Mitazamo tofauti siyo usaliti ni demokrasia

Mitazamo tofauti siyo usaliti ni demokrasia

kambitza

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2013
Posts
2,045
Reaction score
1,326
Siku hizi ukiwa tofauti kimawazo na mwenzako unabatizwa jina ( Msaliti ) kana kwamba unatumiwa na watu wengine.....

Mwenye busara mmoja, alisema Utofauti wa kimitazamo ni mbolea inayoleta ustawi imara unaoweza kuimarisha msingi katika jambo lolote.
Na Kugandamiza utofauti wa kimitazamo ni sawasawa na kujichimbia kaburi.

Bahati mbaya sana watu waoga wenye mamlaka (Hasa Afrika ) ndiyo vinara wa kuhakikisha utofauti wa kimitazamo unaonekana kama ni usaliti na wengi wao wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwaaminisha wafuasi wao na kuchochea hisia hizo kwa gharama yoyote..

Hebu jaribu kuwaza yule aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa marekani Collin Powell wa chama cha Republicun alivyojitokeza waziwazi kumpigia debe Rais Obama wa Democratic ingekuwa hapa ingekuwaje?? Wenzetu ni majemedari kwenye demokrasia waliibuka waliompinga lakini chama cha bwana mkubwa huyu kiliwachukulia wote kama wanatimiza wajibu wao wakidemokrasia na walitumia utofauti huu wa kimtazamo kuendelea kuimarisha chama chao.

Nchi yetu inasafari ndefu sana kufikia demokrasia ya kweli.

TUPINGANE ILA TUSIPIGANE
TUTOFAUTIANE ILA TUHESHIMIANE.
 
Usemayo sawa, lakini mtazamo tofauti ufanyike katika njia zinazokubalika kufuatana na kanuni za chama, na siyo kuandaa mipango ya kisirisiri.

Njia ya namna hii huwezi kuita mtazamo tofauti. Mtazamo tofauti toa mbele ya vikao kila mtu asikie -- unaogopa nini
?
 
Huo nao ni mtazamo tofauti...
 
Usemayo sawa, lakini mtazamo tofauti ufanyike katika njia zinazokubalika kufuatana na kanuni za chama, na siyo kuandaa mipango ya kisirisiri.

Njia ya namna hii huwezi kuita mtazamo tofauti. Mtazamo tofauti toa
mbele ya vikao kila mtu asikie -- unaogopa nini
?

Kuna mambo ya kuzungumzwa kwenye vikao na kuna mengine si ya
kuzungumzwa. Kwa hiyo kama watu wanataka kumuomba mwanachama fulani
agombee uongozi ulitaka waseme nn ndani ya kikao?

Kutumia usomi wao kufanya utafiti na SWOT analysis juu ya mtu wanayemtaka tena kwa siri bila kukiboa chama kuna tatizo gani? Labda kama kuna jingine
 
wewe umejuaje ni mtizamo tofauti. Kama huwezi kuuweka huo mtizamo hapa kama mfano si ulichosema kwa maana ya CDM ni upuuzi? Weka facts tukuelewe mfano. Zito alikula rushwa akaingia msituni kusambaratisha chama. Huu ulikuwa mtizamo wake. Kamati kuu ikaliona hili ikaamua kumtimua, na huu ndio mtizamo wake. Na kama ni suala la sera iko wazi mahali pekee ni kwenye kikao.
 
Nimeandika kuhusu demokrasia huko kwingine unanipeleka wewe.....
 
All time along, when a political party chases one of its leader, weakness comes and not strength. when Mrema left CCM, for the first time the party became vulnerable. NCCR took the torch only to go into wilderness after top leaders failing to embrace tenets of democracy. Zitto who has likened himself as a chicken on the pot has got his mother who are his voters and supporters who seem disenchanted, alienated and in disbelief. it means they may continue with him but they will never spport the party let' s say its presidential candidate. Is this not a loss to the party which needs every vote from anywhere possible to gain majority? What about Arfi? the bigger picture is that the real bone of contention in CDM is a limited democracy. History is vital. Also my experience with friends from moshi and arusha is that they are always communal but not democratic and they cannot even tolerate it. that is how they are brought up. if you are with them, they will want you to eat what they eat, drink by consensus and leave the place at the same time and anything different means unfriendship. it is an easy way of dealing with ordinary things but communalism always crumble when faced with advanced challenges especially democracy.
 
Historia? Historia haiwezi kusimama peke yake kama benchmark for right decision.
 
You have missed the backbone of this argument. the success of. any political party is hinged on respect to democratic principle or else that party becomes a religious cult.
 
Siku hizi ukiwa tofauti kimawazo na mwenzako unabatizwa jina ( Msaliti ) kana kwamba unatumiwa na watu wengine.....

Mwenye busara mmoja, alisema Utofauti wa kimitazamo ni mbolea inayoleta ustawi imara unaoweza kuimarisha msingi katika jambo lolote.
Na Kugandamiza utofauti wa kimitazamo ni sawasawa na kujichimbia kaburi.

Utofauti wa kimtizamo ktk nini au lipi? kwa muumini mzuri wa democrasia hutofautiana na wenzake ktk hoja za kutetea itakadi za vyama vyao na si ktk kuibua mambo yanayofarakanisha viongozi,mfano mzuri ni pale Rais Mao tse dong wa CCP ,alipomteua mtetea sera za kuchanganya uchumi wa kijamaa na kibepari ili kuleta mabadiliko kwa uchumi wa nchi,Deo xiao ping alikuwa ni mtetezi wa itikadi na si maslahi yake kama walivyo hawa wa kwetu wasaka tonge.alipambana na viongozi wenye miono ya karibu walimchukia na kumuona ni msaliti ktk kuujenga ujamaa wa kikomunist,Leo china imepaa kwa sababu yake.Tunataka kuwaona akina ZZK wenye mawazo kama ya rais Deng.

Kurumbana ndani ya chama kuwe ni ktk kuboresha ujenzi wa misingi bora kutetea itikadi ya chama na si kukosoa kusikovumilika kwa lengo la kujipatia umaarufu na vyeo,huku hakujengi chama bali kunabomoa.Wanasiasa wetu hususani wa vyama vya upinzani waonyeshe utofauti kati yao na watawala ili wanainchi wawatofautishe na kuwapa dhamana.
 
Kuna mambo ya kuzungumzwa kwenye vikao na kuna mengine si ya
kuzungumzwa. Kwa hiyo kama watu wanataka kumuomba mwanachama fulani
agombee uongozi ulitaka waseme nn ndani ya kikao?

Kutumia usomi wao kufanya utafiti na SWOT analysis juu ya mtu wanayemtaka tena kwa siri bila kukiboa chama kuna tatizo gani? Labda kama kuna jingine
Utafiti gani wa sirisiri tena wa kupinduana? huo unaitwa usaliti au uhaini.
 
Utafiti gani wa sirisiri tena wa kupinduana? huo unaitwa usaliti au uhaini.

Kama ulikuwepo huu ni uhaini tu, hauna jina mbadala. Tena hawa wanaopanga uhaini kwenye chama wakipata upenyo wanaweza panga uhaini kudondosha serikalini si wakuchukuliwa kirahisi. Hebu fikiria watu kama hawa wakutane na PK nini kitatengenezwa hapo?
 
Kuna mambo ya kuzungumzwa kwenye vikao na kuna mengine si ya
kuzungumzwa. Kwa hiyo kama watu wanataka kumuomba mwanachama fulani
agombee uongozi ulitaka waseme nn ndani ya kikao?

Kutumia usomi wao kufanya utafiti na SWOT analysis juu ya mtu wanayemtaka tena kwa siri bila kukiboa chama kuna tatizo gani? Labda kama kuna jingine
Mkuu umenena ukweli mtupu hawa viongozi wa chama wanalao moyoni waraka hauna matatizo kabisa ndio demokrasia ilivyo.
 
yaani mnataka mtu apende chama bila kupenda vyeo? chama kama hicho hakipo labda iwe famailia ambapo baba yupo tu. kama mwanachama anafikiri anaweza kuendesha chama vizuri kuliko waliopo lazima apewe fursa ya kugombea na ashindane na wenzake wanaotaka na akichaguliwa aongoze. akishindwa basi. na akishinda imlipe, aishi vizuru zaidi na nguvu zaidi. ndiyo maana ya demokrasia.
 
Kuna mambo ya kuzungumzwa kwenye vikao na kuna mengine si ya
kuzungumzwa. Kwa hiyo kama watu wanataka kumuomba mwanachama fulani
agombee uongozi ulitaka waseme nn ndani ya kikao?

Kutumia usomi wao kufanya utafiti na SWOT analysis juu ya mtu wanayemtaka tena kwa siri bila kukiboa chama kuna tatizo gani? Labda kama kuna jingine
Nimesoma ule ujumbe wote kwa hakika naungana na wewe mimi sikuona tatizo, tena mtu anayeitwa MM alikuwaanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi halali wa chama toka chini hadi juu! Najiuliza hii si ndio demokrasia what else jamani?
 
Kuna mambo ya kuzungumzwa kwenye vikao na kuna mengine si ya
kuzungumzwa. Kwa hiyo kama watu wanataka kumuomba mwanachama fulani
agombee uongozi ulitaka waseme nn ndani ya kikao?

Kutumia usomi wao kufanya utafiti na SWOT analysis juu ya mtu wanayemtaka tena kwa siri bila kukiboa chama kuna tatizo gani? Labda kama kuna jingine

Inawezekana kuwa kufanya kitu kama hicho kwa siri kitakuwa hakibomoi chama. Au unataka kutuamisha kuwa cheupe ni cheusi?
 
Back
Top Bottom