambia wadada/wamama ndivyo wanavyoishi mjini cku hizi ukimpata buzi/mchumba kinachofatia ni kumweka "sawa", nilibisha/kugoma kabisa nikamwambia kama alinipenda jinsi nilivyo na kwa imani yangu haya ni majaribu tu yana mwisho wake, alinijibu kwamba mie nimezidi kuzabaa sana., huyu mdada kuna wakati alikorofishana na mr wake akarudi kwao kwa muda kidogo,kipindi kdgo akackia mr ana mwanamke mwingine, alikuwa na safari za kila leo mara naenda cjui rombo nimeambiwa kuna baba mmoja anajua dawa sana, mara naenda wapi na wapi mpaka huyu mwanamke anikome/anijue mimi sio wa kuchezea, hakuna kilichosaidia na mwanaume akamuoa huyo mdada mwingine, ma frnd mpaka kesho ni kuzunguka na safari kwenda kutafuta dawa zenye makali zaidi, hiyo ndio imani yake kwamba huyo mwanamke mwingine ka2mia madawa kumteka mume wake na ana imani kuna cku mume atamrudia tu mana ametekwa na madawa....kila mtu ana imani yake juu ya haya mambo.
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  huyo frnd wangu mie mpaka nikawa namuuliza mbona kama unamu over dose sana mumeo wewe?coz atakuambia leo baba nanilii kaamka kagomba gomba hapo ndani nadhani kuna kitu tu, kesho nitaenda kwa nani cjui nikaangalie, yani kawa kama mtabiri kitu kidogo ndani anakimbilia huko, nadhani ndio anaendaga ku renew cjui, kuna cku nilimkalisha chini kuongea nae juu ya haya mambo, nikamuuliza kwann anajitesa sana hana imani rohoni,nikamshauri apunguze basi kidogo coz hata mwanaume akidhurika na hayo madawa hatajua ni ipi imemdhuru, but haelewi! yani ndio imani yake hii aliyonayo kwamba mambo hayaendi maishani mpaka uende kwa "babu"
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mami huyu frnd wangu anaishi kwa wacwac kupitiliza, yani kila ki2 anajishtukia, ofcn mambo yakienda vcvyo atasema kuna m2 ananichezea, kila ki2 kashajiwekea ukombozi wake ni kwa "babu"...yani nimeshaongea nae mpaka nimechoka.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kuna dada mmoja alikuwa rafiki yangu wa karibu mpaka tukawa wapenzi wa kuchezeana kwa makubaliano maalumu kila mwenzie akipata wa kuoa au kuolewa tunavunja uhusiano wetu dada huyu alimpata jamaa mmoja alikuwa fundi mechanics anaishi kimara alinieleza kwa vile nilikuwa rafiki yake wa karibu sana akawa ananipa updates akaja kukugundua yule kaka anatumia mzizi kumpata tu alimpata kwa mzizi nayo waligundua ndugu zake yule binti kuwa amelishwa kitu si bure kutokana mahuba yalivyo kuwa yanapitiliza aliniambia aliitwa na dada yake Songea akapewa naye dose kurudi Kimara yule mme dose imekwisha ukaanza ugomvi wa mala kwa mala mpaka ikafikia kipindi jamaa wakawa wanapelekana polisi ilivyo fikia vile yule dada akampata mme mwingine ambaye walikubaliana kuwa wataoana na akawa tayari kumwache yule mechanics huyu kaka ni ofisa mmoja hapo Kibaha na anaishi hapo hapo huyu dada alikuwa anaenda kwa yule kaka wa kibaha lakini cha ajabu yule kaka kila akitaka kupata haki yake ya tunda la roho yaani penzi anakuta kule kumebana balaa kwa mke kila akipaka pate anashindwa yaani mahala pale panakuwa sealed bikra si bikra ilimtokea jamaa kama mala 3 hivi anashindwa kufaidi au kuzindua tunda lake cha kushangaza akirudi kwa mechanics jioni jamaa anakula kama kawaida yaani anamega kiulainiiiiiiii akajua pengine yule wa Kibaha anamatatizo lakini msumali alisema ulikuwa unasimama kama kawa lakini akitaka kupigilia anashindwa......yule dada akaniambia nikamwambia wasiliana na dada yako Songea akawasiliana naye akaambiwa njoo kwenda kule wakafanya manuva akafunguliwa kumbe yule fundi alimfunga asitoke nje baada ya kugundua muda wowote atatoswa basi dada huyu alipo rudi tu akammmwaga yule fundi na sasa ameolewa na huyu jamaa wa Kibaha na sasa wana mtoto mmoja maisha swaaaaaaaaaaaafi.
  Mizizi ipo jamani na ina fanya kazi kweli.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Unakosea inabidi tujadili ili watu tuwe makini maana kuna ndugu zetu na rafiki zetu wamezingilwa na haya maswala ya mizizi nani wa kuwaokoa kama sio mimi na wewe?
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  NGOJA tusikie...lazima watu watazileta tu humu.Vuta subira.
   
 18. M

  Msindima JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Makubwa jamani,Hivi ni miziz au dawa?sijaelewa hapo nifafanulieni jamani kama ni mizizi au dawa?
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mizizi aina ya dawa na si kila mzizi ni dawa ipo special inategemea unataka umwite mpenzi wako wa zamani au unataka umkamate mpenzi wako asikohoe au unataka mpenzi wako asiende kwa nyumba ndogo sasa kuna dawa za kienyeji aina ya mizizi au miti shamba.
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Fidel hiyo yako kali uwiii, kuziba/kuzibuliwa! kweli kuwa uyaone.
   
Loading...