Salamu kutoka kusini! Kusini Kuchele
Naanza na malalamiko yangu kwa hii mitandao ya simu ya Tanzania!
Moja. Hivi kuna ulazima gani, pindi mtu anaacha kutumia line ya mtandao flani au anafariki dunia,halafu hiyo line ya simu anapewa mtu mwingine baada ya miezi kadhaa?
Hivi inakuaje aliyekua anatumia hiyo line ya simu, kaifanyia mambo ya utapeli, kauwa watu, kaiba, kakaba watu hadi kufa, kabaka na matukio mengine ya kuogofya, hamuoni kwamba huyo mtu anakua kwenye kesi ambazo hazimuhusu?
Mbili! Nimechukua line ya mtandao flani hivi,kila siku napigiwa simu na Bank x,wanahitaji marejesho ya mkopo wao,ambao nilichukua, sasa mbona Mimi sijawahi chukua mkopo kwenye hiyo bank?
Kumbe aliyekua anatumia line ya hii simu ndo anayetafutwa! Mara nitumiwe sms za mapenzi! Mpenzi wangu siku hizi hata hunijali, hata pesa za matumizi hunitumii kabisa! Kuna siku kidogo nife, nilisoma, sms inayosema salio la kiasi flani, limetolewa kwenye account yako! Haaa nikatahamaki, kumbe ni hii line ya ajabu!
Tatu! Mnavunja ndoa za watu, hivi kweli nani ataelewa kwamba, hii sms sio ya kwangu,ni yatu mwingine?
Nne! Hivi mtu alifariki, na kwenye line zake kuna pesa,hua zinaenda wapi hizi pesa? Jamani tunapigwa mchana kweupe! Natamani kujua hii kitu!